Mimi ni Mkristo, lakini nakuunga mkono, na pia naunga mkono kuanzishwa kwa mahakama hii. Hivi tatizo liko wapi? Mbona haya ni mambo private kabisa ya imani ya mtu? Na kama ni suala la wakristo kugharimia mambo ya kiislamu, mbona hatujiulizi yafuatayo: (1) Ijumaa, waislamu wanatakiwa msikitini, lakini na kazini pia (2) Jumamosi, wakristo (wasabato) wanatakiwa waende kanisani na KUPUMZIKA (3)Jumapili, wakristo wengine wote wanatakiwa waende kanisani na KUPUMZIKA. Hapo hatuoni kama kodi za watanzania wote, bila kujali imani ya mtu zinalipia mambo ambayo ni ya wakristo? Hivi ni kwa nini hatuangalii ni kwa kiasi gani uchumi wa nchi unaathirika kwa kutofanya kazi siku 2 katika wiki? Nani anagharimia au kufidia mapato yanayokosekana katika siku hizo 2, kama si mwananchi kupitia VAT na kodi zingine, hasa katika nchi kama hii ambapo wawekezaji wasio weusi wameachwa wafanye biashara zao bila kulipa kodi inavyostahili? No, tukae chini tukubaliane kupingana bila kupigana, lakini pia hatimaye tuwe fair. Mahakama ya Kadhi ianzishwe, na iwezeshwe kufanya kazi zake. Nchi hii ni yetu sote!!