Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,837
- 59,508
Mamlaka ya udhibiti wa Chakula na madawa TFDA jana imetoa tamko la kuzuia utumikaji wa maji ya Lady Jaydee mara moja baada ya taratibu za usajili wa maji hayo katika mamlaka hiyo kutofuatwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wahusika mamlaka hiyo imetoa agizo kwa kampuni inayotengeneza maji hayo A-One products & Bottlers ambayo ni kampuni tanzu ya Mohammed enterprises kuzuia na kutengeneza pamoja na kurudisha kiwandani chupa zote zenye maji hayo
Taarifa hiyo ilisema maji hayo ya Lady Jaydee yalizinduliwa siku ya Alhamisi iliyopita katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Paradise jijini bila kufuata tarartibu husika za usajili wa bidhaa zozote zinazolika ama kunywewa.
Taarifa zaidi kutoka kwa wakurugenzi wa mamlaka hiyo ya chakula na madawa inasema mbali ya kuamuru chupa hizo kurudishwa mamlaka hiyo imetawanya sehemu mbali mbali wakaguzi wake ili kuzuia usambazaji au uuzaji wa chupa ambazo tayali zilishaingia sokoni au kwenye maghala ya kuhifadhi vitu.
Ni kosa na hairuhusiwi kisheria kwa mtu yeyote kuzindua, kutawanya au kuuza bidhaa ya chakula ama kinywaji bila kupata idhini ya mamlaka hii ya TFDA alisema mkurugenzi wa Chakula bwana Raymond Wigenge.
Sisi tulipata taarifa ya kuwapo kwa maji hayo tarehe 31 ya mwezi wa kumi na mbili 2010 na kuanza kufuatilia kwa watengenezaji pamoja na mawakala wao wa usambazaji wa maji hayo.
Tukimnukuu bwana wigenge alisema "Ilibidi kuchukua hatua za za haraka kusimamisha uzalishaji ikiwemo kuzirudisha chupa zote na kusimamisha matangazo ya promosheni ya bidhaa hiyo ya maji na pia kuwapa maelekezo ya nini kifanyike kabla ya kuendelea kuzalisha maji hayo.
Alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo mume wa Lady Jaydee ambaye ndio meneja wake alikiri kupokea taarifa hiyo na kusema mchakato wa kufuata utaratibu wa usajili katika mamlaka husika tayari umesha anza na hivyo wanategemea hautapita muda mrefu uzalishaji wa maji hayo utaendelea.
Source:Bongo5