Maharusi wa siku hizi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maharusi wa siku hizi!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Uncle Jei Jei, Feb 7, 2012.

 1. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,069
  Likes Received: 606
  Trophy Points: 280
  Zamani wakati wa harusi, bibi harusi alikuwa hawezi hata kumtizama padri au mchungaji anapofungisha ndoa! Mda mwingi alikuwa kainama kitu kilichotafsiriwa kuwa alikuwa na aibu aibu na heshima kwa mumewe! Siku hizi mambo tofauti kabisa,! Utakuta bibi harusi katoa macho, muda wote anacheka, achilia mbali wengine kuserebuka ukumbuni mpaka jasho kuwatoka! Kifupi, wengi wao wanakuwa hawana utulivu kama tuliozoe kuuona, kinyume chake mwanaume ndo huonyesha utulivu! Jamani, hii husababishwa na nini?? Wadada mnaotarajia kuolewa, jaribuni kutulia siku ya harusi, msituache na mishangao!
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hizi analysis zingine sijui huwa mnazitoa wapi...
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,052
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wadada kuolewa ni zali siku hizi...
   
 4. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Acha waselebuke maana ni bahati kubwa kwa dunia ya leo kwa binti kuolewa. Wengi wao wamebaki kuzaa tu.
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,138
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  TF hii ni JF zaidi ya uijuavyo
  May be kaona harusi moja au mbili na bi harusi walikuwa hivyo kaja na conclusion yake.
   
 6. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,069
  Likes Received: 606
  Trophy Points: 280
  hudhuria maharusini utayaona!
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hivi kuolewa ni bahati?? Kwanini iwe ni bahati?
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 180
  Nadhani anakuwa na uhakika zaidi as wanakuwa washajuana kitambo tena ukichunguza wengi unakuta ana mimba ya miezi kadhaa.
  Iyo inaweza kuwa inachangia pia
   
 9. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,022
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  we umeliona hlo tu mbn hujazungumzia tendo la ndoa zaman ilikuwa n kama taboo linafanyika gizan hata kuona maungo ya mwanaume n mwiko ikiwezekana mwanamke kafumba macho ila siku hizi tatizo wananyonya wanalamba kila vurugu hata uwanjan watu wapo tayar kufanya.
   
 10. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu bahati ni lugha ya kitakwimu. "Probability" or a "chance of ocurance" siku hizi ni ni ndogo sana.
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,134
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Mmmh, hadi mfumo dume utakapokutoka kichwani
  Utaendelea kuona hayo hayo mauza uza
   
 12. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,163
  Likes Received: 490
  Trophy Points: 180
  Kwa mtazamo wangu maharusi wa zamani walikuwa wanainama kwa kuonesha aibu kwa sababu anakuwa hajazoeana na mwanaume anayemuoa. Lakini siku hizi watu wanafunga ndoa wakati tayari wameshaishi pamoja, wameshazaa kwa kifupi wanabariki ndoa maana tayari wameshakuwa mwili mmoja, kwa hiyo bi harusi hawezi kuinama
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Sasa mtu hata kucheka siku ya harusi yake mnaanzishia thread? Kweli Watanzania mna mambo.
   
 14. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii nayo ni sababu ya msingi sana.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,025
  Likes Received: 5,193
  Trophy Points: 280
  kwa wakristu harusi ni tendo la mara moja maishani kwa nini asifurahie?
  kwa nini asimuangalie mchungaji ? kwani anang'ata?
  na kuna mengi yanaweza kutokea kipindi cha maandalizi ya harusi, mnaposimama altareni waacheni wajinafasi
   
 16. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Swala si kucheka. Aibu na staha kwa mwanamke ina raha yake. Siku hizi mmetuzoea sana.
   
 17. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,609
  Likes Received: 412
  Trophy Points: 180
  Waulize wadada kwa PM watakwambia kwanini? Lakini hapa jamvini hawatathubutu na wanakuwa wakali sana Lol
   
 18. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,052
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hawacheki wanaserebuka sana hadi bwana harusi anaona aibu yeye inabidi atizame chini.
   
 19. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2012
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 821
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Zamani walikuwa wanatembea kwa miguu ama kupanda punda, kulikuwa hakuna magari. Wakabadili wakaanza kupanda baiskeli, hamjauliza kwa nini wamekiuka maadili, wakabadili wanapanda magari wamevaa mavazi ya kizazi cha leo. Kila kitu kinabadilika kuendana na wakati, kizazi kijacho kama utakuwa hai, utaona na wao wana staili yao utakayoiita ya ajabu. We zoea staili ya kizazi chako, vizazi vyao waachie wenyewe, Kwishney.
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Hiyo staha na aibu mnapima kwa kijiko kipi? Cha chakula au cha chai? Alafu aone aibu kwani anakua mtupu? Embu acheni umbea. . .harusi za watu wengine zinawauma kisa? Subirini zenu muwaambie kabisa wake zenu hamna kufanya hili wala lile, sio mnapangia watu wengine.
   
Loading...