Majibu kwa hotuba ya Lissu Bungeni

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,970
45,848
Ningependa kujibu hoja ya Lisu kuhusina na kauli aliyoitoa kwamba kwakua Mpaka sasa Rais Hakutoa Tangazo la serikali ili kukasimisha majukumu ya mawaziri kwa mawaziri waliopo kwamba kunafanya maamuzi yaliyotolewa na mawaziri kabla ya kutoa Tangazo hilo kua batili, kua kauli hiyo sio sahihi na kwamba imetolewa kwa lengo la kisiasa tu la kupotosha jamii kutokana na ukweli ulipo, nazungumza hivyo kutokana na maelezo nitakayoyatoa hapa;

1. Ni kweli kwamba kama hakuna waziri,Rais pekee ndie anakua waziri wa wizara husika na ni kweli kwamba kulingana na sheria za nchi yeye ndiye waziri namba moja, hivyo anapoteua mbunge yoyote yule kua waziri moja kwa moja anampa mbunge huyo mamlaka yake kama waziri namba moja, na Utaratibu wa kisheria ni kwamba waziri anapoteuliwa na kukubali uteuzi na kuapishwa kama Waziri anakua na mamlaka kamili kuhusiana na wizara husika kama angalikua nayo Rais. Tafsiri hii inapatikana kutokana na Kifungu cha 4 kinachotoa tafsiri; Cha sheria ya Tafsiri, sura ya kwanza ya sheria za Nchi, kama ilivyohaririwa mwaka 2002 inasema ( Section 4 of the Interpretation of Laws Act, Cap 1 , R.E 2002);

" Minister has the meaning given in Section 9 of this Act, in addition it includes the Vice President, the Prime Minister, andthe Minister, means the Minister Responsible for the matter in question and includes the Deputy Minister for the timem being performing the functions of that Minister or, if there is no minister responsible for the matter in question, mans the President"

Baada ya kuangalia Tafsiri ya sheria kuhusu nini Maana ya Waziri ni vyema tukaangalia namna waziri anavyoteuliwa,

Ibara ya 55 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977, Sura ya Pili ya sheria ya Nchi inasema ( The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 Cap 2 of the Laws of the United Republic of Tanzania)

55.-(1) All Ministers who are members of Cabinet by virtue of Article 54 shall be appointed by the President after consultation with the Prime Minister and they shall be responsible for such offices as the President may, from time to time, by writing under his hand and the Public Seal.

(2) In addition to the Ministers referred to in subarticle (1) the President may, after consultation with the Prime Minister, appoint Deputy Ministers. All Deputy Ministers shall not be members of Cabinet.

(3) The President may appoint any number of Deputy Ministers who shall assist Ministers in the discharge of their duties and functions. i

(4) All Ministers and Deputy Ministers shall be appointed from among Members of Parliament.

(5) Notwithstanding the provisions of subarticle (4), in the event that the President is obliged to appoint a Minister or a Deputy Minister after dissolution of Parliament then he may appoint any person who was a Member of Parliament


Tafsiri ya Ibara ya katiba hapo juu ni kua Waziri anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika majukumu ya uwaziri wake baada ya Rais kushauriana na Waziri Mkuu.

Waziri mteule atakua na mamlaka ya uwaziri katika wizara husika baada ya kupewa hati ya uteuzi yenye mhuri na sahihi ya Rais wa Jamhuri.

Ili waziri awe waziri kamili baada ya uteuzi wake, inabidi aape mbele ya Rais kiapo cha utii na kutimiza wajibu wa uwaziri wa wizara husika aliyoteuliwa; Katiba ya jamhuri ya Muungano Ibara ya 56 inasema;

Art. 56.A Minister or a Deputy Minister shall not assume office until he has first taken and subscribed before the President, the oath of allegiance and such other oath relating to the execution of the functions of his office as may be prescribed by an Act of Parliament.

Tafsiri yake ni kwamba Waziri hatakua waziri kamili mpaka atakapofanya kiapo cha utii mbele ya rais na kiapo cha kutimiza majukumu ya uwaziri mbele ya Rais.

Kwa kuangalia Maneno yaliyomo katika vifungu vya sheria tajwa hapo juu, utaona kua waziri anapata nguvu kamili za uwaziri baada ya kuapa mbele ya rais na kupewa hati ya uteuzi yenye sahihi na mhuri wa rais.

Kutokana na hoja ya Lisu kua mawaziri wamefanya majukumu yao kinyume na utaratibu wa sheria na hivyo kufanya maamuzi yao kua batili kwa kua hakuna tangazo la serikali ya kukasimisha majukumu ya uwaziri, kauli hiyo inatupeleka kwenye mjadala wa JE Waziri anakua waziri baada ya kuapishwa ama baada ya tangazo la serikali?

Wakati tukitafuta majibu ya Swali lililojitokeza ni vyema kwanza tukapata tafsiri ya nini maana ya Tangazo la Serikali au Government Notice;

Sheria ya Tafsiri ya Sheria ama ( The Interpretation of Laws Act) inatupa majibu, katika kifungu cha 4 kinasema;

" Government Notice means any subsidiary legislation made by the President, a minister or other public officer or authority pursuant to the power conferred by any Act"

Nini maana ya Subsidiary legislation;

Kifungu cha 4 cha sheria Tajwa kinasema;

" Subsidiary legislation means any order, proclamation, rule,rule of court,regulation,notice,by-law, or instrument made under any Act, or any other lawful authority"

Kifupi baada ya kupitia kifungu cha tafsiri ya sheria, utaona kwamba, maana ya tangazo la serikali ni kua ni wakara unaotokana na maamuzi, au amri au tangazo kwa uma, kutokana na sheria zilizopo au mamlaka yoyote husika.

Ili tuweze kupata maana ya Tangazo la serikali kulingana na hoja ya lisu tunapata maana kwamba, Rais alipaswa kutoa waraka kwa uma kukasimisha mamlaka ya uwaziri kwa baadhi ya wateule"

Sasa tuangalie hoja zifuatazo; je waziri anasita kua waziri kwakua hakutangazwa kwa uma kupitia waraka? Jibu ni hapana kwakua Sheria za nchi zinasema kwamba Waziri atakua waziri kamili mara baada tu ya kuapa mbele ya rais na kupata hati ya uteuzi yenye mhuri na sahihi ya Rais.

Swali la kujiuliza ni JE? kuna waziri yoyote katika serikali ya sasa anayefanya majukumu yake bila ya kua na hati ya uteuzi wala bila kuapa kiapo cha utii mbele ya Rais? Jibu ni Hakuna.

Tangazo la rais la kukasimisha mamlaka ya uwaziri ni taratibu tu za kiserkali ambazo tumejiwekea ili kuweka mambo kua kitaalam zaidi na kukosekana kwa tangazo hilo hakumfanyi waziri kutokua waziri kwani jambo muhimu ambalo linahitajika ni KIAPO NA HATI YA UTEUZI.

Hivyo kwa hoja hizo, hoja ya Lisu inakosa uhalali kisheria na ni ya kisiasa inayopaswa kupuuzwa.
 
Wewe ni jurisprudent charlatan huwezi kukopi mavifungu na kuyapa tafsiri za english to swahili halafu ukaishia kusema huo ndio uhalali...
Sheria husika ipo katika lugha ya kiingereza, weka tafsiri yako ambayo wewe unaona ni sahihi, ni sheria hizo hizo ndizo anazitumia lisu kujenga hoja yake, nimeweka majibu yangu, which is subject to discussions and kama kuna clarifications mahali unaweza fanya,
 
Halafu hii kutafuta umaalufu huwa sometimes Ina waharibia vibaya..yaani ukawa sasahiv wanatapatapa hawana pakushika. Tuna waheshimu lkn itafika mahali tutaanza kuwadharau maana mmekosa hoja zenye mshiko..muache rais afanye kazi.
 
Umeanisha vizuri sana. Ni kweli kwamba mawaziri huwa mawaziri kamili baada ya kula kiapo mbele ya rais.
Lakini, kabla hawajaanza kutimiza majukumu yao Umma unapaswa kutaarifiwa kwanza kupitia tangazo la serikali kama sheria ilivyoainisha.
Hivyo basi, uwaziri wao kwa nafasi ni halali lakini, bado hawajatambulishwa kwa umma ili wayaanze rasmi majukumu yao. Kitendo cha kutangazwa kwa umma ndiyo description kwao.

N.B
Haya uliyoyaket si majibu kwa hoja ya Lisu bali ni mjadala juu ya hija ya Lissu.
 
Wewe ni jurisprudent charlatan huwezi kukopi mavifungu na kuyapa tafsiri za english to swahili halafu ukaishia kusema huo ndio uhalali...
Kosoa alipokosea usiletelongolongo wasomi tumemsoma, sheria za nchi yetu nyingi ziko kwenye lugha ya malkia.
 
Asante Antipas Lissu...Afadhali mtoa mada amesema ukweli,kuwa "Wakati wanaendelea kutafuta majibu sahihi ya hoja ya Lissu"...walau haya ndio "majibu" ya mwanzo ya wanaotakiwa kujibu
Huku jopo jingine likijichimbia ndani kuendelea kutafuta majibu kumjibu mtu mmoja
Lissu huwa namuelewaa sana...hana unafiki wala kujipendekeza
 
Umeanisha vizuri sana. Ni kweli kwamba mawaziri huwa mawaziri kamili baada ya kula kiapo mbele ya rais.
Lakini, kabla hawajaanza kutimiza majukumu yao Umma unapaswa kutaarifiwa kwanza kupitia tangazo la serikali kama sheria ilivyoainisha.
Hivyo basi, uwaziri wao kwa nafasi ni halali lakini, bado hawajatambulishwa kwa umma ili wayaanze rasmi majukumu yao. Kitendo cha kutangazwa kwa umma ndiyo description kwao.

N.B
Haya uliyoyaket si majibu kwa hoja ya Lisu bali ni mjadala juu ya hija ya Lissu.
Mkuu kwa mantiki hiyo kutokutambulishwa kupitia waraka hakumfanyi waziri kutokua waziri wala alichokifanya kua batili.

Hayo ni majibu yangu, na kama mjadala utakua umeanza well and good tujadiliane kuona usahihi ni upi badala ya kupotoshana.
 
mkuu umeandika kwa kirefu sana bila kupepesa macho umeandika pumba bora ungeandika habari za tramp
 
Hoja ya Lissu bado ina mashiko...suala la kukasimisha mamlaka lipo kisheria na si hiyari ya Magufuli.
 
Back
Top Bottom