Mahakama ya Kadhi "Ruksa" - Pinda

Mahakama ya Kadhi "Ruksa" - Pinda

Status
Not open for further replies.
Sina tatazo na mahakama ya kadhi kuanzishwa Tanzania tatizo ikiwa gharama za uendeshaji zitabebwa na waIslam wenyewe.Sina tatizo ikiwa tatizo la mirathi na ndoa litahusu watu wa dini mbili tofauti ie Islam na Christian halitasikilizwa katika mahakama ya kadhi.

WaIslam ni raia wa Tanzania wana haki ya kuabudu kwa kufuata misingi ya dini yao bila kubughudhiwa.

Mbona gharama za shule na hospitali za makanisa zinalipiwa na kodi za Waislaam pia?.
 
Sioni tatizo kama wewe au Waislamu wakiamua kufanya hivyo wao kama wao. Binafsi yangu hilo ni swala lenu kama Waislamu. Sifikiri kama kuna mtu amekataa msifanye hivyo. Mimi nakataa kufanya hayo uliyoyasema kwa kutumia kodi za watanzania. Mimi ni mpagani, iweje nitoe kodi yangu kuendesha dini yako ambayo sina haja nayo. Natoa kodi ili nipewe huduma nzuri za matibabu na siyo kuendeshea imani za watu wengine.
Wewe huoni tatizo lakini Katiba inasema tuna sheria mbili hivyo sii swala la jinsi gani unajisikia wewe.. Ni sawa na mimi niseme sikubaliani na maamuzi ya secular law kwa nini tusifuate sheria law au waisokuwa waislaam tu ndio wafuate sheria hiyo - Hatutafika popote katiba inaruhusu na ndio argument ya waislaam..
Maadam ktk kifungu cha sheria kinachosimamia ndoa na mirathi kinaruhusu sheria za kiasili na secular zitumike basi waislaam wanayo haki ya sheria hizo kutumiwa kama wanavyosajili ndoa zao kisheria na zikatambuliwa. Nchi hii inaongozwa na Katiba na katiba imeruhusu mahakama kutumia sheria za kiislaam na kiasili pale inapohitajika (maswala ya ndoa na mirathi). Sasa kwa nini hili liwe swala la Waislaam kwa sababu ati tu wakatoliki hawana?.. Je hii sii ndio maana waislaam wanadai nchi yetu inaongozwa na mfumo kristu yaani only what is accepted in Christianity ndio mpango mzima!..

Kuna mkuu wa majeshi mmoja ana wake sijui 20 na watoto zaidi ya 100, huyu sheria ya seculra itaweza vipi kuamua maswala yake na urithi,au talaka?.. Je unafikiri ni busara ikitokea ugonvi baina ya watoto na wake zao serikali itatumia sheria gani kufanya maamuzi ambayo ki secular hakuna lakini yapo ktk asili ya huyu Mkurya.. Tumewauliza vizuri tu hiyo secular inasema nini kama mke kaomba talaka na kuachika ktk ndoa ya kiislaam lakini kaacha kuna mke mwingine na watoto ktk ndoa. Sheria yenu inasema vipi? hamkunijibu hadi leo lakini bado mnataka waislaam wachukue jukumu hilo wenyewe. Wakigombana na kutishiana kifo serikali itawaachia pia waislaam kwa sababu sio swala lao?..
 
Nimekuelewa vizuri isipokuwa wewe mwenyewe ndio hujajielewa. Kama unataka kuzijua faida kwa nini wewe unaona mke kanisani faida zake ni zipi?.. Kwa nini usiende kuoa ktk ofisi ya Halamashauri ikiwa wewe unataka sheria za secular?.

Vivyo hivyo Muislaam ana haki kama yako anaoa mke muislaam kwa kuamini sheria zake ktk haki ya ndoa na ndipo sheria za talaka na mirathji zinapomhusu, wewe usiye na sheria hizi ndio unaenda mahakama au unamwacha mkeo bila talaka na kuvuta kimada mwingine ukitumia dini kutohallaisha ndoa ya pili ati huruhusiwi kutoa talaka, hivyo unamtumia tu huyo binti ambaye ukifa anaondoka hana kitu, mirathi inakuwa tatizo ambalo haki za mke na watoto zinaamuriwa na serikali.

Waislaam wameyaona haya wazazi wengi wakiacha mali kwa kumrithisha mtu mwingine kabisa wakiwaacha watoto na mke hawana kitu, ndipo walipoona uhalali wa watoto kuwa warithi halisi wa mali hizo na sio kuandika will ambayo inawaondoa watoto na mke. Lazima watu hawa wawe ktk mirathi no matter what!
Wewe unaijua nchi yetu, ufisadi hadi vyumbani na hakuna mahala watu wanauana kama kwenye urithi na pengine ndio vifo vingi vya crimes zetu hutokana na mali. Kama ipo sheria ya mgao mara zote utakuta inasaidia kuondoa crimes maana kila mtu anajua fungu lake.

Ndio maana nimesema ninatumia instincts zangu! Not necessarily niende kanisani, nimejitambua zaidi ya nilivyokuwa huko nyuma. Sheria ya ndoa ya 1971 mbona inakidhi matakwa sana pamoja na kuwa na mapungufu kama sheria ya kiislamu ilivyona mapungufu au sheria yoyote duniani. Ina maana huwa kakuna rufaa katika mahakama za kiislamu, kama ni hivyo basi kuna kasoro kubwa. Nimesoma rufaa nyingi CA zikitoka mahakama za kiislamu baada ya kutoridhika.
 
Sidhani kama serikali imewahi kukataa mahakama ya kazi, kinachogomba ni kodi ya nani itakayotumika kughalimia mahakama hizo? Hii ya breweries au kodi ya nani?

Hiyo mbona ipo siku nyingi sana na ndiyo kesi ya madaktari iko huko.
 
Regional Commissioner?

Nilidhani najibizana na academician kumbe you are illiterate. It is acknowledged internationally RC to stand for Roman Catholic in matters related to religion. You are less informed and most likely not knowledgeable!!!!
 
Sasa "Roman" na Uafrika wapi na wapi? au wewe ni Mroma?
 
Sasa "Roman" na Uafrika wapi na wapi? au wewe ni Mroma?

Kiarabu na uislamu wapi na wapi? Wewe ni mwarabu wa Muskat! Ni mambo tuliletewa na waliotutawala/waliotukamata utumwa ndio maana nasema sometimes natumia my instincts katika kujibu matakwa ya dini yangu sometimes.
 
Hivi unawapongeza uliowapongeza kwa faida zipi kuwa na mahakama ya kadhi? What benefit interms of economy, social, political etc will you gain by having kadhi courts re-established. Usiwa na jaziba we nijibu ni faida zipi utazipata? Labda na mimi naweza kubadili dini nizifukuzie hizo faida!!
Kama sio Muislam sio rahisi kujua faida zake, kwa vile you will view the whole issue negatively. Lakini itoshe kwako kuwa kesi nyingi za Ndoa na Mirathi za Waislamu hazitakuwa katika Mahakama hizi za kawaida hivyo itapinguza workload kwa Mahakimu wachache waliopo ambao anyway wako overloaded. Wajane wengi wa Kiislamu wanadhulumiwa na ndugu za waume zao waliofariki, wanatelekezwa na mayatima, kwa sababu tu Mahakimu wengi hawako compatible na sheria za ndoa na mirathi za Kiislamu ingawa zinatambuliwa rasmi na sheria za nchi, hivyo wajane hao wanachelewa sana kupata haki zao (eg nina Shemeji yangu alifiwa na Mume sasa ni 12yrs anafuatilia mahakamani na hajapata haki, huenda mpaka atakufa na asiipate) Mahakama ya Kadhi inarahisisha sana upatikanaji wa haki hizo, na masuala ya ndoa ni kadhalika. Mkoloni hakuwa mpumbavu kuientertain Mahakama hii, hata nchi zenye Waislam Wachache kama Kenya wameiestablish siku nyingi, sijui kwanini Tanzania waliiondoa, sijui ni kwa interests za nani hasa, kama ni gharama, Waislam katika nchi hii ni significant portion ya Tax paying population, tax ambayo Billions zinaenda kufinance miradi ya Makanisa ambayo huduma zake ni very expensive kwa mlipa kodi mdogo wa kawaida (eg Shule na Hospitali za Mission) Walipa kodi wa Kiislam wanavumilia, ni vyema basi Wakristo nao wakavumilia wananchi wenzao wa Kiislam wakirekebishiwa masuala yao, tutaenda vizuri as a Unified Nation, la sivyo, kama kuna agenda ya siri, au Kama dini moja itajiona ni superior na inastahili mgao wa keki ya taifa na nyingine haistahili.... basi..!! Bila haki hapawezi kuwa na amani.
 
rais wa tano said:
(1) Ijumaa, waislamu wanatakiwa msikitini, lakini na kazini pia (2) Jumamosi, wakristo (wasabato) wanatakiwa waende kanisani na KUPUMZIKA (3)Jumapili, wakristo wengine wote wanatakiwa waende kanisani na KUPUMZIKA. Hapo hatuoni kama kodi za watanzania wote, bila kujali imani ya mtu zinalipia mambo ambayo ni ya wakristo? Hivi ni kwa nini hatuangalii ni kwa kiasi gani uchumi wa nchi unaathirika kwa kutofanya kazi siku 2 katika wiki? Nani anagharimia au kufidia mapato yanayokosekana katika siku hizo 2, kama si mwananchi kupitia VAT na kodi zingine
Cha kusikitisha zaidi ni kuwa hawa Wasabato ambao ni wachache sana ukilinganisha na Waislamu nao wamepewa siku yao ya kupumzika (Jumamosi) kwa heshima tu ya Ukristo wao, upande wa pili Muislamu anaambiwa ni upuuzi kudai siku ya Ijumaa kuwa ni siku ya mapumziko.......tugawaneni tu hii nchi ili upuuzi huu uishe!
 
Kama sio Muislam sio rahisi kujua faida zake, kwa vile you will view the whole issue negatively. Lakini itoshe kwako kuwa kesi nyingi za Ndoa na Mirathi za Waislamu hazitakuwa katika Mahakama hizi za kawaida hivyo itapinguza workload kwa Mahakimu wachache waliopo ambao anyway wako overloaded. Wajane wengi wa Kiislamu wanadhulumiwa na ndugu za waume zao waliofariki, wanatelekezwa na mayatima, kwa sababu tu Mahakimu wengi hawako compatible na sheria za ndoa na mirathi za Kiislamu ingawa zinatambuliwa rasmi na sheria za nchi, hivyo wajane hao wanachelewa sana kupata haki zao (eg nina Shemeji yangu alifiwa na Mume sasa ni 12yrs anafuatilia mahakamani na hajapata haki, huenda mpaka atakufa na asiipate) Mahakama ya Kadhi inarahisisha sana upatikanaji wa haki hizo, na masuala ya ndoa ni kadhalika. Mkoloni hakuwa mpumbavu kuientertain Mahakama hii, hata nchi zenye Waislam Wachache kama Kenya wameiestablish siku nyingi, sijui kwanini Tanzania waliiondoa, sijui ni kwa interests za nani hasa, kama ni gharama, Waislam katika nchi hii ni significant portion ya Tax paying population, tax ambayo Billions zinaenda kufinance miradi ya Makanisa ambayo huduma zake ni very expensive kwa mlipa kodi mdogo wa kawaida (eg Shule na Hospitali za Mission) Walipa kodi wa Kiislam wanavumilia, ni vyema basi Wakristo nao wakavumilia wananchi wenzao wa Kiislam wakirekebishiwa masuala yao, tutaenda vizuri as a Unified Nation, la sivyo, kama kuna agenda ya siri, au Kama dini moja itajiona ni superior na inastahili mgao wa keki ya taifa na nyingine haistahili.... basi..!! Bila haki hapawezi kuwa na amani.

Honestly I dont have a negative outlook with Islam. Naheshimu sana dini za wengine, lakini najiuliza kuna faida gani kuwa na mahakama hizi? Nimekuelewa, seems kuna faida, lakini wanawake wengi wanasema wanaonewa na sheria hizo!!!!!. Sijawahi kumsikia mwanamke wa kiislamu akiridhia kuwa mke mwenza!!! Kuna appelas nyingi sana Court of appeal za TZ kupinga mirathi ya kiislamu kuwa haki haikutendeka etc. Anyway, kila mtu ana haki ya kuchagua dini anayoipenda bila kuathiri matakwa ya wengine. Nawatakia mafanikio mema.
 
Jana, (ingawa sikusikia jibu lote) kipande kidogo nilichokisikia kinanifanya ni sadiki kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pita Pinda alipokuwa akijibu hoja za bajeti jana jioni kaonesha kuridhia kwa Serikali kuanzishwa tena kwa Mahakama ya Kadhi baada ya kufungiwa kwa muda mrefu na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika (na baadae Tanzania) Julius Kambarage Nyerere.

Tunawapongeza Watanzania wote kwenye haya maamuzi mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Kuwarudishia Waislaam Kadhi na mahakama ya Kadhi ni katika kuwapa uhuru wao wa kuabudu uliodhulumiwa na utawala wa awamu ya kwanza.

Tunatumai mchakato wa kuzirudisha mahakama za kazi utakuwa wa kasi zaidi.

Hongera Waislaam, Hongera Kikwete, Hongera Pinda, Hongera Watanzania.

Hao watanzania unawapongeza ni kina nani? Nani kakuambia watanzania wote wameridhia mahakama ya kadhi? Usitake maoni yako yawe ya watanzania wote.
 
Kiarabu na uislamu wapi na wapi? Wewe ni mwarabu wa Muskat! Ni mambo tuliletewa na waliotutawala/waliotukamata utumwa ndio maana nasema sometimes natumia my instincts katika kujibu matakwa ya dini yangu sometimes.

Kiarabu ni lugha kubwa katika Afrika, hata Kiswahili tunachoandika hapa kina asilimia kubwa sana ya maneno ya kiarabu. Uislaam haubebi jina la taifa au kabila fulani ni 'universal", maana ya Islaam ni kujisalimisha kwa muumba wako mmoja, ambae ndio yeye kwake tunajisalimisha kwa kufuata mfumo wa maisha (dini) aliotupangia.

Dini maana yake ni mfumo wa maisha, sasa wewe Mmakonde, Mndengereko, Msukuma, Mhindi, Mchina, Mbrunei ufate mfumo wa maisha wa Warumi, tutafika?
 
Mahakama ya kadhi......!!!!!!
SERIKALI HATUNA SHIDA IKIWEPO TATIZO HATUTAKI KATU KATU KATUUUU.... SERIKALI ITUMIE FEDHA KUHUSIKA NAO AU KULIPIA MAJAJI AU NAMNA YOYOTE ILE, WAISLAM WAENDESHE WENYEWE KWA FEDHA ZAO, WATAJUA WATATOA WAPI FEDHA NA NDIO MAANA WAISLAM HAWAKUPENDA WAENDESHE WENYEWE WANATAKA SERIKALI ILIPIE FEDHA KUIENDESHA WHICH IS BILLIONS OF TSHS.... HATUKUBALI.... NIPO TAYARI KUTANGAZA KANISANI KILA J2 KUPINGA WAZI WAZI KWA WAUMINI WA KIKRISTO..... hatukubali hatubali....iwepo ok... ila serikali isitie mguu huko kwa namna yoyote....

nimesoma gazeti la nipashe linasema kuwa serikali itgharamia mafunzo yatakofanyika nje ya nchi kuhusiana
na namna ya kuendesha mahakama ya kadhi ikanishangaza sana nikajiuliza huku sio kutumia kodi za wananchi
ku establish/promote one religion wakati huo huo ikijitangaza kuwa haina dini.

Binafsi nataka kuwepo na mahakama ya kazi lakini sitaki serikali iwe na mkono wa fedha kwa sababu ya kuepuka
kuwa controlled na serikali kwa sababu ukishakubali pesa ya serikali basi umeuza uhuru wako kama ambavyo
imetokea kwa bakwata. naomba ujadili hoja iliyopo mezani ya serikali kutumia kodi za wananchi kugharamia
mafunzo ya kidini ya dini moja na siyo kumjadili mtu.
 
Kiarabu ni lugha kubwa katika Afrika, hata Kiswahili tunachoandika hapa kina asilimia kubwa sana ya maneno ya kiarabu. Uislaam haubebi jina la taifa au kabila fulani ni 'universal", maana ya Islaam ni kujisalimisha kwa muumba wako mmoja, ambae ndio yeye kwake tunajisalimisha kwa kufuata mfumo wa maisha (dini) aliotupangia.

Dini maana yake ni mfumo wa maisha, sasa wewe Mmakonde, Mndengereko, Msukuma, Mhindi, Mchina, Mbrunei ufate mfumo wa maisha wa Warumi, tutafika?

Unajichanganya ndugu yangu. Mfumo wa maisha kutoka wapi, mtwara, kagera, kigoma au uarabuni. Nambie wapi katika kabila lako kuna sheria ya kufuga ndevu, kuvaa suruali fupi, kupiga mawe mtu mpaka afe etc. Mfumo wa maisha ya kiarabu!!! siyo ya kimakonde , kisukuma, etc. Tumeletewa, waafrika hawakuwa na huyo mungu wa kirumi wala wa kiarabu, tuliabudu mibuyu, mapango etc. Wakaja wakatuvuruga wakatuletea ya kwao!!! Ndio maana sometimes kama nilivyosema natumia instincts kujibu matakwa ya dini
 
Universal. Hauna kabila wala Taifa. Huo ndio Uislaam.
 
Universal. Hauna kabila wala Taifa. Huo ndio Uislaam.

There is no universality in Islam!!! Ilitoka kwa waarabu, waafrika hatukuwa na uislamu wala ukristo. haya ni mambo ya waarabu!! warumi!!!!
 
Hakuna cha michango ya Wakristo wala nini hapo, ni pesa za MOU hizo ndizo zinazofanyakazi, mwenzako alishauriwa amshauri mbunge wake ili aibue hoja bungeni kuhusu matumizi ya pesa za MOU akakimbia hapa!

Kubali kataa,wakristo wanachangia wenyewe....na ikumbukwe serikali haitachangia wala kusaidia chochote!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom