Kwani bila hiyo mahakama hayo masuala yanashughulikiwa vipi?[Originally posted by SAFARI NI SAFARI]
Kwa kawaida yangeshughulikiwa na mahakama hizi za kawaida na kwa muda mrefu yamekuwa yakishughulikiwa na mahakama hizihizi za kawaida.Kwa mfano kwa suala la miradhi ili kutambua uwepo wao serikali ilizigawanya sheria katika makundi matatu nayo ni sheria za kimila,sheria za kiislamu na sheria za kiserikali.Katika kutoa hukumu sheria za kiislamu za mirathi zimekuwa zikitumika ikibainika mhusika alikua muislamu na alikuwa anaishi maisha yake kwa kuzingatia sheria za kiislamu.Mimi sijui hawa jamaa wanatafuta nini?nafikiri lengo lao nchi hii iwe ya kiislamu!
Kenya ina mahakama ya Kadhi, je ni ya kiislam?