THE SPIRIT THINKER
JF-Expert Member
- Sep 9, 2019
- 388
- 552
KITABU CHA KWANZA
Nyuma ya mafanikio yeyote kuna uhalifu.
- BALZAC
Sura ya kwanza
Amerigo Bonasera alikuwa ameketi ndani ya jengo namba tatu la mahakama kuu ya kihalifu la New York akisubiri haki itendeke; alipiwe kisasi kwa wanaume ambao walikuwa wamemjeruhi binti yake kikakitili wakijaribu kumbaka.
Jaji, bwana mmoja mwenye mwili mkubwa, alikunja nguo yake kuipa hewa mikono huku akiwaangalia kwa umakini vijana wawili waliokuwa wamesimama mbele ya dawati lake. Uso wake ulikuwa mkavu ukionesha nuru ya madaraka aliyokuwa nayo. Lakini kulikuwa na kitu ndani ya muonekano huo ambacho Amigo Bonasera alihisi, ila hakuelewa kilikuwa ni nini.
“Mmeonesha tabia mbovu sana,” Jaji alisema kwa ukali.
Ndiyo, ndiyo, alijiwazia Bonasera. Wanyama. Wanyama.
Wale vijana waliinamishwa vichwa vyao chini kwa aibu.
“Mmeonesha tabia mbovu sana na bahati yenu hamkumbaka huyo binti. Vinginevyo ningewaweka nyuma ya nondo kwa miaka ishirini.” Jaji alitulia, macho yake yakahama kumtazama Amerigo Bonasera, halafu akayahamisha tena kutazama karatasi zilizokuwa juu ya dawati lake. Aliguna kabla ya kuongea tena.
“Lakini kwa sababu ya umri wenu, na kwakuwa hamna rekodi yeyote mbaya, kwa sababu ya familia yenu ambayo pia inaishi kwa kufuata sheria, na kwa sababu lengo la sheria sio kulipa kisasi, nitalifuta hili shauri.”
Ni kwa uzoefu wa mikasa ya hapa na pale kwa zaidi ya kipindi cha miaka kumi uliomfanya Amerigo Bonasera asioneshe chuki na hasira yake waziwazi. Binti yake mpendwa alikuwa bado yupo hospitalini huku taya zake zikiwa zimeshonwa baada ya kuvunjwa na hawa wanyama wawili; na bado sheria ilisema wataachiwa huru? Ilikuwa ni maumivu. Aliwatazama wazazi wa wale wanyama wawili wakiwakumbatia vijana wao. Familia yote ilikuwa na furaha na nyuso zao zilionesha tabasamu.
Mate machungu yalipanda hadi kooni kwa Bonasera. Akayazuia kwa meno yake yaliokuwa yameumana. Alisimama kipindi wale vijana wawili wanampita kutoka nje ya mahakama wakiwa wanajiamini, macho yao yakionesha ushindi. Aliwaacha wapite bila kusema neno lolote.
Wazazi wa wale wanyama walikuwa wanafuatia kwa nyuma, walikuwa na umri sawa na wa kwake. Walimtazama Bonasera kwa aibu, ila macho yao yalionesha wanashangilia ushindi walioupata.
Bonasera alishindwa kujizuia na kujikuta akiropoka, “Mtalia kama jinsi nilivyolia na kuomboleza – Nitahakikisha nawafanya mlie kama vijana wenu
walivyosababisha mimi nilie.”
Wakili wa utetezi alitokea kwa nyuma na kuwasukuma wateja wake waondoke. Kundi la askari lilitokea kumkinga Amerigo Bonasera. Hata hivyo haikuwa inahitajika kufanyika hivyo.
Katika miaka yake yote aliyoishi Marekani, Amerigo Bonasera aliamini kwenye sheria na ustaarabu. Na alikuwa amefanikiwa katika hilo. Lakini sasa hivi, akili yake ilikuwa imejaa chuki na hasira. Ingawa akili na mifupa ya fuvu lake ilikuwa imejawa na mawazo mabaya ya kwenda kununua bunduki na kuwaua wale vijana wawili, Bonasera alimgeukia mke wake na kumfafanulia, “Wametufanya wajinga.” Alitulia halafu akapata maamuzi ya mwisho, bila kuogopa gharama na hasara za uamuzi wake. “Ili haki itendeke ni lazima tukampigie magoti Don Corleone.”
Kwenye hoteli moja iliyopambwa kwa samani za gharama, Jonny Fontane alikuwa amelewa kwa wivu kama mume wa mwanamke yeyote. Akiwa kajilaza kwenye sofa jekundu, alikunywa pombe kali na kuikata ladha yake kwa kufakamia maji ya baridi. Ilikuwa ni saa kumi alfajiri na alikuwa na mawazo kedekede juu ya kumuua mke wake pindi atakapofika nyumbani. Hiyo ni kaama angerudi nyumbani usiku huu. Ilikuwa ni muda mbaya wa kuanza kumpigia simu mke wake wa kwanza ambaye walikuwa wameachana na kuanza kumuuliza kuhusu watoto au kuanza kuwapigia simu marafiki zake kuwaeleza anayopitia. Kuna kipindi wangefurahishwa na Jonny kuwapigia simu muda kama huo , lakini kwa sasa alikuwa ni kero kwao.
Akiwa anaendelea kuushusha mvinyo wake, alisikia mke wake akifungua mlango, lakini aliendelea kunywa hadi mke wake alipofika sebuleni na kusimama kando yake. Alikuwa ni mwanamke mzuri, mwenye uso wa malaika, macho yenye mvuto wa ajabu na mwenye mwili wenye kila mvuto kwa mwanamume yeyote. Kwenye runinga uzuri wake ulikuwa ni maradufu ya hapo. Mamilioni ya wanaume ulimwenguni walikuwa wanavutiwa na Margot Ashton. Na walikuwa tayari kulipa fedha nyingi ili tu wautazame uso wake kwenye sinema.
“Ulikuwa wapi?” Johnny Fontane aliuliza
“Nilikuwa nafanya mapenzi,” Alijibu Margot.
Alikuwa anadhani Johnny kalewa. Ila alishangaa kumuona Johnny ananyuka kwa kasi na kumkaba shingo. Lakini ile sura ya malaika na macho yenye mvuto, Johnny Fontane alisalimu hasira zake na kuwa mnyonge tena. Margot alifanya kosa jingine, alitabasamu kwa namna ya kumkebehi Johnny ambaye aliinua mkono wake kumpiga ngumi.
“Usinipige usoni, Johhny. Kuna filamu tunaanza kushuti hivi karibuni.”
Margot alikuwa anacheka. Johnny alikuwa anampiga ngumi za tumboni hadi akaanguka chini. Johnny alimrukia kwa juu. Aliendelea kumpiga ngumi kwenye mapaja na miguuni. Ilikuwa ni adhabu kali. Laiti kama angelikuwa anampiga vile usoni, basi angemharibu sura au kumtoa meno kabisa.
Hata hivyo hakuwa akimpiga kwa nguvu sana.
Asingeweza kufanya hivyo. Na Margot alilifahamu hilo.
Johnny Fontane aliinuka juu. Alikuwa anamchukia yule mwanamke pale chini, lakini uzuri wake ulikuwa ni kama kinga fulani ya maajabu. Margot pia aliinuka kutoka sakafuni. Alianza kuchezacheza huku akiimba, “Johnny usiwahi kuniumiza, Johnny usiwahi kuniumiza.” Halafu ghafla akasema, “Mjinga mkubwa, unanipiga kama mtoto mdogo. Kwanza haujui mapenzi na ukiwa kitandani unakuwa kama mtoto. Unadhani mapenzi ni kama hizo nyimbo zako ulizokuwa unaimba zamani?”
Halafu Margot akakimbilia chumbani na kujifungia.
Johnny aliketi sakafuni. Dharau aliyooneshwa ilimkera. Lakini ugumu na ujasiri uliomfanya akaishi kwenye ulimwengu wa Hollywood ulimfanya anyanyue simu ya mezani na kuomba gari kwaajili ya kumpeleka uwanja wa ndege. Kulikuwa na mtu mmoja tu ambaye angeweza kumsaidia. Angerudi zake New York. Angeenda hadi kwa mtu huyo mwenye busara na upendo. Baba yake wa kufikia Don Corleone.
Wote hawa na wengine wengi walikuwa wamepokea mwaliko kwenye harusi ya Miss Constanzia Corleone ambayo ingefanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa nane 1945. Baba wa bibi harusi, Don Vito Corleone, hakuwahi kuwasahau marafiki na jirani zake ingawa kwa sasa alikuwa anaishi kwenye jumba lake kubwa la kifahari. Mapokezi ya wageni wote yangefanyika ndani ya jumba hilo halafu sherehe zingeendelea siku nzima. Hakuna ubishi hili lingekuwa ni tukio la kipekee. Vita kati ya Marekani na Wajapani ilikuwa imeisha kwahivyo kusingekuwa na usumbufu wowote. Asingetokea mtu yeyote wa serikalini kuomba watoto wa kiume wa Don Corleone kwenda kusaidia taifa kupambana kwenye vita hiyo. Hata hivyo, harusi ndiyo sehemu pekee ambayo watu wangeitumia kuonesha furaha yao.
Kwahivyo Jumamosi asubuhi rafiki za Don Corleone walifurika kutoka New York kuonesha heshima. Wengi walikuwa wamebeba bahasha zilizowekewa pesa kama zawadi za maharusi, hakukuwa na cheki za benki. Ndani ya bahasha kulikuwa na kikaratasi kilichoonesha jina la mtu aliyeileta zawadi kuonesha kuwa alimheshimu Godfather. Heshima ambayo ama kwa hakika ilitafutwa kwa muda mrefu.
Don Corleone alikuwa ni mtu ambaye kila mwenye shida alikuja kwake kuomba msaada, na hakuwahi kuwaangusha watu wake. Hakuwahi kutoa ahadi za uongo, au sababu za kujitetea kwamba mikono yake ilikuwa imewekewa mipaka na watu wenye nguvu zaidi duniani kuliko yeye. Ilikuwa sio lazima awe rafiki yako, au eti uwe na uwezo wa kumlipa ndiyo akusaidie! Kitu kimoja tu ndicho kilikuwa kinatakiwa. Kwamba, wewe mwenyewe, ukiri urafiki wako kwake. Halafu haijalishi hali yako ya kiuchumi, Don Corleone angelichukua tatizo lako kama tatizo lake kwa moyo mmoja. Na asingeruhusu kitu chochote kisimame njiani kuzuia utatuzi wa tatizo la mtu yeyote. Malipo yake? Urafiki, heshima ya jina la “Don”, na wakati mwingine furaha ya kuitwa “Godfather.” Au kumuonesha heshima tu. Hakuwa akilenga faida yeyote. Zawadi ndogondogo kama asali au mkate vilitosha sana. Hata hivyo, ilieleweka kuwa ni tabia njema kujiona upo kwenye deni naye na kwamba alikuwa na haki ya kukuita wakati wowote na kukuomba ulilipe deni lake kwa msaada wa huduma ndogondogo.
Sasa leo hii, kwenye harusi ya binti yake, Don Vito Corleone alikuwa amesimama kwenye mlango wa jumba lake kubwa la kifahari kuwasalimia wageni wake wote waliokuwa wanafika hapo. Wengi wakiwa ni wale anaowafahamu na kuwaamini. Maisha mazuri waliyokuwa wakiishi yote ilikuwa ni kwa sababu ya Don na hawakuona aibu kumuita Godfather mbele ya uso wake. Hata watu ambao walikuwa wanashughulikia maandalizi ya harusi walikuwa ni rafiki zake. Aliyekuwa anasimamia vinywaji alikuwa ni bwana mmoja ambaye zawadi yake kwenye harusi hii ni vinywaji vyote vitakavyotumika. Wahudumu wengine walikuwa ni marafiki za watoto wa kiume wa Don Corleone. Chakula kilichokuwa kwenye meza mbalimbali kilikuwa kimepikwa na mke wa Don akishirikiana na marafiki zake na ukumbi ulikuwa umepambwa na rafiki wa binti yake Don Corleon ambaye alikuwa anaolewa leo.
Don Corleone alikuwa ni rafiki wa kila mtu. Aliwapokea maskini na matajiri, watu wenye ushawishi na nguvu na hata wale wanyonge – na aliwaonesha upendo sawasawa. Hakumbagua yeyote. Hiyo ndiyo ilikuwa hulka yake. Na wageni walimsifia sana kwa suti aliyokuwa amevaa. Ilimkaa vizuri sana kiasi kwamba kwa mtu ambaye hakuwa anamfahamu angehisi yeye, Don Corleone, ndiye bwana harusi mwenyewe.
Mlangoni alikuwa amesimama na vijana wake wawili kati ya watatu. Mkubwa kabisa, alibatizwa kwa jina la Santino ila wengi walimwita Sonny isipokuwa Don mwenyewe. Sonny Corleone alikuwa mrefu wa futi sita, na nyewele zake zilimfanya aonekane mrefu zaidi. Uso wake ulikuwa mpana na mashavu yake yalikuwa na mashimo. Alikuwa na nguvu kama za ng’ombe dume na ilikuwa inafahamika alikuwa na maumbile makubwa kiasi kwamba mke wake alikiogopa kitanda cha ndoa kama wanaoamini katika dini wanavyoogopa moto wa jehanamu. Inasemekana alipokuwa mdogo alikuwa amepita kwenye madanguro mengi, hata wanawake ambao walikuwa makonkodi kwenye biashara ya kujiuza walipoona maumbile yake waliomba awaongezee pesa ya malipo.
Leo, hapa kwenye harusi, baadhi ya wasichana waliofika walikuwa wanampima Sonny kwa macho ya wiziwizi huku wakimtega. Lakini kwa siku ya leo walikuwa wanapoteza muda wao tu. Licha ya uwepo wa mke wake na watoto wake watatu, Sonny Corleone, alikuwa na mipango na msindikizaji wa dada yake kwenye harusi, Lucy Mancini. Lucy, akiwa anafahamu kila kitu alikuwa amekaa bustanini. Alikuwa amejaribu kumchombezachombeza Sonny kwa takribani wiki nzima iliyopita na alikuwa amefanikiwa kumshika Sonny maungoni.
Hakujali kwamba, Don Corleone, hakuwa akimuona Sonny kama mtoto wake bora. Sonny Corleone alikuwa na nguvu, alikuwa ni jasiri. Alikuwa na utu na moyo wake ulikuwa mkubwa kama yalivyokuwa maumbile yake. Lakini hakuwa na uvumilivu kama wa baba yake. Yeye alikuwa ni mwepesi wa hasira ambazo mara nyingi zilimpelekea kufanya makosa kwenye maamuzi yake. Ingawa alikuwa na msaada mkubwa kwenye biashara za baba yake, bado wengi hawakumuona kama angekuja kurithi uendeshaji wa biashara ya baba yake siku akifariki.
Kijana wa pili alikuwa ni Fredrico, wengi walimwita Fred au Fredo. Alikuwa ni aina ya mtoto ambaye wazazi wengi wa kiitalia walifunga na kumuomba Mungu awapatie mtoto kama huyo. Alikuwa mwaminifu, na alikuwa yupo tayari kufanya lolote kwaajili ya baba yake na hata akiwa na umri wa miaka thelathini bado alikuwa akiishi na wazazi wake. Alikuwa ni mfupi, hakuwa na uzuri wowote ila sura yake ilionesha alikuwa ni mmoja wa wanafamilia wa Don Corleone. Hakuwahi kumkera baba yake au kumuudhi, lakini licha ya yote hakuwa na ule muonekano au viashiria vya kiongozi, hivyo yeye pia hakutazamiwa kama atamrithi Don Corleone.
Mtoto wa tatu, Michael Corleone, hakuwa amesimama na ndugu zake au baba yake. Alikuwa amejitenga upande wa bustani kwenye kona ya mwisho kabisa. Lakini hata akiwa huko bado macho ya wageni yaliweza kumfikia.
Michael Corleone alikuwa ni mtoto wa mwisho wa Don na mtoto pekee ambaye alikataa kuishi kwa maelekezo ya baba yake. Sura yake haikutofautiana sana na ya ndugu zake. Ngozi yake ilikuwa na rangi ambayo kama ingelikuwa kwa msichana basi msichana huyo ataitwa mrembo. Ama kwa hakika Michael alikuwa ni handsome. Kuna kipindi baba yake alihofia kuhusu ushababi wa mtoto wake huyo. Hofu ambayo ilifutwa siku ambayo Michael Corleone alifikisha miaka kumi na saba.
Sasa hivi huyu mtoto alikuwa amekaa peke yake kuonesha alikuwa amejitenga na baba yake na familia yake. Pembeni yake alikuwa amekaa binti wa kimarekani ambaye kila mtu alikuwa amesikia habari zake na leo ndiyo walikuwa wanamuona kwa mara ya kwanza. Michael alikuwa ametumia heshima na kumtambulisha msichana wake huyo kwa kila mtu, ikiwemo familia yake. Na kusemwa kweli hawakuvutiwa naye. Alikuwa ni mwembamba sana, wa kawaida, uso wake ulipaswa kuwa kwa mtu mwenye jinsia ya kiume. Jina lake pia lilikuwa la ajabu masikioni mwao; Alikuwa anajiita Kay Adams. Laiti kama angewaambia kwamba jina lake ni la kawaida tu kwenye tamaduni ya Marekani wangeguna.!
Kila mtu aligundua pia Don hakuwa anamzingatia sana kijana wake huyu wa tatu. Kabla ya vita Michael alikuwa ndiye kijana pendwa wa Don Corleoe na alimchagua awe mrithi wa biashara zote za familia wakati sahihi utakapofika. Michael alikuwa na sifa za utulivu na akili kama ya baba yake, na alikuwa amezaliwa tu na uwezo wa kuwafanya watu wafanye vitu kwa amri yake. Lakini vita vya pili vya dunia vilipoanza, Michael Corleone alijitolea kupigana na jeshi la majini.
Aliipinga amri ya baba yake kwa kufanya hivyo.
Don Corleone hakuwa na lengo, au nia, ya kumwacha kijana wake mdogo akauawe kwenye uwanja wa vita kuitetea nchi ya kigeni. Madaktari walihongwa, na vikao vya siri vilifanyika. Kiwango kikubwa cha pesa kilitumika kuhakikisha haingii vitani. Lakini Michael alikuwa na miaka ishirini na moja na hakuna kitu kingeweza kufanyika kubadilisha maamuzi yake.
Alijiandikisha na kupigania ukanda wa bahari ya Pasifiki. Akawa Kapteni na kushinda medali nyingi.
Mwaka 1944 picha yake ilichapishwa kwenye gazeti la Life Magazine na maandishi ya kazi alizozifanya. Rafiki mmoja wa Don Corleone alimuonesha gazeti hilo Don, na Don aliguna kwa huzuni na kusema, “Anayafanya hayo
yote kwa watu baki tu anaisahau familia yake.”
Michael alipotolewa jeshini mwaka 1945 ili kuuguza majeraha yake, hakuwa anafahamu baba yake ndiyo alikuwa ameandaa mipango yote hadi atolewe jeshini. Alikaa nyumbani kwa wiki chache tu, halafu, bila kuzungumza na yeyote, akajiunga na chuo cha Dartmouth College kilichopo Hanover. Kwa hivyo akawa ameondoka nyumbani kwao. Muda ulikuwa umepita hadi leo aliporejea nyumbani tena kwaajili ya harusi ya dada yake na kuwatambulisha mchumba wake huyu ambaye hakuwavutia.
Michael Corleone alikuwa anamuonesha Kay Adams ucheshi kwa kumwambia hadithi za hapa na pale kuhusu wageni waliokuwa wamefika harusini hapo. Hata hivyo mawazo ya Kay Adams yalikuwa kwa kile kikundi kidogo cha watu waliojetenga kwenye meza yao
wakinywa mvinyo. Watu hao walikuwa ni Amerigo Bonasera, Nazorine, Anthony Coppola na Luca Brasi. Kwa mawazo yake, Kay Adams aligundua watu hawa hawakuwa na furaha.
Michael alitabasamu, “Hawana furaha ndiyo,” Michael alisema. “Hapo walipo wanasubiri wakutane na
baba. Lazima kuna kitu wanataka awasaidie.”
Na hilo lilionekana kwenye macho ya wanaume wale, kila mara macho yao yalikuwa kwa Don Corleone.
Don Corleone alikuwa bado amesimama akiwasalimia wageni wake wa hapa na pale, Chevrolet nyeusi iliingia na kuegeshwa upande wa pili. Wanaume wawili waliokuwa ndani ya gari hilo walichomoa vijitabu na kuanza kuandika namba za sahani za magari yaliokuwa yameegeshwa pale. Sonny alimgeukia baba
yake. “Wale jamaa, lazima ni asakri.”
Don Corleone alijibu, “Siumiliki mtaa mimi, kwahivyo wanaweza kufanya wanachojisikia.”
Uso wa Sonny ulibadilika kuwa mwekundu kwa hasira. “ Wale wajinga hawana heshima kabisa.”
Alizishuka ngazi za nyumba na kwenda hadi ile gari ilipokuwa imeegeshwa. Akauweka uso wake karibu na wa yule dereva, ambaye hakutetemeka. Baadala yake aliingiza mkono mfukoni na kutoa kadi ya utambulisho.
Sonny akapiga hatua kuondoka bila kusema kitu. Akatema mate chini yakaruka kwenye kioo na kuondoka. Alifanya hivyo kwa maksudi ili yule dereva ashuke kumfuata kwenye nyumba, lakini yule dereva hakufanya hivyo.
Alipofika aliposimama baba yake alisema, “Wale jamaa ni FBI. Nimeona wanaandika namba zote za magari yaliyopo hapa. Wajinga wakubwa.”
Don Corleone alikuwa anawafahamu ni akina nani. Hivyo marafiki zake wa karibu sana alikuwa amewashauri waje nyumbani hapo kwa kutumia magari ambayo sio ya kwao. Na ingawa hakupenda alichokifanya Sonny, lakini aliona tukio lile lilikuwa na faida.
Ingewashawishi wale jamaa kuwa ujio wao ulikuwa ni wa kushtukiza na hawakuwa wakitegemewa. Kwahivyo Don hakuwa amekasirika. Alikuwa amejifunza zamani za kale kwamba, Jamii huwa inatoa dharau ambazo ni za kupuuza, na kwamba kwenye huu ulimwengu huwa kuna nyakati ambapo mtu mnyonge zaidi, kama akiyafumbua macho yake, anao uwezo wa kumshinda mtu yeyote mwenye nguvu na ushawishi. Ni jambo hili lililomfanya Don Corleone asipoteze heshima kutoka kwa marafiki zake.