Mahakama kuchunguza sababu za kifo cha aliyedaiwa kujinyonga Mahabusu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,364
8,096
1676352390303.png
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni (Kinondoni), itafanya uchunguzi huo baada ya familia ya Marehemu Stella Moses kupinga maelezo ya kituo cha Polisi Mburahati yaliyodai Stella alijinyonga baada ya kujisalimisha kituoni hapo Desemba 20, 2020.

Washtakiwa katika shauri hilo ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar (DZPC), Kamanda wa Polisi Kinondoni (RPC), Kamanda wa Polisi Mburahati (OCD), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), iliyofanya uchunguzi wa chanzo cha Kifo bila kutoa Matokeo.

Mahakama ya Kivukoni imesema Wajibu Maombi wakiwemo Jeshi la Polisi, hawakutekeleza wajibu wao Kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa Taarifa na Kuwasilisha Nyaraka za Uchunguzi Mahakamani kuonesha chanzo cha kifo hicho.

=================

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni (Kinondoni) itaanza kufanya uchunguzi wa chanzo cha kifo cha mwanamke aliyedaiwa kufia mahabusu katika kituo cha Polisi Mburahati, Stella Moses kuanzia Februari 17, mwaka huu.

Mahakama hiyo imewaita wadaawa katika shauri la maombi ya uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho ikiwataka kufika mahakamani hapo tarehe hiyo kwa ajili ya kuanza uchunguzi huo.

Wakili wa familia ya marehemu Stella, Peter Madeleka alilieleza Mwananchi kuwa mahakama hiyo ilitoa hati ya wito huo Februari 8, mwaka huu.

Mahakama imetoa wito huo zaidi ya mwezi mmoja na nusu tangu ilipotoa uamuzi wa kukubali kufanya uchunguzi wa mwili wa marehemu.

Uamuzi wa kufanya uchunguzi ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga Desemba 19, 2022 kutokana na shauri la maombi namba 3 la mwaka 2022 lililofunguliwa na shemeji wa marehemu, Emmanuel Kagongo, kwa niaba ya familia ya marehemu.

Stella alifariki dunia usiku wa kuamkia Desemba 20 2020 akiwa mahabusu ya kituo cha Polisi Mburahati alikojisalimisha baada ya kupata taarifa kuwa alihitajika kituoni hapo.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni ilieleza Stella alijinyonga, lakini familia haikukubaliana na maelezo hayo badala yake ikaomba ufanyike uchunguzi huru kujua chanzo cha kifo chake, bila mafanikio.

Miaka miwili baada ya mwili kuzikwa, familia ikaenda mahakamani kufungua maombi hayo ya uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho.

Wadaiwa katika shauri hilo ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspector General of Police - IGP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam (DZPC) na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni (RPC).

Wengine ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mburahati (OCD), mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), iliyofanya uchunguzi wa kitabibu wa chanzo cha kifo cha marehemu, lakini haikuwahi kutoa taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Akizungumzia utaratibu wa uchunguzi huo, wakili Madeleka alisema pamoja na mambo mengine mahakama itatembelea maeneo yanayohusiana na tukio la kifo hicho na kuwauliza wahusika maswali mbalimbali.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni makaburini kwenye kaburi alikozikwa marehemu na mahabusu alikodaiwa kujinyonga.

Kituoni hapo, wakili Madeleka alisema mahakama itataka kujua kutoka kwa askari waliokuwa zamu wakishughulika na mapokezi na hifadhi ya mahabusu ni kwa namna gani walitimiza wajibu wao na kuona mazingira yanayoweza kumfanya mahabusu ajinyonge.

Pia Madeleka alisema mahakama itakwenda Muhimbili ambako mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa kitabibu wa chanzo cha kifo hicho, kuona ni namna gani waliendesha uchunguzi wao.

Awali wakati akitoa uamuzi wa kukubali maombi ya kufanya uchunguzi huo, Hakimu Kiswaga alisema kutokana na hoja za mwombaji na viapo kinzani vya wajibu maombi watatu hakuna ubishi kuwa Stella alifariki dunia katika mazingira tata akiwa katika kituo Cha Polisi Mburahati.

Alisema kwa kuwa wajibu maombi hususan Polisi hawakutekeleza wajibu wao wa kisheria yaani kutoa taarifa na hakuna taarifa zozote za uchunguzi uliofanyika kuonyesha chanzo cha kifo hicho, zilizowasilishwa mahakamani, basi mahakama hiyo ina jukumu la kuamuru ufanyike uchunguzi huo.

“Hivyo mahakama hii inaamuru ufanyike uchunguzi wa kifo cha Stella Moses ambaye mahakama inaona kwamba alifariki unnatural death (kifo kisicho cha asili) akiwa chini ya Jeshi la Polisi Mburahati, Desemba 20, 2020,”alisema Hakimu Kiswaga.

MWANANCHI
 
Majibu ya postmortem yakiwa na utata. Daktari mwenye ethics hawezi kuyatoa. Maana anaingia kwny mgogoro na Dolla
 
Mtu aende akajinyonge Polisi baada ya kujisalimisha mwenyewe hicho kitu hakipo wala hakihitaji uchunguzi huyo angejinyonga huko nyumbani kwake, wahuni wamemuua hao nilisikitika sana niliposoma hiyo taarifa Tanzania watu ni makatili sana ila wamejivisha ngozi ya Kondoo hawana tofauti na Wazulu.
 
Majibu ya postmortem yakiwa na utata
Daktari mwenye ethics hawezi kuyatoa
Maana anaingia kwny mgogoro na Dolla

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Umeongea kinyume chake mkuu.

Mimi nadhani ingesomeka hivi, Daktari mwenye ethics ndiyo angeyatoa kama yalivyo no matter what. Ethics of any profession must be adhered to, no matter what, even at the expense of the state.
 
Huu utoto umezidi sasa. Ukiingia mahabusu unasachiwa na unaacha kila kitu kaunta; mkanda, viatu, pesa, funguo, cheni n.k. Vitu vyote ambavyo vinaweza kumfanya mtu ajinyonge (kwa mfano mkanda) vinahifadhiwa na polisi na mtuhumiwa anapewa PPR (hii ni karatasi yenye orodha ya vitu vilivyoachwa kaunta na mtuhumiwa).

Hapa kuna mawili, either uzembe wa askari kwa kutomkagua vizuri hivyo akaingia na kitu kilichomsaidia ajinyonge, au polisi wanahusika kumuua.

Uchunguzi wa kina ufanyike na haki ionekane imetendeka.
 
Itakuwa walimuua aisee
Naomba kuboresha wazo lako

1 :- Walimtesa katika kupata maelezo kutokana na mateso na kipigo akafariki wakaamua kutengeneza sinema ya kujinyonga.

2. Huenda walimtaka kingono (polisi na ngono ni samaki na maji) katika kubisha wakambaka na kumuua kuondoa ushahidi (visa hivi ni vingi)

Hitimisho: kazi ya upolisi ni kazi ya LAANA kama kuna uwezekano epusha kabisha uzao wako kuingia katika hii kazi.
 
Mtu aende akajinyonge Polisi baada ya kujisalimisha mwenyewe hicho kitu hakipo wala hakihitaji uchunguzi huyo angejinyonga huko nyumbani kwake, wahuni wamemuua hao nilisikitika sana niliposoma hiyo taarifa Tanzania watu ni makatili sana ila wamejivisha ngozi ya Kondoo hawana tofauti na Wazulu.
Halafu kamanda Muliro anasema tuombe lifti kwenye magari yao, yàan ujipeleke mwenyewe kwenye mdomo wa mamba.

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Huu utoto umezidi sasa. Ukiingia mahabusu unasachiwa na unaacha kila kitu kaunta; mkanda, viatu, pesa, funguo, cheni n.k. Vitu vyote ambavyo vinaweza kumfanya mtu ajinyonge (kwa mfano mkanda) vinahifadhiwa na polisi na mtuhumiwa anapewa PPR (hii ni karatasi yenye orodha ya vitu vilivyoachwa kaunta na mtuhumiwa).

Hapa kuna mawili, either uzembe wa askari kwa kutomkagua vizuri hivyo akaingia na kitu kilichomsaidia ajinyonge, au polisi wanahusika kumuua.

Uchunguzi wa kina ufanyike na haki ionekane imetendeka.
Hapo unamanisha mtuhumiwa aliingia na ngazi na askari hakuona hakukua na mahabusu wezake alikua pekeake ausiyo
 
Majibu ya postmortem yakiwa na utata. Daktari mwenye ethics hawezi kuyatoa. Maana anaingia kwny mgogoro na Dolla

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kama mauaji yalitokana na visa binafsi; yaani muuaji na aliyeuliwa, hapo dolla ina interest gani! Unafikiri kila dhuluma inayofanyika ina interest ya dolla? Kwani huyo anayekukamata hawezi kutumia mwanya huo kwa masilahi yake binafsi?
 
Back
Top Bottom