Majibu kwa hotuba ya Lissu Bungeni

Majibu kwa hotuba ya Lissu Bungeni

Hoja ya Lissu bado ina mashiko...suala la kukasimisha mamlaka lipo kisheria na si hiyari ya Magufuli.
Hoja ni kua kutokukasimishwa kwa mawaziri kupitia waraka hakufanyi yaliyofanywa na mawaziri kua batili, hiyo ndio hoja yangu.
 
Msamehe bure kapewa na nepi na marope bila kutafuna pia hana uwezo wa kutafuna
Huu ni mtazamo wangu wa hoja ya lisu kutokana na tafsiri ya sheria nilizotumia, kama kuna ukakasi nakaribisha marekebisho.
 
Huu ni mtazamo wangu wa hoja ya lisu kutokana na tafsiri ya sheria nilizotumia, kama kuna ukakasi nakaribisha marekebisho.
1. Sheria haitafsiliwi kwa jibu la ndiyo au hapana kama unavyofanya linganisha hoja za lissu na sheria zako.

2. Huna sifa wala weledi wa kutafisiri sheria ndiyo inavyojitokeza hapa

3. Hotuba iliwekwa hapa wote tumeisoma na kuitolea maoni ya kuafiki au kutokuafiki. Majibu hayatatoka JF bali yatatolewa na serikali iliyowasilisha na kuweka hoja mbele ya bunge ili ijadiriwe.
 
Ningependa kujibu hoja ya Lisu kuhusina na kauli aliyoitoa kwamba kwakua Mpaka sasa Rais Hakutoa Tangazo la serikali ili kukasimisha majukumu ya mawaziri kwa mawaziri waliopo kwamba kunafanya maamuzi yaliyotolewa na mawaziri kabla ya kutoa Tangazo hilo kua batili, kua kauli hiyo sio sahihi na kwamba imetolewa kwa lengo la kisiasa tu la kupotosha jamii kutokana na ukweli ulipo, nazungumza hivyo kutokana na maelezo nitakayoyatoa hapa;

1. Ni kweli kwamba kama hakuna waziri,Rais pekee ndie anakua waziri wa wizara husika na ni kweli kwamba kulingana na sheria za nchi yeye ndiye waziri namba moja, hivyo anapoteua mbunge yoyote yule kua waziri moja kwa moja anampa mbunge huyo mamlaka yake kama waziri namba moja, na Utaratibu wa kisheria ni kwamba waziri anapoteuliwa na kukubali uteuzi na kuapishwa kama Waziri anakua na mamlaka kamili kuhusiana na wizara husika kama angalikua nayo Rais. Tafsiri hii inapatikana kutokana na Kifungu cha 4 kinachotoa tafsiri; Cha sheria ya Tafsiri, sura ya kwanza ya sheria za Nchi, kama ilivyohaririwa mwaka 2002 inasema ( Section 4 of the Interpretation of Laws Act, Cap 1 , R.E 2002);

" Minister has the meaning given in Section 9 of this Act, in addition it includes the Vice President, the Prime Minister, andthe Minister, means the Minister Responsible for the matter in question and includes the Deputy Minister for the timem being performing the functions of that Minister or, if there is no minister responsible for the matter in question, mans the President"

Baada ya kuangalia Tafsiri ya sheria kuhusu nini Maana ya Waziri ni vyema tukaangalia namna waziri anavyoteuliwa,

Ibara ya 55 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977, Sura ya Pili ya sheria ya Nchi inasema ( The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 Cap 2 of the Laws of the United Republic of Tanzania)

55.-(1) All Ministers who are members of Cabinet by virtue of Article 54 shall be appointed by the President after consultation with the Prime Minister and they shall be responsible for such offices as the President may, from time to time, by writing under his hand and the Public Seal.

(2) In addition to the Ministers referred to in subarticle (1) the President may, after consultation with the Prime Minister, appoint Deputy Ministers. All Deputy Ministers shall not be members of Cabinet.

(3) The President may appoint any number of Deputy Ministers who shall assist Ministers in the discharge of their duties and functions. i

(4) All Ministers and Deputy Ministers shall be appointed from among Members of Parliament.

(5) Notwithstanding the provisions of subarticle (4), in the event that the President is obliged to appoint a Minister or a Deputy Minister after dissolution of Parliament then he may appoint any person who was a Member of Parliament


Tafsiri ya Ibara ya katiba hapo juu ni kua Waziri anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika majukumu ya uwaziri wake baada ya Rais kushauriana na Waziri Mkuu.

Waziri mteule atakua na mamlaka ya uwaziri katika wizara husika baada ya kupewa hati ya uteuzi yenye mhuri na sahihi ya Rais wa Jamhuri.

Ili waziri awe waziri kamili baada ya uteuzi wake, inabidi aape mbele ya Rais kiapo cha utii na kutimiza wajibu wa uwaziri wa wizara husika aliyoteuliwa; Katiba ya jamhuri ya Muungano Ibara ya 56 inasema;

Art. 56.A Minister or a Deputy Minister shall not assume office until he has first taken and subscribed before the President, the oath of allegiance and such other oath relating to the execution of the functions of his office as may be prescribed by an Act of Parliament.

Tafsiri yake ni kwamba Waziri hatakua waziri kamili mpaka atakapofanya kiapo cha utii mbele ya rais na kiapo cha kutimiza majukumu ya uwaziri mbele ya Rais.

Kwa kuangalia Maneno yaliyomo katika vifungu vya sheria tajwa hapo juu, utaona kua waziri anapata nguvu kamili za uwaziri baada ya kuapa mbele ya rais na kupewa hati ya uteuzi yenye sahihi na mhuri wa rais.

Kutokana na hoja ya Lisu kua mawaziri wamefanya majukumu yao kinyume na utaratibu wa sheria na hivyo kufanya maamuzi yao kua batili kwa kua hakuna tangazo la serikali ya kukasimisha majukumu ya uwaziri, kauli hiyo inatupeleka kwenye mjadala wa JE Waziri anakua waziri baada ya kuapishwa ama baada ya tangazo la serikali?

Wakati tukitafuta majibu ya Swali lililojitokeza ni vyema kwanza tukapata tafsiri ya nini maana ya Tangazo la Serikali au Government Notice;

Sheria ya Tafsiri ya Sheria ama ( The Interpretation of Laws Act) inatupa majibu, katika kifungu cha 4 kinasema;

" Government Notice means any subsidiary legislation made by the President, a minister or other public officer or authority pursuant to the power conferred by any Act"

Nini maana ya Subsidiary legislation;

Kifungu cha 4 cha sheria Tajwa kinasema;

" Subsidiary legislation means any order, proclamation, rule,rule of court,regulation,notice,by-law, or instrument made under any Act, or any other lawful authority"

Kifupi baada ya kupitia kifungu cha tafsiri ya sheria, utaona kwamba, maana ya tangazo la serikali ni kua ni wakara unaotokana na maamuzi, au amri au tangazo kwa uma, kutokana na sheria zilizopo au mamlaka yoyote husika.

Ili tuweze kupata maana ya Tangazo la serikali kulingana na hoja ya lisu tunapata maana kwamba, Rais alipaswa kutoa waraka kwa uma kukasimisha mamlaka ya uwaziri kwa baadhi ya wateule"

Sasa tuangalie hoja zifuatazo; je waziri anasita kua waziri kwakua hakutangazwa kwa uma kupitia waraka? Jibu ni hapana kwakua Sheria za nchi zinasema kwamba Waziri atakua waziri kamili mara baada tu ya kuapa mbele ya rais na kupata hati ya uteuzi yenye mhuri na sahihi ya Rais.

Swali la kujiuliza ni JE? kuna waziri yoyote katika serikali ya sasa anayefanya majukumu yake bila ya kua na hati ya uteuzi wala bila kuapa kiapo cha utii mbele ya Rais? Jibu ni Hakuna.

Tangazo la rais la kukasimisha mamlaka ya uwaziri ni taratibu tu za kiserkali ambazo tumejiwekea ili kuweka mambo kua kitaalam zaidi na kukosekana kwa tangazo hilo hakumfanyi waziri kutokua waziri kwani jambo muhimu ambalo linahitajika ni KIAPO NA HATI YA UTEUZI.

Hivyo kwa hoja hizo, hoja ya Lisu inakosa uhalali kisheria na ni ya kisiasa inayopaswa kupuuzwa.
Mkuu, ungejibu hii hoja na sio maneno mengi nje ya uwanja.

HOJA YA LISSU

Tarehe 15 Aprili, 1980, Bunge hili lilitunga Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Kiuwaziri, Sheria Na. 10 ya 1980. Sheria hiyo ilipata ridhaa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na kuanza kutumika Mei Mosi ya 1980. Pamoja na mambo mengine, Sheria hiyo ilimpatia mamlaka ya kuainisha idara, shughuli na mambo mengine ambayo kwayo kazi na majukumu yake amebaki nayo yeye mwenyewe au ameyakasimu kwa Mawaziri na tarehe ya kuanza kutekeleza majukumu hayo.

Tangu wakati huo, imekuwa ni sheria, na sehemu ya mila na desturi ya kikatiba ya nchi yetu, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kuainisha – kwa kupitia Tangazo lililochapishwa katika Gazeti la Serikali – Wizara, idara, shughuli na mambo mengine ambayo Rais amejibakizia mwenyewe, na yale ambayo amekasimu majukumu yake kwa Mawaziri. Utafiti wetu unaonyesha mambo yafuatayo katika miaka 36 na ya utekelezaji wa Sheria hii:
 
1. Sheria haitafsiliwi kwa jibu la ndiyo au hapana kama unavyofanya linganisha hoja za lissu na sheria zako.

2. Huna sifa wala weledi wa kutafisiri sheria ndiyo inavyojitokeza hapa

3. Hotuba iliwekwa hapa wote tumeisoma na kuitolea maoni ya kuafiki au kutokuafiki. Majibu hayatatoka JF bali yatatolewa na serikali iliyowasilisha na kuweka hoja mbele ya bunge ili ijadiriwe.
Ingekua hivyo unavyotaka wewe iwe JF kusingekua na mjadala wowote.

Sheria zipo ili zitafsiriwe, na kama sina sifa wala weledi wa kutafsiri hata lisu hana sifa wala weledi wa kutafsiri sheria yoyote ile , kwa kua mwenye jukumu la kutafsiri sheria ni MAHAKAMA. Kwa nafasi yake, analo jukumu la kutunga sheria ila sio kuitafsiri. Hoja yako ingekua na maana kama ungesema sina mamlaka ya kutoa tafsiri SAHIHI.

Ndio maana nikasema aliyoyasema Lisu ni upotoshaji kwani tafsiri yake sio sahihi ni ya kisiasa zaidi.
 
Bado hujamjibu lissu,waziri tayari ameapishwa na amekuwa waziri halali.Hoja ya lissu ni kuwa majukumu ya waziri ni yapi?Majukumu ya mawaziri sio ya kudumu na hubadilika kulingana na muda na Rais aliyepo!Kuna mamlaka ambayo Rais kwa utashi wake akaona ni vema akabaki nayo na kutompa waziri,ila baadaye akaona ampe mamlaka hayo waziri.Ndio Rais alitakiwa atoe waraka wa majukumu ya mawaziri ili wajue nini wanapaswa kufanya!Ni sawa na wewe umeajiriwa halafu hujapewa majukumu na bosi wako we ukafika ukaanza kufanya ujuavyo!ndio yale aliyosema sugu mawaziri wanaongozwa na mizuka!wakimuona Rais katokezea bandarini,wao kesho wako magetini!
 
Mkuu, ungejibu hii hoja na sio maneno mengi nje ya uwanja.

HOJA YA LISSU

Tarehe 15 Aprili, 1980, Bunge hili lilitunga Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Kiuwaziri, Sheria Na. 10 ya 1980. Sheria hiyo ilipata ridhaa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na kuanza kutumika Mei Mosi ya 1980. Pamoja na mambo mengine, Sheria hiyo ilimpatia mamlaka ya kuainisha idara, shughuli na mambo mengine ambayo kwayo kazi na majukumu yake amebaki nayo yeye mwenyewe au ameyakasimu kwa Mawaziri na tarehe ya kuanza kutekeleza majukumu hayo.

Tangu wakati huo, imekuwa ni sheria, na sehemu ya mila na desturi ya kikatiba ya nchi yetu, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kuainisha – kwa kupitia Tangazo lililochapishwa katika Gazeti la Serikali – Wizara, idara, shughuli na mambo mengine ambayo Rais amejibakizia mwenyewe, na yale ambayo amekasimu majukumu yake kwa Mawaziri. Utafiti wetu unaonyesha mambo yafuatayo katika miaka 36 na ya utekelezaji wa Sheria hii:

Elewa hili kwanza; Tangazo la serikali ni sheria, na nimeshaainisha kwenye majibu yangu, soma kwanza uelewe kabla ya kujibu mada yoyote.
 
Kunamchangiaji amesema umma ungefahamishwa kama mawaziri hao wangethibitishwa kwenye gazeti la serikali. Tujiulize hivi tunaposema gazeti la serikali ni gazeti lipi hilo na je linawafikia wananchi wangapi nchi hii hasa wale waliopo vijijini. Labda hapo iwe tu kwamba utaratibu wa sheria ufanyike ili kuukamilisha uteuzi wa mawaziri hao lakini sio kuufahamisha umma kupitia gazeti hilo.
 
Bado hujamjibu lissu,waziri tayari ameapishwa na amekuwa waziri halali.Hoja ya lissu ni kuwa majukumu ya waziri ni yapi?Majukumu ya mawaziri sio ya kudumu na hubadilika kulingana na muda na Rais aliyepo!Kuna mamlaka ambayo Rais kwa utashi wake akaona ni vema akabaki nayo na kutompa waziri,ila baadaye akaona ampe mamlaka hayo waziri.Ndio Rais alitakiwa atoe waraka wa majukumu ya mawaziri ili wajue nini wanapaswa kufanya!Ni sawa na wewe umeajiriwa halafu hujapewa majukumu na bosi wako we ukafika ukaanza kufanya ujuavyo!ndio yale aliyosema sugu mawaziri wanaongozwa na mizuka!wakimuona Rais katokezea bandarini,wao kesho wako magetini!
Huo ni mtazamo wako ambao haujaleta kajibu ya hoja yangu hoja yangu imejijkita katika kujibu hoja ya Lisu kua kwakua hakuna mwongozo wa serikali wa kukasimisha madaraka hivyo yaliyofanywa na mawaziri ni batili, nimejibu kua huo sio usahihi wa mambo kwani mawaziri waliopo wote mpaka sasa ni halali kwani wameapa mbele ya rais na wanahati za uteuzi kama sheria zinavyotaka iwe. Kwakua wapo kihalali hakuna haramu yoyote waliyofanya.
 
Elewa hili kwanza; Tangazo la serikali ni sheria, na nimeshaainisha kwenye majibu yangu, soma kwanza uelewe kabla ya kujibu mada yoyote.
Waswahili wanasema......ukiwa mwongo Kwanza uwe na kumbukumbu.......
Mwisho wa bandiko lako umemaliza hivi...


Tangazo la rais la kukasimisha mamlaka ya uwaziri ni taratibu tu za kiserkali ambazo tumejiwekea ili kuweka mambo kua kitaalam zaidi na kukosekana kwa tangazo hilo hakumfanyi waziri kutokua waziri kwani jambo muhimu ambalo linahitajika ni KIAPO NA HATI YA UTEUZI.

Hivyo kwa hoja hizo, hoja ya Lisu inakosa uhalali kisheria na ni ya kisiasa inayopaswa kupuuzwa.
 
Ingekua hivyo unavyotaka wewe iwe JF kusingekua na mjadala wowote.

Sheria zipo ili zitafsiriwe, na kama sina sifa wala weledi wa kutafsiri hata lisu hana sifa wala weledi wa kutafsiri sheria yoyote ile , kwa kua mwenye jukumu la kutafsiri sheria ni MAHAKAMA. Kwa nafasi yake, analo jukumu la kutunga sheria ila sio kuitafsiri. Hoja yako ingekua na maana kama ungesema sina mamlaka ya kutoa tafsiri SAHIHI.

Ndio maana nikasema aliyoyasema Lisu ni upotoshaji kwani tafsiri yake sio sahihi ni ya kisiasa zaidi.
Mbona wewe ni mwanasiasa kuliko Lissu kwa jinsi unavyotumika.

Umesahau kuwa kabla ya yeye kujibu hoja, huanza kwa kunukuu sheria inayompa madaraka ya kutoa au kujibu hoja iliyowasilishwa na serikali.

Uwe mkweli kwa nafsi yako wewe umepost hii kisiasa. Mimi ninachokuambia ni kuwa kwa jinsi ulivyoandika ni wazi huna sifa wala weledi wa uliyoyaweka. Rudia hoja yangu kuwa serikali itajibu hoja za Lisu hata kimagumashi.

Wewe unachokifanya ni kutafuta promo kwa manufaa yako na waliokutuma kwa kuparamia hoja za Lissu usiyokuwa na uwezo nazo.
 
Mtoa hoja aidha ukoshallow sana kwenye sheria au unamihemko ya kutetea chochote kinachopingwa kuhusiana watawala wa ccm.
 
Huo ni mtazamo wako ambao haujaleta kajibu ya hoja yangu hoja yangu imejijkita katika kujibu hoja ya Lisu kua kwakua hakuna mwongozo wa serikali wa kukasimisha madaraka hivyo yaliyofanywa na mawaziri ni batili, nimejibu kua huo sio usahihi wa mambo kwani mawaziri waliopo wote mpaka sasa ni halali kwani wameapa mbele ya rais na wanahati za uteuzi kama sheria zinavyotaka iwe. Kwakua wapo kihalali hakuna haramu yoyote waliyofanya.
Kwanini unakua mgumu wa kuelewa!?
Unaweza ukawa waziri lakini usiwe na madaraka flani. Madaraka waziri huyapata pale tu Raisi anapoyakasimisha, na zetu la kukasimisha lipo kisheria.
 
Mbona wewe ni mwanasiasa kuliko Lissu kwa jinsi unavyotumika.

Umesahau kuwa kabla ya yeye kujibu hoja, huanza kwa kunukuu sheria inayompa madaraka ya kutoa au kujibu hoja iliyowasilishwa na serikali.

Uwe mkweli kwa nafsi yako wewe umepost hii kisiasa. Mimi ninachokuambia ni kuwa kwa jinsi ulivyoandika ni wazi huna sifa wala weledi wa uliyoyaweka. Rudia hoja yangu kuwa serikali itajibu hoja za Lisu hata kimagumashi.

Wewe unachokifanya ni kutafuta promo kwa manufaa yako na waliokutuma kwa kuparamia hoja za Lissu usiyokuwa na uwezo nazo.
Ni haki yangu ya kikatiba kutoa maoni kuhusiana na jambo lolote lile linaloihusu serikali au bunge, As long as i am exercising my constitutional right, hayo mengine uliyoyazungumza kwangu hayana nafasi, and on top of everything the forum allows each and every thing to be discussed here, as long as sheria haijavunjwa. I have been here and done this before. Wewe huna mamlaka yoyote ya kuninyima mimi kutoa maoni yangu. Kama hujapenda nilichoandika. Acha wengine wajadili.
 
Umeanisha vizuri sana. Ni kweli kwamba mawaziri huwa mawaziri kamili baada ya kula kiapo mbele ya rais.
Lakini, kabla hawajaanza kutimiza majukumu yao Umma unapaswa kutaarifiwa kwanza kupitia tangazo la serikali kama sheria ilivyoainisha.
Hivyo basi, uwaziri wao kwa nafasi ni halali lakini, bado hawajatambulishwa kwa umma ili wayaanze rasmi majukumu yao. Kitendo cha kutangazwa kwa umma ndiyo description kwao.

N.B
Haya uliyoyaket si majibu kwa hoja ya Lisu bali ni mjadala juu ya hija ya Lissu.
labda tumuulize tundu lisu yeye alikuwa mbunge baada ya kutolewa ktk gazeti la serkali au baada ya kuapishwa? naomba ufafanuzi alianza ubunge lini baada ya uchaguzi
 
Mleta mada naona hutaki kuelewa,lengo lako sio kujifunza bali kupotosha kwa kila namna kwa manufaa yako binafsi!Pengine labda hujawahi kuona hata muundo huo wa waraka wa ukasimishaji wa madaraka!
Waraka huo unaeleza yale ambayo waziri anatakiwa kuyafanya,hii ni sawa na job discription!Mamlaka haya ya kazi hupewa kisheria na kwa utaratibu ambao umewekwa kisheria!Mawaziri wanaweza wakawa halali ila maamuzi waliyofanya bila kupewa mamlaka kisheria yakawa batili!
 
Huwezi kupangua hoja za mwanasheria Msomi aliyebobea kama Tundu Lisu kwa hoja nyepesinyepesi na quotations mbili tatu,inabidi ujiandae hasa na nondo za uhakika otherwise una display ignorance yako
 
Back
Top Bottom