Mahakama ya Kimataifa ya ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa Rais Vladmir Putin wa Urusi

Do u think and believe that writing in a foreign language will make ur point more meaningful? We andika tu kiswahili utaeleweka mzee. Kutumia lugha ya kigeni ni kuwabagua au kuwaweka pembeni baadhi ya wenzetu humu jukwaani ili wasiweze kuchangia.
Hatujasema ni kiwango gani cha Elimu kinatakiwa ili Hoja iwe na mashiko. Mbona hata PhD holders wanaweza kuongea utumbo?
Usinishambulie,Mimi hiyo nimeinukuu kutoka kwenye source!
Labda ungesema niitafsiri!
Sasa kwanini wewe umeanza Kwa lugha hiyo hiyo unayoilalamikia?
Kikubwa rejea lazima ifanyike!
 
Apo n kuchezea sharubu za simba mkuu Apa unaongelea mbabe wa dunia Putin Nani huyo mwenye ubavu huo wa kumkamata
Tuvute subira kidogo kitaeleweka. Usijekushangaa game linaisha kilaini Putin akiwa amehifadhiwa kwenye sefu mahali fulani.
 
Ni shida aisee kwani wamemwondolea kinga. Maana yake kwa sasa Putin hana Immunity tena. Yani CD4 zimeshuka chini kabisa ya kiwango.Ugonjwa wowote, hijack, assassination na watu wake watamwepuka au kumsaliti bila kikwazo, personaly kisaikolojia atakuwa na wasiwasi mkubwa zaidi juu ya uhai wake - Atakosa muda wa kufikiria vita. Anaweza kupatwa na kiharusi, shinikizo la damu, moyo au kukimbilia mafichoni kwa usalama zaidi n.k.
Hayo unawaza wewe kwa mtu jasusi mkubwa kama putin anajua walipokimbilia kujifichia kupunguza haibu wala hawezi kua na presha hiyo ni hadaa tu kwa dunia ili waonekane wana sauti
 
Majaji wa mahakama ya kimataifa (ICC),imetoa hati ya kukamatwa popote atakapopatikana rais wa urusi Vladimir Putin.

=====

Katika ya uamuzi wake, ICC imemtuhumu Rais wa Russia kuhusika na uhalifu wa kivita kutokana na kufanya uvamizi na kutwaa ardhi Nchini Ukraine ingawa Moscow imesema hatua hiyo haina maana yoyote.

View attachment 2555625

Pia, Hati ya Mahakama ya ICC imeeleza kuwa Rais Vladimir Putin aliagiza mashambulizi yaliyosababisha Watoto kuhamishwa kinyume cha Sheria pamoja na uhamisho usio halali wa Raia kutoka eneo la Ukraine na kuingia Nchini Urusi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova amema "Maamuzi ya ICC hayana maana kwasababu Urusi haiko kwenye Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, hivyo haiwajibiki chini yake."
Mwanzoni watu walikuwa wanalalamika hii mahakama ni kwa ajili ya marais wa Afrika. Baada ya rais wa Urusi kutakiwa kukamatwa, watu wameanza kukimbilia vichaka vipya.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Safi sana je hiyo biblia ilikuelezea nini kuhusu vita ya muisrael na mfilist kipindi Israel wanaingia ndani ya nchi yao ya ahadi 🤠🤠🤠
labda unisaidie nini0tofauti kt ya nchi ya ahadi na nchi ya asili.? Yakobo alipompiga mungu, huyu mungu alimuambia kuanzia leo taifa lako litaitwa israel. Kabla ya hapo hilo taifa lilikuwa linaitwaje?
 
Urusi amekamatwa pabaya hapo anawalinzj wengi zaid ya mwanzo wenzie ulaya hawana hata stress wanamuangalia akijigamba huku wakiendelea kumfinya kidogo kidogo west acha wale jamaa sio mchezo wao wamemuwekea vikwazo yeye hajaweka kuonesha bado anawahitaji aiseee Mwisho wa Urusi
 
Urusi amekamatwa pabaya hapo anawalinzj wengi zaid ya mwanzo wenzie ulaya hawana hata stress wanamuangalia akijigamba huku wakiendelea kumfinya kidogo kidogo west acha wale jamaa sio mchezo wao wamemuwekea vikwazo yeye hajaweka kuonesha bado anawahitaji aiseee Mwisho wa Urusi
Wafinye Nuclear kama wanauwezo. Hii kitu mwisho wake ni WW3 amini kwamba.
 
Majaji wa mahakama ya kimataifa (ICC),imetoa hati ya kukamatwa popote atakapopatikana rais wa urusi Vladimir Putin.

=====

Katika uamuzi wake, ICC imemtuhumu Rais wa Russia kuhusika na uhalifu wa kivita kutokana na kufanya uvamizi na kutwaa ardhi Nchini Ukraine ingawa Moscow imesema hatua hiyo haina maana yoyote.

View attachment 2555625

Pia, Hati ya Mahakama ya ICC imeeleza kuwa Rais Vladimir Putin aliagiza mashambulizi yaliyosababisha Watoto kuhamishwa kinyume cha Sheria pamoja na uhamisho usio halali wa Raia kutoka eneo la Ukraine na kuingia Nchini Urusi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova amesema "Maamuzi ya ICC hayana maana kwasababu Urusi haiko kwenye Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, hivyo haiwajibiki chini yake."
Swala ni nani atakayemkamata,maana nasikia jamaa ni Komando...
 
US wakati huu amepanda mtumbwi wa vimbwengo,Yeye na wenzake wachague 1 kati ya kusitisha kupeleka usaidizi wa kijeshi Ukraine kisha diplomasia itumike kumaliza vita au waendelee kutoa usaidizi na ku_risk chumi zao.
 
labda unisaidie nini0tofauti kt ya nchi ya ahadi na nchi ya asili.? Yakobo alipompiga mungu, huyu mungu alimuambia kuanzia leo taifa lako litaitwa israel. Kabla ya hapo hilo taifa lilikuwa linaitwaje?
Ok nitajaribu kukufafanulia licha ya kuwa unaweza tafuta bibli ukasoma maana zipo hadi play store....

 Hapo awali kulikuwa na mcha Mungu Ibrahim (abraham) siyo taifa, alikuwa na mke wake Sarah aliyefikisha hadi miaka 70 bila mtoto ila mwenyezi akamjalia akapata mtoto Isaka (Isaac), naye akampata watoto Yakobo (Israel) na Essau ndipo Israel ikazaliwa baada ya mchuano unaoufahamu wewe...
 
Vita part two wanawapa mwanya magenerali wa kirusi kupindua Russia kwa kumkamata kuwa wasipate shida wakimpindua kuwa wampeleke wapi ni the Hague

Hadi hilo tamko kutolewa ina maana assessment ya vita inaonyesha mwelekeo mzuri wa Putin kuchokwa ndani ya Russia kwenye inner circle za chama tawala na jeshi
46sm37507vk81.jpg
 
Back
Top Bottom