Maji ya Lady Jay Dee yamepigwa stop!!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,773
59,123
jaydee_water_stop.jpg

Mamlaka ya udhibiti wa Chakula na madawa TFDA jana imetoa tamko la kuzuia utumikaji wa maji ya Lady Jaydee mara moja baada ya taratibu za usajili wa maji hayo katika mamlaka hiyo kutofuatwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wahusika mamlaka hiyo imetoa agizo kwa kampuni inayotengeneza maji hayo A-One products & Bottlers ambayo ni kampuni tanzu ya Mohammed enterprises kuzuia na kutengeneza pamoja na kurudisha kiwandani chupa zote zenye maji hayo
Taarifa hiyo ilisema maji hayo ya Lady Jaydee yalizinduliwa siku ya Alhamisi iliyopita katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Paradise jijini bila kufuata tarartibu husika za usajili wa bidhaa zozote zinazolika ama kunywewa.

Taarifa zaidi kutoka kwa wakurugenzi wa mamlaka hiyo ya chakula na madawa inasema mbali ya kuamuru chupa hizo kurudishwa mamlaka hiyo imetawanya sehemu mbali mbali wakaguzi wake ili kuzuia usambazaji au uuzaji wa chupa ambazo tayali zilishaingia sokoni au kwenye maghala ya kuhifadhi vitu.

Ni kosa na hairuhusiwi kisheria kwa mtu yeyote kuzindua, kutawanya au kuuza bidhaa ya chakula ama kinywaji bila kupata idhini ya mamlaka hii ya TFDA alisema mkurugenzi wa Chakula bwana Raymond Wigenge.
Sisi tulipata taarifa ya kuwapo kwa maji hayo tarehe 31 ya mwezi wa kumi na mbili 2010 na kuanza kufuatilia kwa watengenezaji pamoja na mawakala wao wa usambazaji wa maji hayo.

Tukimnukuu bwana wigenge alisema "Ilibidi kuchukua hatua za za haraka kusimamisha uzalishaji ikiwemo kuzirudisha chupa zote na kusimamisha matangazo ya promosheni ya bidhaa hiyo ya maji na pia kuwapa maelekezo ya nini kifanyike kabla ya kuendelea kuzalisha maji hayo.

Alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo mume wa Lady Jaydee ambaye ndio meneja wake alikiri kupokea taarifa hiyo na kusema mchakato wa kufuata utaratibu wa usajili katika mamlaka husika tayari umesha anza na hivyo wanategemea hautapita muda mrefu uzalishaji wa maji hayo utaendelea.

Source:Bongo5
 
ndio tatizo letu wabongo,hayo maji yangekuwa ya mchina ingekuwa poa tu,lakini kwasababu ni mzalendo anayetafuta riziki lazima akwamishwe.
arggggggggggg nimechoka na bongo,afadhali nisipokuwepo,upuuzi mtupu,kwani mkimfanyia feva ya kuendelea kuwepo maji na huku akiwa anakamilisha taratibu itakuaje?
na wewe jide vipi bana?mbona unatuangusha?sasa na wewe unataka kuwa kama fisadi bila ya kufuata taratibu?
 
Wabongo tusikwamishane, nyie TFDA siku nyingine mkisikia kuna mbongo mwingine anataka kuzindua misosi au manywani ni vizuri mkatoa reminder notes on requirements before launch of the product badala ya kuwindana mitaani... Fanyeni hayo kwa wachina na wawekezaji uchwala wa kigeni
hawajakosea ni taratibu tu za kiintelijisia
 
hiyo ndo nguvu zaidi na ari zaidi na kasi zaidi katika nchi hii
 
Kwa vile yeye alilaunch hiyo brand officially ndiyo mana ilikuwa rahisi kumfuatilia.

Hivi lakini huyo Mohamnmed Enterprises hawafahamu sheria za nchi kuhusu vyakula au wameamua kuuchuna na kuendelea mbele?
 
inawezekana walikua wanajua process za kufuata bt wakaamua kupotezea !
c unajua jide amezoea promo za bongo flava{bfu}
 
Mbona watu mnashindwa kuelewa si swala la mchina mhindi au mjerumani. Maji ni mali ya taifa hamuelewi. Akitaka auze juice halafu ayaite Lady what ever....nchi zilizoendelea hutaona eti maji yana jina la mtu nani kasema hao wenye pesa hawajaliona hilo. Idara husika inafanya kazi yake sawa sawa rudisheni maji. Huu ndio mwanzo wa kutawaliwa. Mbona viwanda vya bia havijazindua hata bia moja kwa jina la mtu.
 
....Kwa Hiyo Bia Pia ni Mali ya Taifa?? Punguza Usongo na Jitihada za Mwenzio Weye, Dah!

wewe uko tz na hujui chochote kabisa kuhusu brand name.
je hujui Toyota,suzuki etc ni majina ya watu binafisi??
Jina lolote lile linaweza likatumika,liwe la kijiji chako,mtaa wako ,ukoo wako, au jina lako mwenyewe.
Mbona watu mnashindwa kuelewa si swala la mchina mhindi au mjerumani. Maji ni mali ya taifa hamuelewi. Akitaka auze juice halafu ayaite Lady what ever....nchi zilizoendelea hutaona eti maji yana jina la mtu nani kasema hao wenye pesa hawajaliona hilo. Idara husika inafanya kazi yake sawa sawa rudisheni maji. Huu ndio mwanzo wa kutawaliwa. Mbona viwanda vya bia havijazindua hata bia moja kwa jina la mtu.
 
Nchi hii kuna hili la 'tukose wote' hela akipata mzungu,mhindi au muarabu ni sawa akipata mbongo mwenzetu inatuuma.Maji haya yalikuwa yanauzwa kwa jina la 'Maisha' hakukuwa na tatizo yakabadilishwa jina tu yaitwe 'lady jaydee' ikawa nongwa kwakuwa Judith angepata pasenti yake kwa kila chupa iuzwayo tukaona itafaidi sana.Maji ni yaleyale,kiwanda kilekile nadhani mmeelewa sasa.
 
Mbona watu mnashindwa kuelewa si swala la mchina mhindi au mjerumani. Maji ni mali ya taifa hamuelewi. Akitaka auze juice halafu ayaite Lady what ever....nchi zilizoendelea hutaona eti maji yana jina la mtu nani kasema hao wenye pesa hawajaliona hilo. Idara husika inafanya kazi yake sawa sawa rudisheni maji. Huu ndio mwanzo wa kutawaliwa. Mbona viwanda vya bia havijazindua hata bia moja kwa jina la mtu.

Uko sawa kabisa mpendwa.
 
Uko sawa kabisa mpendwa.

Na wewe uelewa wako ni kama wake....ardhi ni mali ya taifa too..then mbona watu wanaita majina yao?Iwe maji?maji haya yamekuwa yakiitwa Maisha kama mkuu hapo juu alivyosema..sasa leo yamebadili jina...kosa..
 
jaydee_water_stop.jpg

Mamlaka ya udhibiti wa Chakula na madawa TFDA jana imetoa tamko la kuzuia utumikaji wa maji ya Lady Jaydee mara moja baada ya taratibu za usajili wa maji hayo katika mamlaka hiyo kutofuatwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wahusika mamlaka hiyo imetoa agizo kwa kampuni inayotengeneza maji hayo A-One products & Bottlers ambayo ni kampuni tanzu ya Mohammed enterprises kuzuia na kutengeneza pamoja na kurudisha kiwandani chupa zote zenye maji hayo
Taarifa hiyo ilisema maji hayo ya Lady Jaydee yalizinduliwa siku ya Alhamisi iliyopita katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Paradise jijini bila kufuata tarartibu husika za usajili wa bidhaa zozote zinazolika ama kunywewa.

Taarifa zaidi kutoka kwa wakurugenzi wa mamlaka hiyo ya chakula na madawa inasema mbali ya kuamuru chupa hizo kurudishwa mamlaka hiyo imetawanya sehemu mbali mbali wakaguzi wake ili kuzuia usambazaji au uuzaji wa chupa ambazo tayali zilishaingia sokoni au kwenye maghala ya kuhifadhi vitu.

Ni kosa na hairuhusiwi kisheria kwa mtu yeyote kuzindua, kutawanya au kuuza bidhaa ya chakula ama kinywaji bila kupata idhini ya mamlaka hii ya TFDA alisema mkurugenzi wa Chakula bwana Raymond Wigenge.
Sisi tulipata taarifa ya kuwapo kwa maji hayo tarehe 31 ya mwezi wa kumi na mbili 2010 na kuanza kufuatilia kwa watengenezaji pamoja na mawakala wao wa usambazaji wa maji hayo.

Tukimnukuu bwana wigenge alisema "Ilibidi kuchukua hatua za za haraka kusimamisha uzalishaji ikiwemo kuzirudisha chupa zote na kusimamisha matangazo ya promosheni ya bidhaa hiyo ya maji na pia kuwapa maelekezo ya nini kifanyike kabla ya kuendelea kuzalisha maji hayo.

Alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo mume wa Lady Jaydee ambaye ndio meneja wake alikiri kupokea taarifa hiyo na kusema mchakato wa kufuata utaratibu wa usajili katika mamlaka husika tayari umesha anza na hivyo wanategemea hautapita muda mrefu uzalishaji wa maji hayo utaendelea.

Source:Bongo5

mbona mtaani yapo kama kawaida
 
Back
Top Bottom