Dkt. Mollel: Wabadhirifu wa fedha za Dawa za MSD kuchukuliwa hatua na TAKUKURU

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 31 leo Mei 23, 2023.

Wabadhirifu wa Dawa na Bidhaa za Afya Kushughulikia
Serikali imesema inachukua hatua mbalimbali kushughulikia changamozo za Ubadhilifu wa Dawa na Bidhaa za Afya Kushughulikia kwa kujenga uwazi zaidi kwenye makabidhiano ya bidhaa hizo kwa kuwapa Wabunge na Wakuu wa Wilaya Nyaraka za Makabidhiano ya Bidhaa hizo.

Pia, inaimarisha mifumo wa usimamizi wa bidhaa za afya ikiwemo kutumia mifumo wa kielektroniki na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara.

Haya yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel Bungeni wakati akijibu Swali la Mbunge wa Kisesa, Lugaha Mpina alietaka kufahamu jitihada zinazofanyika ili kudhibiti dawa na bidhaa za afya Nchini.

Mbunge huyo pia ametaka kufahamu ni namna gani Serikali inaiwezesha Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika kutekeleza majukumu yake na kuongeza ufanisi, namna ilivyochukua hatua kwa wabadhirifu waliotajwa na CAG pia uwepo wa malimbikizo ya madeni yenye thamani ya zaidi ya bilioni 259.

Dkt. Mollel amesema pia TAKUKURU inashughulikia orodha ya watu waliotajwa kwenye ubadhirifu wa MSD na mambo yakikaa sawa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

Amesema pia MSD kujiendesha kama Procurement Entity na sio kama bohari ya dawa hivyo suala la kuongezewa mtai litazingatiwa.
 
Bunge hili lililopora chaguzi limejaa Mapaka,labda ufuatilie wewe pamoja na mke wako

mkutano wa porojo porojo na posho posho wa kupiga pesa za watanzania. Pia moleli anatabia za uzushi uzushi sana, muwe nae makini
 
Blah blah miyeyusho jazz band

Maigizo bongo movie tu

Ze comedy show + futuhi

Ova
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 31 leo Mei 23, 2023.

Wabadhirifu wa Dawa na Bidhaa za Afya Kushughulikia
Serikali imesema inachukua hatua mbalimbali kushughulikia changamozo za Ubadhilifu wa Dawa na Bidhaa za Afya Kushughulikia kwa kujenga uwazi zaidi kwenye makabidhiano ya bidhaa hizo kwa kuwapa Wabunge na Wakuu wa Wilaya Nyaraka za Makabidhiano ya Bidhaa hizo.

Pia, inaimarisha mifumo wa usimamizi wa bidhaa za afya ikiwemo kutumia mifumo wa kielektroniki na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara.

Haya yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel Bungeni wakati akijibu Swali la Mbunge wa Kisesa, Lugaha Mpina alietaka kufahamu jitihada zinazofanyika ili kudhibiti dawa na bidhaa za afya Nchini.

Mbunge huyo pia ametaka kufahamu ni namna gani Serikali inaiwezesha Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika kutekeleza majukumu yake na kuongeza ufanisi, namna ilivyochukua hatua kwa wabadhirifu waliotajwa na CAG pia uwepo wa malimbikizo ya madeni yenye thamani ya zaidi ya bilioni 259.

Dkt. Mollel amesema pia TAKUKURU inashughulikia orodha ya watu waliotajwa kwenye ubadhirifu wa MSD na mambo yakikaa sawa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

Amesema pia MSD kujiendesha kama Procurement Entity na sio kama bohari ya dawa hivyo suala la kuongezewa mtai litazingatiwa.
Hizi porojo muwe mnawauzia wajinga
 
Back
Top Bottom