nyamadoke75
Member
- Apr 1, 2020
- 87
- 280
Wadau wa Maendeleo na wasomi wilayani Longido wamejipanga kuishtaki mahakamani Halmashauri ya Longido kwa ubadhirifu wa fedha za umma baada ya kubaini kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri ,Stephen Ulaya na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Simon Oitesoi ndio chanzo cha uchochoro wa upotevu wa fedha za Umma.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ,Mkurugenzi huyo anadaiwa kushinikiza baadhi ya miradi hewa kutengewa fedha zinazomnufaisha yeye na Mwenyekiti wa Halmashauri ikiwemo upotevu wa sh.Million 81 fedha ya ujenzi wa kituo cha afya Ketumbeine pamoja na sh.Million 17 mradi hewa zahanati ya Irikaswa.
Katika hatua nyingine halmashauri hiyo imekua ikiidhinisha fedha kuelekezwa kwenye miradi iliyoibuliwa na wananchi na baadaye kurudi nyuma na kuzitaka fedha hizo kinyume na taratibu ikiwemo kwenye miradi ya afya na Elimu.
Hivi karibuni halmashauri hiyo ilitenga kiasi cha sh million 35 kwa ajili ya kukamilisha zahanati ya Naadare iliyopo kata ya ilorienito tarafa ya Ketumbeine lakini baada ya fedha hizo kufika kwenye Account ya kijiji Mkurugenzi alitoa maelekezo ya kulipwa mzabuni hewa anayeishi mto wa mbu ambaye hata kamati ya ujenzi haimfahamu.
Wakili wa kujitegemea ,Samaito Laizer amesema tunahitaji kufahamu ukweli na Tunahitaji kuona watu Wakiwajibika Kwa matendo yao,ndio maana nimechukua siku nzima,kupitia sheria na kuufahamisha Umma haki zao Ili wawe na Msimamo na wasitishwe Kwa lolote.
Alisema wamejipanga kufungua Kesi Mahakama Kuu, High Court Arusha,tunajua baadhi ya maazimio yalopitishwa na Baraza la Madiwani yamekuwa paralyzed,hatazingatiwi Wala kutekelezwa,pamoja na ukiukwaji mkubwa wa Kanuni za makusanyo na Uthibiti wa Matumizi wa FEDHA.
.....
Pichani Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido, Steven Ulaya kushoto na mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Simon Oitesoi.