Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Mahakama ya Korona Kinondoni Jijini Dar es Salaam, imetoa hukumu hiyo Ijumaa Septemba 22, 2023 imetoa uamuzi wa uchunguzi ilioufanya kuhusu mazingira ya kifo cha Stella Moses ambaye alifariki akiwa mahabusu katika Kituo cha Polisi Mburahati, Desemba 20, 2020, ambapo imesema kifo chake kilisababishwa na mtuhumia kujinyonga.
Katika uamuzi huo Mahakama imesema kujinyonga kulifanyika licha ya mwili wake kukutwa na majeraha kichwani na shingoni.
Stella Moses akiwa na umri wa miaka 30, alijisalimisha kituoni hapo baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa anahitajika, baadaye ikatangazwa kuwa amefariki, tukio ambalo lilizua mvutano mkubwa baina ya Polisi na ndugu wa marehemu kwa kile wanachodai kuna mazingira tata ya kifo hicho.
Ndugu wa marehemu waliamua kufungua kesi Mahakamani dhidi ya Jeshi la Polisi na Hospitali ya Taifa Muhimbili wakitaka uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.
Walifungua shauri hilo baada ya kutoridhika na upelelezi, mwenendo wa uchunguzi wa tukio na sababu za kifo hicho, hivyo wakitaka ufanyike uchunguzi huru.
Shauri hilo lilifunguliwa na shemeji wa marehemu, Emmanuel Kagongo kwa niaba ya familia ya marehemu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam, Kivukoni (Kinondoni) kupitia kwa wakili Peter Madeleka.
Itakumbukuwa naada ya kifo cha Stella, Jeshi la Polisi kupitia aliyekuwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Ramadhani Kingai, lilitoa taarifa kuwa Stella, mama wa Watoto wawili amefariki Dunia baada ya kujinyonga akiwa mahabusu kwa kutumia nguo yake.
Kingai ambaye kwa saa ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) alisema inaonekana mwanamke huyo alikuwa na madeni mengi na kwamba baada ya kuchunguza waliona kifo hicho hakikusababishwa na uzembe wa askari, kwa kuwa wakati mtuhumiwa anaingizwa mahabusu taratibu zote, ukiwemo ukaguzi, zilifuatwa.
Hata hivyo kufuatia uamuzi huo Wakili wa upande wa wafungua shauri, Peter Madeleka amesema hawajalizika na uamuzi huo wanakusudia kukata rufaa Mahakama Kuu.