Maisha Plus Tv Show ya Masoud Kipanya

Maisha Plus Tv Show ya Masoud Kipanya

nakumbuka machache sana maana most were kind of silly
kwamfano yule kijana kutoka Zanziba alivyokuwa anaulizwa kuhusu afya yake na kwamba voice box yake iko wapi - imekaa sijui kushoto au miguuni...akawa anasema tu DUUH!na kuamini kila alichokuwa anaambiwa na akina Masoud.
Na huyo ndiye mshindi! teh teh teh
 
THE SHOW SIO MBAYA SANA, GOOD IDEA. ILA MIMI NINGESHAURI KUA ZAWADI ISITOLEWE KWA MSHINDI WA KWANZA TU, BALI KWA WASHINDI WATANO WA KWANZA, NI KILA MSHIRIKI KUANDOKA NA KIFUTA JASHO.

WAWE WANASHINDANA KATIKA MICHEZO YA KUTUMIA AKILI ZAIDI KULIKO NGUVU. Pia tungependa kuona kilichotekea kwa yule Binti alie pigwa na gogo, mchezo mzima ulikuaje. Si Hajafa, wasiwasi wako nini?
 
././././././././././loading network./././././././././././../
 
Kweli zawadi za kibongo huwa hazina uhusiano wa Kwanza hadi wa tatu ama wa tano...
kwa bahati mbaya huwa sianga hicho kipindi kwa sababu ya TBCCM, watafute channel or tv station nyingine...
 
Kwa sababu ni lazima kuwe na mshindi wa kwanza, ila sio maana yake amewazidi wenzake kila kitu.
 
kwa mfano, kwa vile tumewashirikisha watu wa nchi jirani, ingependaza kama angalu mmoja wao akawa mshindi wa nafasi yoyote katika tano bora ili kuzidi kuvutia wageni. MWISHO WA SIKU ITAKU MAISHA PLUS BIG BROTHER TANZANIA.
 
Jamani kusema ni rahisi kuliko kutenda. Masoud ni kijana mchapakazi na mbunifu. Wengine wanasema alifukuzwa kazi clouds! sawa, lakini hajakaa na kulialia au kuombaomba kama wanavyofanya watanzania wengi pindi wakutwapo na matatizo. Sidhani kama anajuta kufukuzwa kwake kazi zaidi ya kusema kwamba walichelewa kumfukuza kazi. Binafsi namfagilia sana masoud kwa kipaji chake cha uchoraji na ubunifu wake. Mosoud kipanya na dismas lyasa ni kati ya vijana wachache Tanzania ninao wakubali sana. Hutakatai kukosoana kwa nia ya kujenga lakini nasi tujiulize tumefanya nini kuendeleza maisha yetu na wenzetu wanaotuzunguka. Tuonyeshe basi na sisi vipaji na uwezo wetu katika nyanja tofauti
 
Back
Top Bottom