Dp800
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 2,302
- 4,684
Naikumbuka hii story ya mama mmoja alifiwa na mtoto wake akaona uchungu mkuu hata asikubali kile kilichotokea basi akaanza kusafiri kwa waganga na makuhani ili aweze kumrudisha mtoto wake maana anampenda sana hivyo hawezi kukubali kufa kirahisi. Katika harakati hizo alijikuta ameingia kwa mganga nguli mwenye sifa za kurudisha maiti. Alipewa dawa ambayo masharti yake ni kuchanganya na udongo wa nyumba/boma ambalo halijawahi kufiwa na mpendwa wao yeyote labda ni mama, baba au mtoto. Mama yule akaanza kuzunguka huku na huko hata asipate sehemu ambayo hawajawahi kufiwa, ndio mara akakaa chini na kujiuliza binafsi kama hawa wote wamefiwa na maisha yameendelea ni kitu gani mimi kinanisumbua mama yule baada ya kuwaza na kuwazua hakuona haja ya kurudi tena kwa mganga bali kukubali changamoto zake kuendelea na maisha yake kama kawaida kwani hakuna yeyote hapa duniani asiye na matatizo hata wale unao waona wanacheka na kufurahi.