Mahakama: Mwanamke aliyefia Mahabusu ya Mahabusu alijinyonga

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mahakama ya Korona Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Septemba 22, 2023 imetoa uamuzi wa uchunguzi ilioufanya kuhusu mazingira ya kifo cha Stella Moses aliyefia mahabusu katika kituo cha Polisi Mburahati Desemba 20, 2020, ikisema kifo chake kilisababishwa na yeye mwenyewe kujinyonga.

Mahakama hiyo imesema kujinyonga huko kulifanyika licha ya mwili wake kukutwa na majeraha kichwani na shingoni.

Stella alifariki dunia usiku wa Desemba 20, 2020, akiwa mahabusu kituoni hapo alikojisalimisha baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa anahitajika, tukio ambao lilizua mvutano mkubwa baina ya Polisi na ndugu wa marehemu kwa kile wanachodai kuwa ni mazingira tata ya kifo hicho.

Katika tukio hilo lililoripotiwa kwa kina na Mwananchi katika toleo la Desemba 23, 2020, Jeshi la Polisi lilidai kuwa mwanamke huyo alifariki dunia baada ya kujinyonga akiwa mahabusu.

Ndugu wa marehemu walipinga taarifa hizo wakidai kuwa kulikuwa na utata wa mazingira ya kifo hicho, badala yake walitaka ufanyike uchunguzi huru ili kujua chanzo halisi cha kifo cha ndugu yao.

Baadaye familia ililazimika kufanya mazishi bila hata kupewa matokeo ya uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho uliofanywa na Hospitali ya Muhimbili.

Miaka miwili baadaye ndugu wa marehemu walifungua shauri la maombi dhidi ya viongozi wa Jeshi la Polisi na uongozi wa Hospitali ya Muhimbili kwa kutokutimiza wajibu wao.

MWANANCHI

Soma zaidi Mahakama kuchunguza sababu za kifo cha aliyedaiwa kujinyonga Mahabusu
 
Back
Top Bottom