Ni kweli inaonekana uelewa wa vijana wetu siku hizi ni mdogo sana sasa sijui ni nini.Ninajoweza kusema ni kwamba vijana wamepoteza ari ya kujisomea mambo yenye kuwaongezea elimu.na kusoma magazeti ya udaku,kusikiliza bongo flavour.na kwenye TV kutazama michezo ya kuigiza tuu.kweli ilinisikitisha sana kwani kwa umri ule mimi niliweza kujua Anti balistic missile ni nini.Niliweza kukuonyesha Kamchatica kwenye atlas iko wapi
Tatizo ni kwamba waTZ wengi hawataki kujiendeleza ili wawe na ufahamu zaidi. Ndio maana waTZ wengi wanabakia kuamini yanayosemwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi ambavyo viko BIASED towards their own views. Nitakupa mifano michache:
1.. Wakati Marekani ikijiandaa kuivamia Irak ya Saddam Hessein, walidai Irak ina silaha za maangamizi. Walidanganya kwani silaha hizo ni 'deterrent', maana yake ni kuwa ukiwa nazo hakuna atakayekuvamia kichwakichwa. UN na Mkaguzi wake mkuu Dk. Hans Blix waliibishia Marekani, lakini ikavamia kibabe. (Wengi mitaani TZ waliamini Irak inazo hizo silaha).
2.. WaTz wengi wanaamini kuwa Wapalestina ni wabaya kwa kuwa wanashambulia Israel kwa kujilipua (suicide bombing). wafahamu kuwa Yassir Arafat aliingia mkenge kwa kusaini mkataba na marekani wakati wa Rais Bill Clinton kukubali kuwa Palestina isiwe na Jeshi hata kabla ya mazungumzo na taifa la Israel linalokalia ardhi ya Palestina. Matokeo yale ni kwamba mpaka leo Israel haionyeshi dalili za kutaka kuondoka kwenye nchi ya Palestina, baili ndio kabisa imejenga ukuta wa kibaguzi kumega maeneo ya wapalestina na kuwafukuza ili kupanua maeneo ya walowezi kutoka Israel. Israel imeendelea kuwashambulia wapalestina miaka yote. Kulle West bank wamekaa kimya kwa kuwa wako chini ya Mahmoud Abbas kibaraka wa Marekani. Kule Gaza hatimaye walichoka kuonewa na kuamua kupambana kwa kutumia silaha walizoweza kupata (mawe, bunduki, makombora madogo ya kujitengenezea wenyewe) dhidi ya silaha za Israel (ndege za kivita, meli za kivita, makombora, silaha za sumu ie. Phosphorus, vikwazo mipaka yote).. Kutokana na propaganda za Magharibi, usishangae ukisikia baadhi ya waTz wakidhani Kujilipua ni ukatili zaidi kuliko mauaji yanayofanywa na Israel ndani ya nchi ya wengine waliyoikalia.
3.. Sheria za kimataifa zanaruhusu nchi zote kuwa na mitambo ya kuzalisha nishati kwa kutumia nguvu za nyuklia. Marekani, huku ikisaidiana na baadhi ya marariki zake wa magharibi, hazitaki nchi wasiopatana nazo ziendelee kwa teknolojia hiyo, pamoja na teknolojia ya kuweka satelaiti anga za juu. Ndio maana inajaribu Kushinikiza Iran isiwe na mitambo ya kuzalisha umeme wa nyuklia, huku ikiruhusu rafiki zake India, Pakistan na Israel kutengeneza na kumiliki SILAHA za nyuklia. Na ndio maana haitaki demokrasia Pakistani kwani rafiki zake akina watashindwa uchaguzi
Pia inajaribu kutumia UN kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini kwa kurusha roketi angani, kitu ambacho kwa sheria za kumataifa ni haki yake. Vyombo vya habari vya Marekani na marafiki na vibaraka wake Marekani vinadanganya kuwa eti wanarusha makombora, kitu ambacho ni uongo.
4.. Even our leaders have fallen into this trap. Our government nowadays fails to take the stand against oppression.
NDIO MAANA MTU ANAPEWA SAHANI YA PILAU AU T-SHIRT ANABADILI CHAGUO LAKE LA KIONGOZI.