Maisha Plus Tv Show ya Masoud Kipanya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha Plus Tv Show ya Masoud Kipanya

Discussion in 'Entertainment' started by Lucchese DeCavalcante, Mar 7, 2009.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Leo nilikuwa naangalia TBC1 TV nikakutana na inayosemekana kuwa ni reality TV show inayoongozwa na aliyekuwa mtangazaji wa power breakfast show ya Clouds FM Masooud Kipanya.

  Show hii inafahamika kama Maisha Plus na ina vijana kama 15 wake kwa waume walioko camp huko kijijini sasa nauliza je hii show madhumini yake nini?

  Natumai kuuliza sio ujinga!
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mimi naona ni Bigbrother ya Bongo! Vijana wako 18 na wanajaribu kuishi maisha ya kijima!

  Wakati wa usaili wa vijana hawa nilijifunza kitu kimoja. Watanzania wengi tu wajinga wa kutupa (labda wengine kati yetu tu wapumbavu)! Kuna vijana waliulizwa waoneshe IQ au Black box zao ziko sehemu gani ya mwini na kweli wakawa wanazitafuta hata kwenye vidole vya miguu. Na kuna mwingine alisema voice box yake iko karibia na magoti! Nadhani hizo tapes wampelekee JK na Timu yake

  Kuhusu vijana wenyewe sitaki kusema mengi. Jaribu kufuatilia mwenyewe!
   
 3. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mie wakati wa usahili kuna wakati sikufurahia namna bwana masoud,Bonda na yule dada..walivyo kuwa wanauliza maswali...mengine yalikuwa si ya kujenga,mengine ni ya kiudalilishaji..na wakati kwa kuwa wao walikuwa wamechoka walikuwa wanafanya kama hawataki.

  Hii ni ubunifu wa masoud lakini haikuwa fair kuwafanyi vijana wale ambao walionekana wengine hawana kazi wanategemea bahati nasibu ya paleNa kupata audiance.
   
 4. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,966
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Ni kweli inaonekana uelewa wa vijana wetu siku hizi ni mdogo sana sasa sijui ni nini.Ninajoweza kusema ni kwamba vijana wamepoteza ari ya kujisomea mambo yenye kuwaongezea elimu.na kusoma magazeti ya udaku,kusikiliza bongo flavour.na kwenye TV kutazama michezo ya kuigiza tuu.kweli ilinisikitisha sana kwani kwa umri ule mimi niliweza kujua Anti balistic missile ni nini.Niliweza kukuonyesha Kamchatica kwenye atlas iko wapi
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Madhumuni yake kama show zote kwenye TV, kuwavutia watazamaji ili waweze kuuza Advertising space.
   
 6. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #6
  Mar 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu hata mimi kuna maswali yaliniboa kidogo.Kwa mfano masoud alimuuliza dada mmoja ni kwanini wanawake wanafua chupi kila wanapooga lakini sio kwa vijana wa kiume,akita kujua kama wanawake ni wachafu sana kuliko wanaume au?hii haikukaa sawa.
   
 7. DDT

  DDT Member

  #7
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfunyukuzi
  Masoud anataka kujiajiri kwenye media baada ya kutoka/kufukuzwa kwenye media. Hana ujanja maana bila hivyo atasahaulika mapema
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Yep, mimi nimetazama kile kipindi mara tatu, wala sikujua kinataka kufundisha nini. Kina sound so fake sioni originality ya watu wenyewe. bora big brother kwani inaweza kumfanya mtu awe au afanye kama angekuwa kwingineko. Kwanza hiyo maisha plus sio eti kun hidden camera hivyo kumfanya mtu awe not very original since anajua kamera inakuwa inamchukua. Vitu vyenyewe wanavyo fanya kwenye kijiji wala havieleweki vinamjenga nini mtu pale ili awe nini! probably am wrong kwa kuwa sijafuatilia kiundani. Masood mwenyewe is so much involved to the extent i feel inabore sana.... dont know. but to me i dont get anything out of it rather than waste of time!
   
 9. m

  mcbenfrank Member

  #9
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 9, 2006
  Messages: 11
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Mtazamo wangu Serikali ya Tanzania sasa imefika wakati wa kuacha kufanya Masikhara na mfumo wa elimu hususan kwa vijana ambao ndio nguvukazi na tegemeo kubwa kwa maendeleo ya Taifa. Ni ukweli usiopingika vijana wamepoteza dira ya kielimu, morali wa kujifunza umepungua sana among vijana, wengi wetu hatuna ufahamu wa kina kuhusu mambo mbalimbali ya msingi yanayoiathiri dunia na jamii kwa ujumla, wengi huishia kusoma vichwa vya habari magazetini na kuridhika bila kupata habari kwa undani, wakati taarifa ya habari kwenye luninga si ajabu kumkuta kijana akibadilisha channel kutafuta channel yenye maigizo ama bongo fleva. Ni nadra sana kumkuta kijana wa kisasa kama wengi wanavyojiita (hususan age btn 7 - 28) ana ratiba ya kwenda Library kujisomea na kujifunza ama kupata ufahamu katika nyanja mbalimbali.
  Serikali kama Serikali ina uwezo mkubwa na wakutosha kuweza kujenga mazingira na motisha kwa namna ambayo itawafanya vijana wajijengee tabia ya kupenda kujifunza.
  Nadhani pia Magazeti ya udaku yangeongezewa kodi hata kwa asilimia 600% zaidi ili ku-discourage manunuzi ya magazeti hayo among vijana ambao wengi huishia kutafuta na kusoma habari za udaku zaidi kuliko kusoma vitabu na majarida yenye kujenga kwowledge.
  Bei ya vitabu vya kujenga knowledge na tafiti ipunguzwe kwa asilimia kubwa ili kuwapa vijana uwezo wa kuvi-afford.
  Naomba niishie hapa kwa sasa, ila bado nna mengi ya kuchangi kuhusu hili suala.
   
 10. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  KP ni kijana anayejitahidi sana,angekuwa ni mwekezaji wa nje kaandaa Maisha Plus tungemsifia,lakini kwa kuwa ni Mtanzania mwenzetu tunamponda...
  Ndio kuna mapungufu mengi katika Maisha Plus lakini tumtie moyo... Na sio kumbeza..
  MASOUD KIPANYA BIG UP!!!!
   
 11. M

  Mwanazuoni Member

  #11
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  halafu tukumbuke ndio kwanza anaanza hii program. Inawezekana mtaji wa kufanya kwa kiwango ambacho tungetaka ni mdogo kama inavyokua kwenye kuanzisha biashara yeyote ile. Tuache kuwa wepesi kumuhukumu na kumkosoa mtu kwa kiwango hiki.

  Kuna mapungufu kweli ambayo kama atafanya tena anatakiwa kushauriwa ayaache. lakini pia siyo late that much kwa sababu jana ndio ilikua siku ya sita kati ya 60 vijana wale watakayokaaa kijijini. ukiangalia kwa haraka na kwa mtazamo wa kukosoa utaona hakuna la maana. Lakini kwa waliona jana wale vijana walijaribiwa kwa pombe na walianza kuonekana sura zao halisi na sio za kuiga kwa kujua kamera inawachukua. Pale kuna watu hawajawahi kushika hata jembe kwa mkono na sasa masudi anawasaidia kuona maisha katika upande wa pili. wanalima na wanafanya kazi zingine za mikono.

  Bado naona kuna la kujifunza toka kwao. lakin pia Masoud katupa picha ni jinsi gani tulio na vijana wenye ufahamu mdogo katika nchi yetu. ni mdogo sana hasa unapoona swali mtu aliloulizwa na amefika form four. Style ya kuwatafuta haikuwa nzuri sana hasa jinsi ya uulizaji wa maswali but all in all they did something
   
 12. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Hii issue siyo ya utanzania au ugeni. On top TBC ni television ya taifa,siyo ya watu kwenda kujaribisha vitu vyao. Program kama ile ilitakiwa iandaliwe vyema ifanyiwe auditing ndo watuletee walaji. Pale siyo sehemu ya kukuza watu na initiatives zao. Hilo nakataa.

  Tupo pamoja kwamba jamaa ni creative sana, ni kweli namkubali sana kwenye katuni. Yuko vizuri sana kwenye katuni lakini kwenye tv...mhh.. nina doubts, hata presentation yake mimi binafsi sioni manjonjo ya kunifanya nifurahie. Labda kwenye radio.

  So long kuna wadhamin wametoa hela yao kwa kurusha kipindi, it does not mean kila mtu tu aje na kitu ambacho hatukielewi theme and outcomes. Everytime naangalia tv at least kuwe na mantik. Pengine kwenye hiyo maisha plus iko lakini mimi to date sijaiona hata during interview. Anyways it is my opinion.
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Dark City... Thanks!

  Kweli kuna viazi mule hadi basi lakini Nadhani sio fair kulinganisha vijana wa maisha plus na ku-conclude kwamba majority wa vijana wako hivyo, kimtazamo naona sio wengi ambao ni mambumbu, tunaowaona mambumbu kwenye maisha plus ni wale wasio na alternatives you can just tell from their looks wako na background gani... kumbuka showbiz bongo bado hailipi na ni alternative ya walioshindwa mainstream life tofauti na developed world where elimu inaweza kuwa alterantive ya walioshindwa sports and entertainment.


  Jaribu kuangalia debates programs hapohapo TBC kwa watoto wa sekondari wapo wanaojitahidi sana tofauti na maisha plus
   
 14. M

  Mundu JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Jambo la maana kubwa ni kumsaidia na kumshauri Masoud katika kuendesha kipindi chake. Kumbeza hakutasaidia kwani tayari jamaa yupo hewani.

  Napatwa na wasiwasi na wandugu wengine hasa wale mlioangalia kile kipindi.... nadhani kingekuwa cha Kizungu/kiingereza kingekuwa ni bora zaidi kwao!

  Sijui hapa tatizo ni Masoud au lugha au...?

  Tumsaidie ili aboreshe kipindi chake. Kwanza amejitahidi sana kwa namna moja au nyingine hadi kufikia pale. Big up Masoud.
   
 15. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160

  Mkuu,
  Umenena jambo la msingi hapa, "kumsaidia na kumshauri Masoud katika kuendesha kipindi chake". Hilo nakubaliana nalo sana. Lakini hamna hiyo provision! Yaani baada ya kipingi hamna mahala tunaambiwa tutoe maoni yetu juu ya uboreshaji. That means hawahitaji msaada wa wasikilizaji na watazamaji. Mbona kwenye vipindi vingine au TV nyingine mwishowe unaona wanaeleza TOA MAONI YAKO na watu tunarusha yetu amboyo tungependa kuyaona.
   
 16. ram

  ram JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Jama wa JF, Masoud anahiji kupongezwa kwa ubunifu aliounonesha. Ni kweli kuna mapungufu mengi tu lakini tukumbuke ndo kwanza ameanza next time atakapoandaa tena nafikiri atafanya vizuri kuanzia jinsi ya kuwatafuata hadi huku kijijini. Tuchukilie mfano wa Bongo Star search ya madam Rita ilivyoanza, ilianza ikiwa na mapungufu lakini ilivyokuja kwa mara ya pili angalau ilionesha kubadilika ukikompare na ile ya kwanza, naamin hata Masoud ataimprove huko mbeleni.

  Ila nashauri wangetoa maybe email address au namba ya simu kwa ajili ya kupokea maoni ya watazamaji.

  Keep it up KP!!!!!!!
   
 17. c

  chichi Member

  #17
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 15, 2007
  Messages: 26
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Sampling ya washiriki hapa inaweza ikawa ni tatizo. Imeonekana washiriki wengi wanauelewa wa kawaida kabisa juu ya mambo ya msingi.
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Hapo umenena mkuu, kwanza kama yupo mhudumu karibu hebu pewa kamoja baridi. Nadhani ni athari za utumwa na ukoloni watu kuona vya kitanzania ni vibaya kushupalia kuponda tuuu!!Kijana wa kitanzania kaanzisha kitu hakina hata muda mfupi badala kuangalia ni jinsi gani anaweza kurekebisha hayo mapungufu watu wanaanza kumpambanisha na big brother, acheni hizo toeni mawazo jenzi sio bomozi. Kwa tasnia ya runinga bado changa na bado tuna safari ndefu, akina masoud wamefungua njia na sisi tu fuate au kama hatuwezi ni bora tukawasaidia badala kukimbilia kumfananisha na big brother. Ungekuwa unajua gharama za kuandaa show ya big brother ana gharama anazotumia masoud ungempongeza KP.
   
 19. D

  Darling Member

  #19
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila kitu local mule.

  masoud amefanya haraka sana kukurusha angefanya utafiti wa kina hata 2-3 years kufanikisha project ile.
  Ikiwa ni pamoja na hata kupata wafadhili wa kuwavisha vijana angalau vitenge vya KTM kuonyesha uwezo wa viwanda vyet n.kSidhani kama big brother was emplemented for six month only.
  Inawezekana nia yake nzuri sana lakini papara ya kutoka imefanya program isieleweke.
   
 20. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  anafanya vizuri sana, nampongeza. acheni majungu.mnamponda ninyi mmefanya nini cha maana? wengine hapa wanaongea kumbe wamekaa bure tu kama bwege.
   
Loading...