LAZIMA NISEME
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 232
- 260
TUMOKINOI MOLLEL SAMAITO (Francis Samaiko - PICHANI) aliwekwa mahabusu kwa kosa la uvunjifu wa amani kwa mujibu wa sheria mnamo tarehe 30/11/2023.
madini ya rubi
Hakuna mgogoro wowote kati ya mmiliki wa leseni (kijiji cha les mundarara) na mwekezaji huyo (northern crystal ruby limited).
HAKUNA USHAHIDI wowote unaonesha kuwa Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Longido amekuwa akiegemea upande wowote wa mkataba huo na badala yake amekuwa akisimamia maslahi ya pande zote mbili.
MHE. MKUU WA WILAYA ya Longido alifanya kikao na viongozi na kuwasisitiza kusimamia rasilimali zilizopo kwenye kata hiyo na kujenga mahusiano mazuri na wawekezaji.
TUMOKINOI MOLLEL SAMAITO aliingilia kwenye kikao hicho bila kuwa na mwaliko wowote katika kikao cha Mkuu wa Wilaya na viongozi wa Serikali.
Tumokinoi Mollel Samaito aliwekwa mahabusu katika kituo cha polisi longido kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha sheria ya tawala za mikoa.