Kama maisha yamekuwa tofauti na matarajio epuka kulazimisha maisha kuwa tofauti

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,485
14,353
Kisaikolojia ipo kanuni huitwa "Law of reverse action" ni kanuni ya kufanya kazi tofauti na vile ambavyo unahisi unatakiwa kufanya.

Kwa mfano ukiwa mnene sana na unataka kupungua uzito kadiri unavyozidi kufanya mazoezi ili upungue uzito ndiyo unazidi kujiona mnene kuliko mwanzo na utapata hasira na kuvunjika moyo na kuacha mazoezi moja kwa moja.

Lakini ukiamua kuupenda muonekano wako na kuishi vile ulivyo hata ukifanya mazoezi inakuwa kwa burudani sio kupungua uzito utaona mabadiliko mwilini haraka sana.

Hivyo hivyo katika maisha yako ipo mipango mingi sana umejiwekea lakini utaona unapata matokeo tofauti lakini kutumia matokeo tofauti kujiwekea malengo mapya ni bora kuliko kulazimisha matokeo yaleyale ya awali .

Hivyo leo tuangalie hatua za kukabiliana na hali ya maisha kuja tofauti na matarajio yako.

Utajifunza yafuatayo
I. Vikwazo vya kufikia malengo yako
II. Ufumbuzi wake

I.VIKWAZO VYA KUFIKIA MALENGO YA KILA MTU NI
Vikwazo vipo katika makundi manne nayo ni

a. MAHUSIANO/FAMILIA

Katika mahusiano au familia kuna vikwazo mbalimbali ambavyo vinaweza kukupa stress navyo ni
1.kutengana na mwenza wako, mahusiano kuvunjika,kifo cha mzazi au mwenza,au mtoto au ndugu au rafiki n.k

2. Mwenza wako kuathirika na uraibu wa pombe kupindukia au dawa za kulevya au kucheza kamari au kutumia pesa nyingi sana ghafla,ugomvi wa wazazi wako na mwenza wako

3. Ugomvi na mwenza wako, kumfumania mwenza wako,watoto kukithiri utovu wa nidhamu,kulea watoto pekeako,ugomvi na wakwe zako

4.hofu ya usalama wa watoto,mtoto kulia sana usiku, mwenza wako kukosa shukurani,

b.MASUALA YA KIAFYA
Unaweza kuwa na "stress" kupita kiasi kwa sababu za masuala ya afya kama vile kuugua muda mrefu sana bila kupata nafuu, kuambukizwa ugonjwa usiokuwa na tiba,kushindwa kusababisha au kupata ujauzito kwa muda mrefu sana, kuathirika na kujichua (masterbation),kupitia màumivu makali sana ya mwili au mifupa,kupata ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu,kuumwa kichwa na mgongo,hedhi kuvurugika, ujauzito kuharibika,unene kupita kiasi

c. MASUALA YA KIFEDHA
Unaweza kupitia "stress" kupita kiasi kwa sababu ya matatizo ya kifedha ambayo vyanzo vyake ni
1.kuingiza fedha kidogo sana kwa mwezi kwa sababu za kukosa ajira au kukosa kazi ya uhakika,kudaiwa fedha nyingi sana, biashara kukosa wateja, kufukuzwa kazi,au kusimamishwa kazi, kustaafu bila maandalizi, kucheleweshewa malipo ya mshahara,

2. MATUMIZI MAKUBWA SANA YA FEDHA
Unaweza kuwa na "stress" kupita kiasi kwa sababu unatumia pesa nyingi sana kwa mwezi labda kwa

a. Kusomesha watoto shule au chuo chenye gharama kubwa sana,talaka au kutengana na mwenza wako,kuwa na uraibu wa pombe kupindukia au dawa za kulevya au kucheza kamari au kutumia pesa nyingi sana ghafla

b. Kuishi maisha ya kifahari sana,kuwa na idadi kubwa sana ya watu tegemezi,mwenza wako kutumia fedha zako bila kukupa taarifa

c. Kuishi bila bajeti,kuzaa au kuoa bila maandalizi, kuchukua mikopo umiza,kufanya biashara ambayo hauna elimu nayo

3. DHARURA
Unaweza kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa sababu ya dharura kama vile kifo cha mzazi au mlezi ambaye anahudumia familia kifedha, talaka, au kutengana na mwenza, safari za ghafla,ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu,kuibiwa fedha, kudhulumiwa fedha, kuvamiwa na wahalifu, kampuni kupunguza wafanyakazi, akaunti za benki kuzuiwa kutoa fedha,majanga ya asili kama mafuriko,ukame ,moto n.k

D. MASUALA BINAFSI

Unaweza kupata "stress" kupita kiasi kwa sababu ya masuala binafsi kama vile hofu kuhusu muonekano wako, kukosa maelewano mazuri na wafanyakazi wenzako, kupelekeshwa sana kazini, hofu ya usalama wako, tishio la kufukuzwa kazi, kupoteza uwezo wa kuona au kusikia,kufanya kazi chini ya viwango, ukaguzi wa kazi zako,hofu juu ya umri kuongezeka bila kupiga hatua yoyote kiuchumi, kupata kesi, kudai watu pesa lakini hawarudishi, ahadi kuvunjwa, kunyimwa haki zako, kukosa ushirikiano kutoka kwa watu wengine, majukumu ya kazini kuongezeka au kubadilishwa ghafla, upweke baada ya watoto kusafiri au kuoa au kuolewa,

MATUKIO YOTE HAYO HAPO JUU HULETA MABADILIKO YAFUATAYO MWILINI
a. Moyo kwenda mbio, kizunguzungu, kupumua haraka haraka, kutokwa jasho bila joto, kubanwa kifua,mwili kufa ganzi, kichefuchefu, kukosa utulivu

B. Tumbo kuvurugika, kupaniki ghafla, kuhisi unataka kudondoka ghafla, kuhisi unataka kufa ghafla,

C. Hofu ya kurukwa akili, uchovu mwili mzima, hasira kupita kiasi, kizunguzungu,kuumia kooni,moyo kuuma sana, kukosa usingizi au kulala sana mpaka unachoka, kujitenga

d. Kuhuzunika sana muda wote,kujuta sana, kujilaumu, kujikosoa kupita kiasi,kuanza kulia kukata tamaa ya maisha,

e. kujiona huna thamani, kujiona mpweke sana, kujiona mwenye dosari nyingi sana, kupoteza hisia za mapenzi, kutamani kujiua

hayo ni mabadiliko ya mwili haina maana kwamba maisha yamefika mwisho.

UFUMBUZI WAKE

Kama maisha yamekuwa tofauti sana na matarajio yako epuka kulazimisha maisha kuja vile umepanga.
Fanya yafuatayo

1. KUWA MWEPESI KUBADILISHA MSIMAMO
Kama binadamu wengine utafanya makosa katika maamuzi yako.Kwa wastani binadamu hufanya makosa kwa 70% ya maamuzi yake ya kila siku hivyo uwezekano wa kufeli katika malengo yako ni mkubwa sana.

Alipata kusema Viktor Franklin kwamba kama huna uwezo wa kubadilisha hali ambayo unapitia,unatakiwa kubadilisha mtazamo wako eneo hilo.

Kutumia njia ileile ambayo haileti matokeo mazuri itafanya upoteze muda mwingi sana badala yake badili njia yako ikiwa njia ya awali haina matokeo mazuri

2. DHIBITI KILE KIPO NDANI YA UWEZO
Alisema Marcus Aurelius mfalme wa Roma ya kale kwamba upo na nguvu ya kudhibiti akili yako sio matukio yenye kutokea nje yako.Huwezi kupanga nini kitokee katika maisha yako ila unapanga ufanye nini kwa kila tukio lenye kutokea maishani mwako.

Huwezi kudhibiti tabia au maamuzi ya wengine.Baadhi ya watu ni wavivu wa kufanya maamuzi,wengine ni wepesi,wapo wenye huruma wapo wasiokuwa na huruma,wapo wenye kujali mahitaji ya wengine wapo wenye kujali maslahi yao binafsi

Watu wa aina hiyo utakumbana nao .

Ikiwa mafanikio yako hutegemea sana maamuzi ya wengine basi uwezekano wa kufeli eneo hilo ni mkubwa sana kwa sababu kila mtu huwa na vipaumbele tofauti

3. FANYA YENYE KUKUSAIDIA
Kama umekata tamaa ya maisha jiulize kama huo ni uamuzi sahihi au Lah ,je unaweza kubadilisha maisha yako kwa kukata tamaa?

Epuka kulaumu mwenendo wa wengine,epuka kulaumu mbinu za mpinzani wako,epuka kurekebisha tabia za wengine,tumia muda wako kuboresha tabia yako utakuwa na amani na utulivu

Makosa ya wengine waachie wenyewe,tabia za wengine waachie wenyewe, maamuzi ya wengine waachie wenyewe wekeza nguvu kurekebisha tabia zako tu ndio zipo ndani ya uwezo wako

4.KUWA MVUMILIVU
zipo nyakati unaweza kufanya kila kitu kwa usahihi lakini hupati matokeo mazuri unaweza kuvunjika moyo lakini hayo ndio maisha yalivyo.

Zingatia kwamba hakuna kitu chochote chenye kudumu milele haijalishi hali ambayo unapitia ni ngumu sana au nzuri sana haiwezi kudumu milele.

Kuna nyakati hali nzuri ya maisha inaanza kwa kuleta majanga makubwa sana yenye kuumiza na kuvunja moyo hivyo kuwa mvumilivu eneo hilo

5. HUZUNI NA FURAHA

Kama upo na furaha sana hivi sasa na endapo utachunguza sana chanzo cha furaha yako utagundua kwamba sio furaha bali ni yale màumivu makali sana moyoni ambayo ulikuwa unapitia ndio yamegeuka kuwa furaha.

Kila chozi la furaha huwa ni matokeo ya kupitia màumivu makali sana na uchungu moyoni.Hivyo wingi wa màumivu moyoni mwako huwa wingi wa furaha yako ikiwa hutokata tamaa eneo hilo.

Ikiwa umejiwekea malengo vikwazo vitakuja njiani kukuonyesha njia sahihi tofauti na ile ulipanga wewe kuitumia

Vikwazo vya mafanikio yako ndiyo njia ya mafanikio yako.

Usilaumu vikwazo angalia mbinu zako za kukabiliana na vikwazo hivyo eneo hilo ndio nguvu zako zipo.
 
Back
Top Bottom