Maisha yamenishinda, vita imenishinda

Sasa kipi bora Wangari? Ajiue au aende akapige mpini kijijini? Unaona jinsi jamaa alivyokata tamaa? Kwani akikaa mjini pesa itajileta?
Kinachomsumbua huyo jamaa na vijana wengine wengi sio pesa ila hana moyo wa kuvumilia magumu/changamoto za dunia hii. Unafikiri kilimo hakina changamoto? Kama ana mentality ya kujinyonga basi hakuna lenye nafuu hapa duniani hata akipewa milioni 100 na MO Dewji.
 
Kuna dada alikua rafiki yangu kamaliza chuo udsm kazi hana,kwao sumbawanga anategemewa,tempo aliyopata kapigwa chini,maisha magumu,kodi hana,kazi anatafuta hapati..alikua ananilalamikia hadi nikawa nahisi atajiua,nilijaribu sana kumpa moyo alikua anaongea Kama wewe mtoa mada,kama mtu ambae kapangiwa FUNGU LA KUKOSA..siku moja natoka kwa mama jioni natembea mdogo mdogo,mdada kanitumia meseji ndefu,nzito Sana,wakati napandisha kilima cha forest,kuna kijana mlemavu akaniomba nimsaidie kumsukuma,hana MIGUU,Mikono yake mifupi Sana,kwenye baiskeli anaonekana Kama mtoto,roho iliuma Sana nikakumbuka kufuru zangu ukikosa mlo mmoja unaona Kama Mungu hakujali kabisa,kakukosea,anakuonea,nikafikiria nilivyo,ninavyoweza kufanya,nikajilinganisha na rafiki niliyekua namsukumiza,nikasema Asante Mungu,umenipendelea Sana..tangu hapo nikaanza kumpuuza yule dada,,hatuna shukurani..silalamiki sina viatu wenzangu hawana MIGUU..learn to show gratitude,kua na moyo mgumu,angalia ulivyobarikiwa,unachomudu,unachoweza fanya..kua jasiri maisha yetu wote yana pressure Life ain't sweet bro for both of us..and we don't owe Lord nothing...
 
Back
Top Bottom