Pole sana. Kwa kweli pole sana.
Inawezekana unahitaji msaada wa nguvu za Mungu kujinasua katika nira za shetani na mawakala wake.
Wachawi, mapepo na majini huenda yamefunga ngome kwenye maisha yako katika ulimwengu wa roho yakitaka kukutaabisha na kukuletea mauti.
Katika injili ya Luka 10:18-19 , Yesu Kristo anasema, "TAZAMA NIMEWAPA MAMLAKA YA KUKANYAGA NYOKA NA NG'E NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI, WALA HAKUNA KITU KITAKACHOWADHURU".
Tubu dhambi zako zote na umuombe Mungu akusaidie kujinasua kwenye ngome za yule mwovu kwa jina la YESU.
Maana Mungu anasema, "nimewapa jina kuu lenye mamlaka, nalo ndilo jina la YESU KRISTO mungu aliye hai".
Yeyote anayelitamka jina hilo akiwa na haki na kibali mbele za Mungu, ataokolewa.
Mungu akusaidie na akuponye maradhi na shida zote.