Majibu kwa hotuba ya Lissu Bungeni

Majibu kwa hotuba ya Lissu Bungeni

Mleta mada naona hutaki kuelewa,lengo lako sio kujifunza bali kupotosha kwa kila namna kwa manufaa yako binafsi!Pengine labda hujawahi kuona hata muundo huo wa waraka wa ukasimishaji wa madaraka!
Waraka huo unaeleza yale ambayo waziri anatakiwa kuyafanya,hii ni sawa na job discription!Mamlaka haya ya kazi hupewa kisheria na kwa utaratibu ambao umewekwa kisheria!Mawaziri wanaweza wakawa halali ila maamuzi waliyofanya bila kupewa mamlaka kisheria yakawa batili!
Uweke hapa huo waraka, pia umekuja na jambo jingine ambalo sio vibaya kulijadili hivi ni job description inayompa mtu nafasi ya ajira au employment contract?
Nasema hivyo kwa maana kwangu mimi nachukulia kiapo kama ni employment contract...
 
Ni haki yangu ya kikatiba kutoa maoni kuhusiana na jambo lolote lile linaloihusu serikali au bunge, As long as i am exercising my constitutional right, hayo mengine uliyoyazungumza kwangu hayana nafasi, and on top of everything the forum allows each and every thing to be discussed here, as long as sheria haijavunjwa. I have been here and done this before. Wewe huna mamlaka yoyote ya kuninyima mimi kutoa maoni yangu. Kama hujapenda nilichoandika. Acha wengine wajadili.
Imekugusa eh?

Hujajiridhisha na ulichoandika ndiyo issue hapa.

Kama uko sahihi basi na mimi nina haki ya kikatiba na kisheria kama uliyonayo. Kama huridhiki na nilchoandika ungenipuuza ningekuelewa kuwa unaelewa

Unaandika siasa unajidai ni sheria kwa kujipima na Lissu. Halafu unataka tujadiri. Nakushauri bure jiridhishe kwa kutafakari kwanza sisi wasomaji wako humu JF pia tuna haki ya kukujibu kwa tafakuri zetu.

Lissu ni level nyingine kwako, kwa CCM na serikali yake. Subiri majibu ya serikali Lissu hajapotoka hatapotoka kwenye masuala ya kisheria. Usitafute promo za kisiasa na kisheria kwa kujipima na Lissu.
 
Huwezi kupangua hoja za mwanasheria Msomi aliyebobea kama Tundu Lisu kwa hoja nyepesinyepesi na quotations mbili tatu,inabidi ujiandae hasa na nondo za uhakika otherwise una display ignorance yako
Haha, Huamini kua alichosema lisu kua sio sahihi au tatizo lako ni Jina lake. Unguli wake unatokana na nini labda, naomba uniwekee kesi yoyote ile aliyoshiriki huyu Nguli ambayo imetengeneza Precedent katika sheria zetu hapa nchini nguli awe yeye na kina Lakha utawaitaje?
 
Imekugusa eh?

Hujajiridhisha na ulichoandika ndiyo issue hapa.

Kama uko sahihi basi na mimi nina haki ya kikatiba na kisheria kama uliyonayo. Kama huridhiki na nilchoandika ungenipuuza ningekuelewa kuwa unaelewa

Unaandika siasa unajidai ni sheria kwa kujipima na Lissu. Halafu unataka tujadiri. Nakushauri bure jiridhishe kwa kutafakari kwanza sisi wasomaji wako humu JF pia tuna haki ya kukujibu kwa tafakuri zetu.

Lissu ni level nyingine kwako, kwa CCM na serikali yake. Subiri majibu ya serikali Lissu hajapotoka hatapotoka kwenye masuala ya kisheria. Usitafute promo za kisiasa na kisheria kwa kujipima na Lissu.
You are getting personal this will not take you anywhere. Haha.
 
Ningependa kujibu hoja ya Lisu kuhusina na kauli aliyoitoa kwamba kwakua Mpaka sasa Rais Hakutoa Tangazo la serikali ili kukasimisha majukumu ya mawaziri kwa mawaziri waliopo kwamba kunafanya maamuzi yaliyotolewa na mawaziri kabla ya kutoa Tangazo hilo kua batili, kua kauli hiyo sio sahihi na kwamba imetolewa kwa lengo la kisiasa tu la kupotosha jamii kutokana na ukweli ulipo, nazungumza hivyo kutokana na maelezo nitakayoyatoa hapa;

1. Ni kweli kwamba kama hakuna waziri,Rais pekee ndie anakua waziri wa wizara husika na ni kweli kwamba kulingana na sheria za nchi yeye ndiye waziri namba moja, hivyo anapoteua mbunge yoyote yule kua waziri moja kwa moja anampa mbunge huyo mamlaka yake kama waziri namba moja, na Utaratibu wa kisheria ni kwamba waziri anapoteuliwa na kukubali uteuzi na kuapishwa kama Waziri anakua na mamlaka kamili kuhusiana na wizara husika kama angalikua nayo Rais. Tafsiri hii inapatikana kutokana na Kifungu cha 4 kinachotoa tafsiri; Cha sheria ya Tafsiri, sura ya kwanza ya sheria za Nchi, kama ilivyohaririwa mwaka 2002 inasema ( Section 4 of the Interpretation of Laws Act, Cap 1 , R.E 2002);

" Minister has the meaning given in Section 9 of this Act, in addition it includes the Vice President, the Prime Minister, andthe Minister, means the Minister Responsible for the matter in question and includes the Deputy Minister for the timem being performing the functions of that Minister or, if there is no minister responsible for the matter in question, mans the President"

Baada ya kuangalia Tafsiri ya sheria kuhusu nini Maana ya Waziri ni vyema tukaangalia namna waziri anavyoteuliwa,

Ibara ya 55 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977, Sura ya Pili ya sheria ya Nchi inasema ( The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 Cap 2 of the Laws of the United Republic of Tanzania)

55.-(1) All Ministers who are members of Cabinet by virtue of Article 54 shall be appointed by the President after consultation with the Prime Minister and they shall be responsible for such offices as the President may, from time to time, by writing under his hand and the Public Seal.

(2) In addition to the Ministers referred to in subarticle (1) the President may, after consultation with the Prime Minister, appoint Deputy Ministers. All Deputy Ministers shall not be members of Cabinet.

(3) The President may appoint any number of Deputy Ministers who shall assist Ministers in the discharge of their duties and functions. i

(4) All Ministers and Deputy Ministers shall be appointed from among Members of Parliament.

(5) Notwithstanding the provisions of subarticle (4), in the event that the President is obliged to appoint a Minister or a Deputy Minister after dissolution of Parliament then he may appoint any person who was a Member of Parliament


Tafsiri ya Ibara ya katiba hapo juu ni kua Waziri anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika majukumu ya uwaziri wake baada ya Rais kushauriana na Waziri Mkuu.

Waziri mteule atakua na mamlaka ya uwaziri katika wizara husika baada ya kupewa hati ya uteuzi yenye mhuri na sahihi ya Rais wa Jamhuri.

Ili waziri awe waziri kamili baada ya uteuzi wake, inabidi aape mbele ya Rais kiapo cha utii na kutimiza wajibu wa uwaziri wa wizara husika aliyoteuliwa; Katiba ya jamhuri ya Muungano Ibara ya 56 inasema;

Art. 56.A Minister or a Deputy Minister shall not assume office until he has first taken and subscribed before the President, the oath of allegiance and such other oath relating to the execution of the functions of his office as may be prescribed by an Act of Parliament.

Tafsiri yake ni kwamba Waziri hatakua waziri kamili mpaka atakapofanya kiapo cha utii mbele ya rais na kiapo cha kutimiza majukumu ya uwaziri mbele ya Rais.

Kwa kuangalia Maneno yaliyomo katika vifungu vya sheria tajwa hapo juu, utaona kua waziri anapata nguvu kamili za uwaziri baada ya kuapa mbele ya rais na kupewa hati ya uteuzi yenye sahihi na mhuri wa rais.

Kutokana na hoja ya Lisu kua mawaziri wamefanya majukumu yao kinyume na utaratibu wa sheria na hivyo kufanya maamuzi yao kua batili kwa kua hakuna tangazo la serikali ya kukasimisha majukumu ya uwaziri, kauli hiyo inatupeleka kwenye mjadala wa JE Waziri anakua waziri baada ya kuapishwa ama baada ya tangazo la serikali?

Wakati tukitafuta majibu ya Swali lililojitokeza ni vyema kwanza tukapata tafsiri ya nini maana ya Tangazo la Serikali au Government Notice;

Sheria ya Tafsiri ya Sheria ama ( The Interpretation of Laws Act) inatupa majibu, katika kifungu cha 4 kinasema;

" Government Notice means any subsidiary legislation made by the President, a minister or other public officer or authority pursuant to the power conferred by any Act"

Nini maana ya Subsidiary legislation;

Kifungu cha 4 cha sheria Tajwa kinasema;

" Subsidiary legislation means any order, proclamation, rule,rule of court,regulation,notice,by-law, or instrument made under any Act, or any other lawful authority"

Kifupi baada ya kupitia kifungu cha tafsiri ya sheria, utaona kwamba, maana ya tangazo la serikali ni kua ni wakara unaotokana na maamuzi, au amri au tangazo kwa uma, kutokana na sheria zilizopo au mamlaka yoyote husika.

Ili tuweze kupata maana ya Tangazo la serikali kulingana na hoja ya lisu tunapata maana kwamba, Rais alipaswa kutoa waraka kwa uma kukasimisha mamlaka ya uwaziri kwa baadhi ya wateule"

Sasa tuangalie hoja zifuatazo; je waziri anasita kua waziri kwakua hakutangazwa kwa uma kupitia waraka? Jibu ni hapana kwakua Sheria za nchi zinasema kwamba Waziri atakua waziri kamili mara baada tu ya kuapa mbele ya rais na kupata hati ya uteuzi yenye mhuri na sahihi ya Rais.

Swali la kujiuliza ni JE? kuna waziri yoyote katika serikali ya sasa anayefanya majukumu yake bila ya kua na hati ya uteuzi wala bila kuapa kiapo cha utii mbele ya Rais? Jibu ni Hakuna.

Tangazo la rais la kukasimisha mamlaka ya uwaziri ni taratibu tu za kiserkali ambazo tumejiwekea ili kuweka mambo kua kitaalam zaidi na kukosekana kwa tangazo hilo hakumfanyi waziri kutokua waziri kwani jambo muhimu ambalo linahitajika ni KIAPO NA HATI YA UTEUZI.

Hivyo kwa hoja hizo, hoja ya Lisu inakosa uhalali kisheria na ni ya kisiasa inayopaswa kupuuzwa.
Acha kituko! Hivi CCM mmeanza lini kujibu hoja za Mh LISSU? Tangu LISSU aingie bungeni sijawahi kuona mbunge yeyote akijibu au akipangua hoja za Lissu! Ile ni namba nyingine, hoja yake huwezi kuijibu kirahisi hivyo! Wewe uache vituko sio fundi wa kufafanua vifungu vya sheria zaidi ya kukopa tu.
 
Mimi sio mwanasheria lakini naomba nifananishe ufafanuzi wako na mchakato wa uchaguzi

uteuzi mgombea Urais katika chama husika = rais kushauriana na waziri mkuu juu ya uteuzi wa waziri

uteuzi/kupitishwa kwa mgombea na tume ya uchaguzi = Rais kutamka baraza la mawaziri

tume kumtangaza mshindi wa uchaguzi = Rais kuwaapisha mawaziri

Tume kumtangza mshindi wa Urais kwenye GN = Rais kumtangaza waziri/baraza GN

Kuapishwa kwa rais = Mamlaka kamili ya waziri



Ukiangalia kwenye mtiririko huo hapo juu upo kisheria na unafuata logic fulani na ni lazima kimoja kifanyike kabla ya kingine kuruka kwa kimojawapo ama kutotekeleza moja ya hivyo kinafanya vyote kuwa batili ama incomplete.

Na ndio maana kabla ya kutamka lazima mtoa tangazo aseme anatoa tamko hilo kwa mamlaka ipi.


Leo hii Lowassa akisema yeye ni rais moja wapo ya vifungu vitambana ni pamoja na GN ya tume iliyotolewa
na kama kuna taratibu zilikiukwa zinaweza kutumiwa kama sehemu ya ukiukwaji wa sheria na hata kubatilisha mammuzi yaliyofanywa.


hivyo GN ni sehemu ya mchakato wa kumpata waziri na muundo wa uongozi kwa ujumla ukiukwaji wake unafanya upatikanaji wa mawaziri kuwa incomplete ama haramu

Ni mimi Bush lawyer
 
hahahahhahah....CCM mnajifariji na Copy paste
 
Mimi nadhani kama kweli haya ni majibu ya serikali, basi huku ni kujichanganya kusiko kwa kawaida.

Tunakumbuka hoja hii hii ilijitokeza wakati wa mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na hata kambi ya upinzani bungeni kususia au kushindwa kutoa hotuba yao na wakatoka ndani ya Bunge.

Katika majibu ya PM juu ya hili, alisema kuwa serikali imeshaandaa taratibu za kisheria juu ya hoja hii na wakati wowote hilo lingetimizwa. Kwa lugha nyingine ni kwamba PM alikiri kuwa ipo kasoro ktk hilo na serikali itarekebisha. Leo kumetokea nini tena??

Na mwisho kabisa, niulize serikali, kwani kuna ugumu gani wa kuandaa na kutekeleza matakwa hayo ya kisheria na kikatiba hata kuendeleza malumbano ambayo kwa mtazamo wangu naona kama hayana maana wala msingi wowote?

Na je, kwani huyu Rais ni tofauti na marais wengine waliomtangulia kiasi ambacho yeye anaongozwa na sheria tofauti, katiba tofauti na taratibu tofauti?......Mbona hatuwasomi vyema hawa watu? Wana matatizo gani eti? Mizuka au ni nini hasa??
 
mkuu umeandika kwa kirefu sana bila kupepesa macho umeandika pumba bora ungeandika habari za tramp
Mkuu tuwekee hizo habar za tramp..hapa kama huna kitu cha kucoment si lazma wakati mwingne unapita kama huoni
 
Hoja ya Lissu bado ina mashiko...suala la kukasimisha mamlaka lipo kisheria na si hiyari ya Magufuli.

Yes, nakubaliana na wewe mkuu. Na si tu suala la kusema kwa sababu hiki hakijafanyika na hata hivi tulivyofanya ni sawa tu!!!

Hawa wanajua na wanakiri kuwa lipo tatizo, lakini wameamua kufa na tai zao shingoni!!

I hope they are working on it silently in their inner rooms. Si ajabu baada ya siku mbili au tatu ukaona kasoro hizo zimerekebishwa kimya kimya!!
 
Umeanisha vizuri sana. Ni kweli kwamba mawaziri huwa mawaziri kamili baada ya kula kiapo mbele ya rais.
Lakini, kabla hawajaanza kutimiza majukumu yao Umma unapaswa kutaarifiwa kwanza kupitia tangazo la serikali kama sheria ilivyoainisha.
Hivyo basi, uwaziri wao kwa nafasi ni halali lakini, bado hawajatambulishwa kwa umma ili wayaanze rasmi majukumu yao. Kitendo cha kutangazwa kwa umma ndiyo description kwao.

N.B
Haya uliyoyaket si majibu kwa hoja ya Lisu bali ni mjadala juu ya hija ya Lissu.
Hata ukisoma kwa makini hoja ya Lissu, imejikita katika hichi ulichoeleza. Nadhan Lissu alikua anakumbusha sheria zinataka nini baada ya Kiapo na mambo mengine kadhaa, basi issue iwe gazzetted kama sheria inavyotaka. Nilivyomuelewa Lissu hapingi kuwa hao Waheshimiwa siyo Mawaziri la hasha, amekumbusha kupewa Job Description,sioni kama ni jambo baya!
 
Mimi nadhani kama kweli haya ni majibu ya serikali, basi huku ni kujichanganya kusiko kwa kawaida.

Tunakumbuka hoja hii hii ilijitokeza wakati wa mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na hata kambi ya upinzani bungeni kususia au kushindwa kutoa hotuba yao na wakatoka ndani ya Bunge.

Katika majibu ya PM juu ya hili, alisema kuwa serikali imeshaandaa taratibu za kisheria juu ya hoja hii na wakati wowote hilo lingetimizwa. Kwa lugha nyingine ni kwamba PM alikiri kuwa ipo kasoro ktk hilo na serikali itarekebisha. Leo kumetokea nini tena??

Na mwisho kabisa, niulize serikali, kwani kuna ugumu gani wa kuandaa na kutekeleza matakwa hayo ya kisheria na kikatiba hata kuendeleza malumbano ambayo kwa mtazamo wangu naona kama hayana maana wala msingi wowote?

Na je, kwani huyu Rais ni tofauti na marais wengine waliomtangulia kiasi ambacho yeye anaongozwa na sheria tofauti, katiba tofauti na taratibu tofauti?......Mbona hatuwasomi vyema hawa watu? Wana matatizo gani eti? Mizuka au ni nini hasa??
Haya sio majibu ya serikali mkuu, haya ni maoni yangu binafsi kutokana na kile kilichozungumzwa na Lisu Bungeni nimeandika kutokana na namna nilivyopitia vufungu vya sheria nilivyoviweka, i might or might not be right. as well as he might or might not be right.
 
naona umepewa uje kupost uku. Hongera umepata buku 7 yako
 
Huo ni mtazamo wako ambao haujaleta kajibu ya hoja yangu hoja yangu imejijkita katika kujibu hoja ya Lisu kua kwakua hakuna mwongozo wa serikali wa kukasimisha madaraka hivyo yaliyofanywa na mawaziri ni batili, nimejibu kua huo sio usahihi wa mambo kwani mawaziri waliopo wote mpaka sasa ni halali kwani wameapa mbele ya rais na wanahati za uteuzi kama sheria zinavyotaka iwe. Kwakua wapo kihalali hakuna haramu yoyote waliyofanya.

Stroke;

Sikiliza mkubwa. Ni hivi na kwa lugha rahisi kabisa, kwamba kwa mtazamo wa kawaida ni okay

Lakini kwa mtazamo wa kikatiba na kisheria ni batili 100%

Na laiti kama kuna watu waliathiriwa na maamuzi flani flani ya watu hawa wakapata guts za kwenda mahakamani kama alivyoshauri Lissu kushitaki, trust me serikali itashindwa tu!!

Kushindwa kwa serikali hakutakuwa na maana kuwa madhambi ya hawa watu waliyoyafanya ni poa, hapana.

Isipokuwa tatizo litakuwa ni kwamba, hatua zilizochukuliwa dhidi yao ni kinyume cha taratibu na sheria, hivyo maamuzi hayo ni obviuos mahakakama itayabatilisha ili serikali irudi ikajipange upya.

Tukumbuke jamani hii ni nchi yenye taratibu, sheria na katiba. Kama kila mtu atajifanyia mambo hovyohovyo kinyume cha sheria, basi itakuwa ni vurugu.

Ndiyo maana mimi nauliza, kuna kigugumizi gani serikali kufanya mambo yake kwa kufuata taratibu na sheria? Kuna ugumu ku - gazzette taratibu na majukumu hayo?

Hapa ndo utapata hata majibu ya kwa nini serikali kila ikipeleka kesi zake mahakamani huishiwa kushindwa tu.

Jibu ni kwamba, viongozi wa serikali wengi hawako smart, hawafuati taratibu na sheria katika mengi ya maamuzi yao ambayo mwisho wa siku huigharimu serikali!!

Tukumbuke mahakamani watu hubishana kwa vifungu vya sheria na si ubabe t
 
Hivi hii mihemko ya kisiasa tunapeleka wapi jamani.
Kama leo mawaziri wametumbua majibu huku hatuna hakika kama raisi ataruhusu watumbue au atakuwa anatumbua mwenyewe haimaanishi tukubali kwakua wanakiuka matakwa ya kikatiba na anacho sema Lisu ni kutekeleza matakwa ya kisheria kwanza ili majipu yakitumbuliwa yasiwe.na mabaki au dosari yeyote kwakuwa kutofanya hivyo kunaweza kuleta madhara endapo wakienda mahakamani. Lakini pia hakuna mahali Lisu amesema Mh JPM asipasue kwakua anajua yeye anatumbua kisheria ila mawaziri ndio bado hawajaruhusiwa kutumbua ila akiwaruhusu hata leo kwa kuwatangaza majukumu yao kwenye GN ndio watumbue. Hivyo ndio katiba ina taka na Lisu anataka katiba ifuatwe

Kwa wale ambao mlitumia akili za kuazima pima hapa sasa
Anaye taka majipu yatumbuliwe kwa kufuata taratibu za kisheria (watumbuaji wawe na mamlaka kisheria ) na anayetaka kutumbua tu ili tumsifu halafu baadaye serikali inapata hasara ni yupi kati ya hao analengo la kutoa mahipu yote. Amka kumekucha hatakama ikiwa mbelekwambele au kuisoma namba
 
Uweke hapa huo waraka, pia umekuja na jambo jingine ambalo sio vibaya kulijadili hivi ni job description inayompa mtu nafasi ya ajira au employment contract?
Nasema hivyo kwa maana kwangu mimi nachukulia kiapo kama ni employment contract...

Kwanza nikupongeze kwa kunogesha mada.

i. Kwa mnasaba wa mjadala nadhani unakubali kuwa kurasimishwa majukumu kwa maandishi kupitia tangazo katika gazeti la serikali ni suala la kisheria na lazima litekelezwe hilo la kwanza.

ii.Umesema wewe unachukulia kiapo cha uwaziri kuwa ni Employment contract hapo unazidi kukosea. Ingekuwa ni hivyo sheria isingelazimisha kukasimiwa kwa madaraka kupitia tangazo rasmi na wala kusingekuwa na loophall rais kupewa mamlaka ya kuunda wizara atakavyo(FIKIRIA ZAIDI HII), Yaani lazima Katiba ingelazimisha majina, idadi na majukumu ya kila wizara kikatiba au kisheria . Lakini huoni kuwa kutakuwa na contradiction pale ambapo rais atafanya majukumu yale yale ya waziri na wakati huo huo waziri akafanya anayofanya rais katika eneo ambalo waziri hajui mipaka yake ya kazi? hilo la pili.

iii. Ushauri kutoka kwangu(ukipenda) Mambo makubwa kama haya ya kitaifa (katiba na sheria) tusitangulize utashi yana athari sana. Nadhani ulimuona Mh mwakyembe alivyokuwa bussy ku take note anajuwa amejifunza kitu ingawa najuwa kwa wanasiasa anaweza kuja kujibu tu ili aonekane kaitetea serikali. pili humu Jf kila mmoja na uwezo wake NAKUSHAURI wengine USIWAJIBU watakupotezea muda. fafanua hoja yako bila jazba.

Kishada.
 
Back
Top Bottom