Kuelekea 2025 Mizengo Pinda anaweza kumsaidia vyema Sana Rais Samia Umakamu Mwenyekiti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
23,549
17,373
1722276994411.png

Mizengo Pinda

Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya Mheshimiwa Abdulahman Kinana kuomba kujiuzulu Umakamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na Hatimaye kukubaliwa ombi lake na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa nimechekecha kwa haraka haraka sana mtu ambaye anaweza kufaa kumsaidia Rais wetu mpendwa katika nafasi hiyo ya Umakamu Mwenyekiti.

Ambapo kwa haraka haraka lakini kwa Umakini wa hali ya juu,nikaona kuwa Mheshimiwa Waziri mkuu mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda,Mtoto wa Mkulima anaweza kuvaa viatu vya Umakamu Mwenyekiti na vikamuenea vizuri sana na kumudu nafasi hiyo.

Sababu ni kuwa Mheshimiwa Pinda ni mtu Mwenye uzoefu mkubwa sana ndani ya chama pamoja na serikali,anakijuwa vyema sana chama na serikali pamoja na miiko na misingi yake.anajuwa kwa undani majukumu na nafasi ya chama na mipaka yake pamoja na msitari ambapo serikali inaanzia.

Mheshimiwa Pinda ni mtu muadilifu asiye na doa la ufisadi wala taswira mbaya kwa chama na jamii, mchapa kazi mtulivu,Mwenye hekima, staha,busara,subira, uvumilivu na Mwenye kudhibiti ulimi na kifua chake. Siyo mtu mwenye hasira wala jazba wala mihemuko.na hivyo kwa aina ya uongozi wa Rais Samia huyu ni mtu sahihi kabisa na wanaweza kuendana vyema sana wakati huu. Lakini pia siyo mtu mjivuni wala hana makundi na hajawahi kuwa na makundi wala kumtengeneza mtu kutaka urais.kwake Taifa kwanza mtu baadaye.hivyo Mh Pinda Anaweza kudhibiti hata nidhamu na kuwalea watu wote kwa usawa bila upendeleo wala kumbeba mtu kwa maslahi yake binafsi .

Mheshimiwa Pinda kihistoria siyo mtu mwenye uroho wala uchu wa madaraka.Ni mcha Mungu na Mwenye hofu ya Mungu kama ilivyo kwa Rais wetu mpendwa Daktari Mama Samia. Pia katika kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu Mheshimiwa Pinda anafaa sana katika kuleta ,kujenga na kuendeleza mshikamano na umoja wa chama. Lakini pia Mheshimiwa Pinda amepita katika mawimbi ya kila aina na kufikia hapo alipo ameshakomaa na kujionea mengi na kujuwa namna ya kuvuka.hivyo atakuwa nguzo pia kukivusha chama kwa kushirikiana na Mwenyekiti wetu katika dhoruba za kila aina.

Mheshimiwa Pinda pia anaheshimika vizuri sana ndani ya chama na kwa wanachama wote.na hivyo kukipa nguvu chama tokea ndani.kwa sababu ni muhimu sana kuwa na makamu mwenyekiti mwenye kusikilizwa na wanachama pamoja na wananchi awapo katika majukwaa ya kisiasa.

Ngoja niishie hapa nakuja kuendelea, lakini kikubwa na Rai yangu kwa Mama yangu Daktari Samia Suluhu Hasssan ni kuteua Mwana CCM mwaminifu kwake,Mtii,msikivu,asiye na makundi,Mwenye misimamo na maono ya kukipa nguvu chama,anayemwamini na kuamini katika falsafa zake za 4R,ambaye hajawahi kuwa na kundi la wasaka Urais. Mtu huyo naamini kuwa ni huyu mzalendo wa kweli na dhati Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda anamfaa vyema mama yetu na chama chetu kwa ujumla wake.

Mama yangu Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan chagua mtu unayemuamini na Utakayekuwa na uhuru na moyo mkunjufu kufanya naye kazi.chagua mtu ambaye mtaweza kuzungumza lugha moja,kupanga mipango mikakati ya pamoja kwa maslahi ya chama chetu. mama yangu chagua mtu ambaye yupo tayari kufa kwa ajili yako na kukutetea ipasavyo hata gizani au ndotoni.

Mama yangu Daktari Samia chagua mtu ambaye hata akiwa wapi atasimama na wewe na kukutetea. ,chagua mtu mama yangu ambaye hawezi kukusaliti wala kukuumiza wala kukufanya ujute kuwa naye karibu.Mama yangu chagua mtu ambaye utataka umpigie simu umuombe ushauri hata kwa mambo mazito bila wasiwasi wala hofu ya kuvuja kwa taarifa.

Mama yangu nimependekeza huyu kwa kuwa huyu ni mtu mnyenyekevu,mpole , hana makuu wala kiburi wala dharau. Siyo mtu atakayefanya kazi kushindana na wewe bali atafanya kazi kushirikiana na wewe. Huyu atafanya kazi ili wewe uonekane bora na siyo kufanya kazi ili kuonekana yeye bora. Huyu naamini anaweza kukubebea kila aina ya Mzigo. Mama yangu,huyu Mzee ameiva kiitikadi na kukomaa kiakili. Huyu ni mtu na nusu. Naamini Atafanya na kutekeleza kwa unyenyekevu mkubwa kwa kila utakacho muagiza . Huyu hata utakapokosea kwa bahati mbaya kibinadamu , basi atataka yeye ndiye abebe lawama na siyo wewe Mama.

Mama nina mengi ya kukwambia ila ngoja niishie hapa kwanza nakuja kuendelea.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Back
Top Bottom