Mimi nina maswali kadhaa ya jinsi gani hizi mahakama za kadhi. Siulizi kwa ubaya lakini ni katika kujuzana tu:
1. Je kama sharia ita kuwa ina contradict sheria mama ya Jamhuri ipi ina take precedent? Kwa mfano sharia iseme kosa "X" lina stahili adhabu "Y" lakini sheria ya Jamhuri ina sema ina stahili adhabu "Z" hapa katiba ipi itaangaliwa? Kama sheria za Jamhuri zita take precedent haitafanya mahakama ya kadhi zisiwe na nguvu? Maana hata katiba ina sheria za ndoa, mirathi nk.
Hizo ni hoja za msingi ambazo ni vema zikajadiliwa kwa utulivu na mantiki bila kuchukua mwelekeo wa ushabiki na kubezana ambako kunaweza kubadilisha sura nzima ya hoja iliyopo.
Sheria za Kiislamu ni moja miongoni mwa vyanzo vya sheria nchini Tanzania, mwaka 1964, Bunge la Tanganyika kwa wakati huo lilipitisha Sharia ya Kiislamu (Sheria ndogo) iliyompa madaraka Waziri aliyehusika na mambo ya Sheria kuandaa na kuchapisha kipengele cha Sharia ya Kiislamu baada ya kushauriana na wanachuoni wa Sharia za Madh-hebu za Kiislamu. Na hatimae Katibu Mkuu wa Bunge wakati huo, alikamilisha kuandika Mswada wa ndoa wenye sehemu 4 (kwa msaada wa masheikh wa madh-hebu za Kiislamu).
Mswada huu uliotolewa kama Sharia ndogo chini ya kifungu kidogo cha Sharia ya Kiislamu (Na: 56 ya mwaka 1964) ikiwa ni sehemu ndogo ya Gazeti la Serikali na Na: 34 la tarehe 27, Juni, 1967.
Ilifahamika kuwa sehemu zilizosalia, kuhusiana na kuwalea watoto na talaka n.k. zingechapishwa mapema. Lakini zoezi hili lilisitishwa na badala yake serikali ilitunga sheria ya Ndoa kupitia Mswada wa Ndoa wa mwaka 1971.
Hata hivyo, kwa mujibu wa kumbukumbu zangu, kanuni ya Sheria ya Kiislamu 1964 bado haijafutwa na bado ni sehemu ya Kitabu cha Bunge.
Hoja ya msingi hapa ni kuwa sheria hizo zilikuwepo, pamoja na kutokuwepo kwa Mahakama ya Kadhi, aidha sheria husika katika mswada jadiliwa zinahusiana tu na yale mambo ya Ndoa, Talaka, Mirathi, na malezi ya watoto kwa Waislamu na hazigusi kabisa uhuru wa raia wengine katika kuabudu dini zao.
2. Kuna wanaosema katiba mpya ita shughulikia mambo ya mirathi, ndoa nk. Je kwa mfano mimi "John" nimuoe "Amina" je sheria ipi ta chukua mkondo? Au hata tuki badilisha kibao na kusema "Abdalah" kamuoa "Jane". Je likitokea swala la mirathi au migogoro ya ndoa mahakama ipi ita husika? Hapa ni under the assumption Muislamu na Mkristo wameoana bila hata mmoja kubadilisha dini. Na je hii haita fanya ndoa kati ya Mkristo na Muislamu zionekane kuwa mwisho wake ni matatizo tu na kuincourage watu kuto kuoa nje ya dini zao?
3. Je hizi sheria za mahakama ya kadhi zita apply kwa kila Muislamu hata ambae hazi taki na hazi kubali? Mfano ni kwamba mimi ni Muislamu nime fanya kosa ndiyo lakini sitaki kuhukumia chini ya mahakama za kadhi bali mahakama za kawaida je ita kuaje hapa? Je haoa Muislamu ata lazimishwa kuhukumia chini ya sheria za kadhi? Kama aki lazimishwa hili halita wakwaza Waislamu ambao hawa amini katika hukumu za sharia? Na kwa upande mwingine isipo kuwa lazima si itaondoa maana nzima ya hizi mahakama?
4. Je zikianzishwa hizi mahakama zita fuata sharia law down to the book ama zita chaguliwa vipengele hadi vipengele? Haoa tujumbuke kwamba maswala ya makosa na hukumu gani iendane na kosa ni la kijamii pia. Ji kama sharia law inasema kitu fulani lakini kwa asilimia kubwa watu (Waislamu) hawata amini hiyo ni hukumu stahiki ita kuaje?
5. Je mtu akiamua kubadilisha dini kwa kuogopa hukumu za sharia itakuaje? Kwa mfano "Omari" kashtakia mahakama ya kadhi akaona kwamba hukumu itakua nzito na akaamua kubadilisha dini kukwepa hukumu ita kuaje?
Nina maswali mengi zaidi ila kwa post hii nadhani ina tosha. Maswali yote haya ni katika kuelimishana tu na natumai yata jibiwa na wataalamu wa hizi mahakama au sharia law.
Kwenye sheria ya ndoa ya Tanzania, kuna ndoa za aina tatu zinazo tambuliwa na serikali.
A: Ndoa ya serikali, ambao inafungwa Bomani.
B: Ndoa za Kidini, Ambazo ni za Kiislam na Kikristo
C: Ndoa za Kimila.
Wanaotaka kuingia kwenye ndoa ni hiyari yao kuchaguwa kati ya mafungu hayo matatu. Ikitokea kuwa ni watu wa Imani na dini tofauti, wengi wao uelekea kwenye ndoa ya kiserikali, yaani wanafunga ndoa yao Bomani na kukiwa na tatizo litatatuliwa uko uko bomani.
Kama ni ndoa ya Kiislam hapo sasa ndipo Kadhi atakapo husushwa, na kama wana ndoa hawataki kutambua mahamuzi ya kadhi, hiyo pia ni hiyari yao wanaweza kwenda kwenye mahakama za kawaida.