Mahakama yatupilia mbali Kesi ya Mbowe ya Kikatiba dhidi ya IGP, DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
499
1,000
Nimesoma sababu za kufutwa kwa kesi ya kikatiba zilizotolewa
a mahakama Kuu ya Tanzania, naomba niseme poleni mnaosoma mkituaminisha mnakuja kufanya mabadiliko ya kifikra kwenye Taifa hili. Nawapa pole kwa sababu kwa Aina hii ya maamuzi sidhani Kama huko tuendako kutakuwa na kesi za miaka ya karibuni za kufanyia rejea. Mahakama iliondoka na akina Jaji Samatta.
Mahakamaba 23, 2021 imeifuta kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na, @freemanmbowetz, kutokana na kilichoelezwa kuwa kuwepo kwa kesi ya msingi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, hivyo malalamiko yake ayawasilishe huko yataweza kushughulikiwa.
 

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,293
2,000
Leo Sept. 23, 2021 saa nane kamili mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam itatoa uamuzi mdogo juu ya mapingamizi ya Serikali katika Kesi ya Kikatiba namba 21/2021 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chasema Freeman Mbowe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na IGP.

Wakati anakabiliwa na Kesi ya Ugaidi, Mbowe alifungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu dhidi ya Serikali akipinga taratibu za kukamatwa na kushtakiwa kwake.

Miongoni mwa madai yake, Mbowe anapinga kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi kimyakimya bila kumtaarifu kwanza kuhusu mashtaka hayo pamoja na maneno ya vitisho anayodai kupewa na polisi kabla ya mashtaka hayo.

Vilevile mwanasiasa huyo anelalamikiwa haki zake kukiukwa kwa ndugu na wakili wake kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilishwa.

Mbowe anadai wakati ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa ofisa wa polisi.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe katika hati ya kiapo chake kinachounga mkono madai yake anazitaja kauli hizo anazodai kuwa zilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni (RPC), aliyemtaja kwa jina Ramadhani Kingai kuwa:

“Wewe si unajifanya unaijua Katiba Mpya, safari hii huchomoki, tunakupiga kesi ya ugaidi”, inasomeka sehemu ya hati ya kiapo hicho cha Mbowe.

Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi kimyakimya katika kesi aliyoungianishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka 2020.

Alisomewa mashtaka hayo bila kuwepo mawakili, wanafamilia wala wanahabari kisha akapelewa rumande kwa kuwa mashtaka hayo hayana dhamana.

Kabla ya hatua hiyo Mbowe alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku tano tangu alipotiwa mbaroni Julai 21, 2021 usiku akiwa jijini Mwanza alikokwenda kwa maandalizi ya kongamano la kudai Katiba Mpya lililokuwa limeandaliwa na Baraza a Vijana wa Chadema (Bavicha).

Usiku huohuo alisafirishwa mpaka Dar es Salaam hadi nyumbani kwake ambako alifanyiwa upekuzi kisha akashikiliwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay hadi alipopandishwa kizimbani.

Wakati akiendelea na Kesi ya Ugaidi, Mbowe kupitia kwa wakili wake, Peter Kibatala alifungua kesi ya Kikatiba dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu.

Katika kesi hiyo namba 21 ya mwaka 2021, Mbowe anadai kuwa mdaiwa wa kwanza (DPP) na wa pili (IGP) walikiuka haki zake za kikatiba kwa kumfungulia kesi nzito ya kikatiba bila kwanza kumtaarifu kwa maandishi na kumwezesha kuwasiliana na wakili wala ndugu zake.

Hivyo, anaiomba Mahakama Kuu itoe nafuu mbalimbali ambazo ni pamoja na masharti ya lazima ya vifungu namba 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na Sheria ya Kudhibiti Uhalifu wa Kupanga na Uhujumu Uchumi, Sura ya 200.

Vifungu hivyo vinatoa sharti la lazima kwa ofisa wa polisi anayemshtaki mtuhumiwa na kwa mahakama ambako mtuhumiwa anashtakiwa kumjulisha mshtakiwa kwa maandishi kuwa atashtakiwa makosa husika, lakini pia vinampa fursa ya kuwasiliana na ndugu na wakili wake kuhusiana na mashtaka hayo.

Vilevile mahakama hiyo inaombwa itamke kuwa kifungu cha 29(1) cha sheria hiyo ya uhujumu uchumi kinachotoa sharti la lazima kwa ofisa wa polisi anayemshikilia mtuhumiwa mahabusu amfikishe katika Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu Mkazi ndani ya saa 48, tangu kukamatwa kwake, kilikiukwa.

Mbowe pia anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa DPP na AG walikiuka haki zake zinazotolewa na kulindwa chini ya masharti ya kifungu cha 29 (1) cha Sheria ya Uhujumu.

Anabainisha kuwa pamoja na mambo mengine, madai hayo yanalenge kuzuia matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi ambako mtuhumiwa anakuwa amewekwa mahabusu baada ya kutiwa mbaroni.

Anadai kuwa alipokuwa akishikiliwa mahabusu aliwekwa katika mazingira yasiyofaa, ikiwemo kulala sakafuni (bila matandiko yoyote) kuanzia Julai 21 alipokamatwa jijini Mwanza mpaka Julai 26, 2021 alipopandishwa kizimbani.

Mbowe pia anaiomba mahakama itamke kuwa DPP na IGP pamoja na Mahakama ya Kisutu, ikitenda kwa amri ya DPP na AG, walikiuka haki zake zinazolindwa na masharti kifungu cha 29 (2) na (3) cha sheria ya uhujumu uchumi kwa kushindwa kumjulisha kwa maandishi kwamba atashtakiwa kwa mashtaka mazito chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Zaidi soma:

Thread 'Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP' Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP


Wazee wa PGO kuna mchochozi huko Marekani nendeni mkamuarest Haraka anatupaka matope.E_-SxKVWYAAQWsQ
 

mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,846
2,000
Kesi ya kikatiba iende uhujumu uchumi tena?
Hakuna tatizo la katiba, kuna tatizo la ki utaratibu, Mbowe anaamini taratibu hazikuafuatwa wakati anakamatwa, ana uwezo wa kupungua hilo ndani ya kesi yake kama wanavyo pinga saivi maelezo ya washtakiwi wengine yasikubuliwe kama ushahidi katika kesi ndogo inayo endelea. Kwa lugha rahisi, mawakili wa Mbowe walikurupuka ili kufurahisha genge na vigelegele vya watu wao.
 

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,367
2,000
Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliyekuwa akipinga namna alivyowekwa kizuizini na kulazwa sakafuni kwa siku tano bila kufikishwa mahakamani.

Mbowe alifungua kesi hiyo Julai 30, mwaka huu akilalamikia namna alivyotiwa mbaroni jijini Mwanza kuweka mahabusu ya polisi kwa siku tano bila kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 kama sheria inavyoelekeza.

Kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzania pia alikuwa akilalamika kiulazwa sakafuni bila matandiko uyoyote wakati akiwa mahabusu.

Katika kesi hiyo namba 21 ya 2021, Mbowe alikuwa akipinga kufikishwa mahakamani bila kuwajulisha mawakili wake au ndugu zake na kabla ya kujulishw kwa maandishi kuhsu mashtaka yaliyokuwa yakumkabili.

Katika kesi hiyo aliyoifungua dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mbowe alikuwa pia akipinga kusomewa mashtaka ya ugaidi yanayomkabilia bila kuwa na wakilia wala kupewa hati ya mashtaka.

Mbowe alikuwa akidai utaratibu huo ulikiuka haki zake za kikatiba, huku akiiomba mahakama hiyo itamke kuwa haki zake zilikiukwa.

Uamuzi wa kuitupa kesi hiyo umetolewa leo Alhamisi Septemba 23 na Jaji John Mgetta aliyesikikiza pingamizi hilo la Serikali kwa niaba ya jopo la majaji watatu waliokua wamepangwa kusikiliza kesi hiyo, akiwemo Jaji Leila Mgonya na Jaji Stephen Magoiga.

Majaji hao wamekubaliana na pingamizi la Serikali lililokuwa na hoja nne lililotaka kesi hiyo isisikilizwa kwa madai ya kuwa na kasoro nyingi za kisheria.

Mahakama Kuu imekataa hoja tatu za pingamizi la Serikali na kubaliana na hoja moja tu ya pingamizi la Serikali iliyodai kuwa Mbowe hakutumia njia nyingine zilizopo kutafuta haki anazodai kabla ya kufungua kesi ya kikatiba.

Mahakama amekubaliana na Serikali kupitia jopo la mawakili wa Serikali lililoongozwa na Wakili wa Serikali Hangi Chang'a kuwa kwa kuwa kuna kesi ya jinai dhidi yake (Mbowe), basi madai yake alipaswa kuyaibua katika Mahakama hiyo kwanza kabla ya kufungua kesi ya kikatiba.

"Kwa hiyo nakubaliana na pingamizi hili la wajibu maombi kwamba hii ni hoja ya kisheria na kama alivyoeleza Wakili Mkuu wa Serikali, Mussa Mbura katika hoja za maandishi, Mahakama inayosikilizwa kesi yake (Mbowe) ya uhujumu uchumi ndiyo mahakama sahihi. Hivyo alipaswa kutoa madai yake huko kwanza," amesema Jaji Mgetta.

Chanzo: Mwananchi
 

Kamugumya

JF-Expert Member
Aug 18, 2021
673
1,000
Toka kizazi cha majaji tajika kama Jaji Lugakingira,Jaji Kati,Jaji Mapigano,Jaji Mwalusanya,Jaji Chipeta na wengine wa aina hiyo waliokuwa real bold spirted judges,kwa sasa tuna kizazi cha majaji wasiojielewa na wasiomjua nguvu waliyonayo katika kusimamia Uhuru wa muhimili wa mahakama katika kutenda haki. Inasikitisha.
 

stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
5,366
2,000
Toka kizazi cha majaji tajika kama Jaji Lugakingira,Jaji Kati,Jaji Mapigano,Jaji Mwalusanya,Jaji Chipeta na wengine wa aina hiyo waliokuwa real bold spirted judges,kwa sasa tuna kizazi cha majaji wasiojielewa na wasiomjua nguvu waliyonayo katika kusimamia Uhuru wa muhimili wa mahakama katika kutenda haki. Inasikitisha.

wakina mdude walivoachiwa muhimili ulikua vizuri ila alipowekwa hatiani mzee baba muhimili mbovu
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,768
2,000
Kumbe mahakama haijakataa hoja za Mbowe ila imeelekeza kwamba, kwa kuwa kesi ya msingi iko mahakama kuu, kitengo cha Uhujumu uchumi, basi huko ndiko mahali sahihi kupeleka madai yake...

On the other hand, kama Jaji angekubaliana na hoja za mleta pingamizi (ambazo obviously ziko sahihi), maana yake alikuwa anaifuta kabisa kesi ya Msingi iliyoko mahakama kuu kitengo cha makosa ya uhujumu uchumi...!

Ndiyo maana, Jamhuri wiki hii yote imesimama kuendelea na usikilizaji wa shauri hili ili kupima na kujadiliana namna ya kulimaliza pingamizi hilo...
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,055
2,000
Mhimili uko kazini

Mungu ibariki Tanzania
Unatakiwa pia kusema Mungu Mbariki Mbowe ili atoke mapema huko korokoroni! Maana hata wewe kada wa ccm, unatambua fika hii kesi ni ya kubambikiwa na polisi wakishirikiana na mfumo, kwa lengo tu la kumkomesha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom