Mimi naona ni Bigbrother ya Bongo! Vijana wako 18 na wanajaribu kuishi maisha ya kijima!
Wakati wa usaili wa vijana hawa nilijifunza kitu kimoja. Watanzania wengi tu wajinga wa kutupa (labda wengine kati yetu tu wapumbavu)! Kuna vijana waliulizwa waoneshe IQ au Black box zao ziko sehemu gani ya mwini na kweli wakawa wanazitafuta hata kwenye vidole vya miguu. Na kuna mwingine alisema voice box yake iko karibia na magoti! Nadhani hizo tapes wampelekee JK na Timu yake
Kuhusu vijana wenyewe sitaki kusema mengi. Jaribu kufuatilia mwenyewe!
Kama waliwalenga vijana wa vijijini au wale ambao kiwango chao cha elimu hakikuwa kigezo katika usaili huo, nadhani ilikuwa ni makosa kuyahusisha maneno kama IQ au Black box katika huo usaili . Hasa ukizingatia kuwa lugha ya taifa si Kiingereza, na lugha ya kufundishia bado ni ugonjwa wa taifa.