Mahakama ya kadhi hii hapa!

Mahakama ya kadhi hii hapa!

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, walisema wahenga.
Lakini angakia mtanzania mwenzangu usije kuitwa MTO PUMBA kwa hiyo tabia yako kutetea waislam.
Eeh! Mkuu thanks kwa kutujuza, kumbe ndivyo ilivyo ivyo.
 
X-Paster umesimama kwenye misingi ya kidini nimekufurahia, si Kama Muadhama Sheikh Simba yuko kisiasa zaidi. Nimekubaliana na mchango wako.

Nonda, asante nimejifunza kitu pia kwenye mchango wako.

Lakini tubadili kwanza katiba yetu kukidhi haja ya kuwa na mahakama ya kadhi. Pia Mahakama kuu iwe na uwezo wa kupindua maauzi ya mahakama ya Kadhi
Huyo Muadhama Sheikh Simba, ndio nani!? Nakwazika hapa kidogo!
 
Mufti mkuu wa waislamu muadhama sheikh simba ametangaza kuwa mahakama ya kadhi kwa ajili ya waislamu itaanza kazi zake hivi karibuni baada ya serikali kukubali kuirudisha tena mahakama hiyo iliyokuweko enzi za nyuma na pia kuiomba serikali kufanya siku kama ya jana tarehe 7 kuwa siku ya mapumziko kwa kuwa ni mwaka mpya wa waislamu!
Source: Gazeti la mwananchi 08.12.10

kama serikali imekubali mahakama hiyo basi naipongeza kwa uamuzi huo wa busara wa kuwapa waislamu kile wanachotaka kwa mujibu wa sheria na kusisitiza hoja ya mufti kufanywa siku ya mapumziko kwa kuingia mwaka mpya wa kiislamu kwa sababu hata dini zingine huwa wanamapumziko siku za mwaka mpya wa tarehe 1.1 kila mwaka hivyo waislamu nao wana haki ya kusherehekea mwaka wao mpya na ifanywe kuwa ni siku ya holliday!!

kwa kweli inaonyesha kwamba watu wengi hawajui wanachokisema! wakristo wana amri na mfumo wao wa kimahakama unaojulikana kama "canons laws " na hapa kuna takribani sheria kama 4300 ambazo zinahusu mirathi,talaka, ndoa, na mahusihano kati ya mtu na mtu na kati ya Mungu na mtu. waislamu pia wana mfumo wao wa kimahakama unatunga sheria za aina mbili yaani "IBADAT NA MUAMALAT" sasa kwa nchi za kidini kama saudia Arabia sheria za kidini ndio zainatwala nchi hiyo yaani mfumo wa kiislamu kwa madhehebu ya suni na sio suni tu bali "wahabiyya" na pia kama Vatican ni nchi ambayo wakazi wake wanafuata canons laws!
kwa Tanzania katiba iliamua sheria zisiwe za kidini na masuala ya dini yasiingie katika mifumo ya nchi bali suala la dini liwe la mtu binafsi!
sasa leo waislamu wakikubaliwa mahakama ya kadhi na sheria Zao katika mfumo wa nchi kesho wakristo wakiomba nao mfumo wao kisheria utambuliwe na serekali hapo hatuna nchi tena!
nchi yetu ni ya "kisekula" yaani isiyofuata sheria ya dini yoyote bali katiba huru na kama tunataka tuuingize Tanzania katika muundo wa kidini amani iliyopo itatoweka kabisa!
kama waislamu wanataka kadhi fine but ifanyike katika misikiti yao na kama wakristo wanataka canons laws sawa lakini ifanyike katika makanisa yao LAKINI TANZANIA ISIINGILIWE NA DINI YOYOTE!
LEO serikali ikiwakubalia waislamu mahakama ya kadhi kesho haitaweza kuwazuia wakristo kuwa na mahakama za "canons" na pia haitawazuia wahindu kuwa na mahakama za kihundu na isiwazuie wapagani na waabudu mashetani kuwa na mahakama zao!
wanaoshabikia mambo ya dini kuingizwa katika serikali "hawajui hasa madhara ya kitu wanachodai"
 
Tumekupata sasa nani atagharamia hii mahakkma na Serikali kwa nini ihusishwe si Waislamu waanzishe tu chini ya BAKWATA kama kitengo?Ukiihusisha serikali ndio taabu zinaanza

Mkuu,

Sina uhakika kama umenipata kweli, Hilo la gharama mimi sijalizungumzia. Ukipitia #55 ya thread hii utaona nimeandika hivi:

"Ama kama ni lazima, serikali iridhie na iruhusu hii mahakama iwepo au wenyewe tu waislamu waianzishe, hapo nafikiri ndio penye mjadala".

Huko kwenye mambo ya gharama watajuana wenyewe, watu wa serikali na waislamu. Mimi si mshabiki katika hili nimechangia kile nilichokipata katika kujitaarifisha, kujisomea, kutafuta habari,na kujifunza.

Hata hivyo najuwa kuna vikundi au vyama hupata ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.
 
Huyo Muadhama Sheikh Simba, ndio nani!? Nakwazika hapa kidogo!

Soma post ya Kwanza ya Mtani wangu Kadogoo

Mufti mkuu wa waislamu muadhama sheikh simba ametangaza kuwa mahakama ya kadhi kwa ajili ya waislamu itaanza kazi zake hivi karibuni baada ya serikali kukubali kuirudisha tena mahakama hiyo iliyokuweko enzi za nyuma na pia kuiomba serikali kufanya siku kama ya jana tarehe 7 kuwa siku ya mapumziko kwa kuwa ni mwaka mpya wa waislamu!
Source:
 
Mkuu!

Kama umenisoma tokea juu, utanielewa! Tusiweke jazba wala kutafuta machukizano ya kiimani. Mahakama ya Kadhi haipo kwenye katiba kwa Mtazamo na uelewa wangu. Basi tutumie fursa hii kurekebisha yale matatizo kwenye katiba mama. Iangalie hii hoja vizuri. Kenya wanahiyo mahakama ya kadhi lakini ni kama haina nguvu zaidi kwa waislam tena kwenye mambo ya ndoa na talaka na mirahi tu. Pia makahama kuu Kenya inaweza batilisha maamuzi ya mahakama hii ya kidini. Sawa ndugu?

lazima kuwa na tahadhari.

kadiri tunavyolainika kukubaliana na matakwa yao, kwao ni ushindi katika vita vyao vitakatifu aka jihad.

sisi tutaona tunajenga mahusiano, lakini wao watakuwa wakitung'ong'a misikitini na kwenye vijiwe vya halua
 
Unataka kutuambia maulidi si katika Uislamu. Hembu nikuulize vizuri maana naona unataka kuzungumza uongo sasa
Unataka nikujibu kitu gani...!? Rejea kusoma tena maelezo yangu, utanielewa.
 
lazima kuwa na tahadhari.

kadiri tunavyolainika kukubaliana na matakwa yao, kwao ni ushindi katika vita vyao vitakatifu aka jihad.

sisi tutaona tunajenga mahusiano, lakini wao watakuwa wakitung'ong'a misikitini na kwenye vijiwe vya halua
Huwe na taadhari wewe kama nani katika nchi hii!?
 
lazima kuwa na tahadhari.

kadiri tunavyolainika kukubaliana na matakwa yao, kwao ni ushindi katika vita vyao vitakatifu aka jihad.

sisi tutaona tunajenga mahusiano, lakini wao watakuwa wakitung'ong'a misikitini na kwenye vijiwe vya halua

Nimekuelewa! Ila Duu
 
Mwaka juzi ATCL ililazimika kuwapeleka hijja bure sasa imekufa....na zile ni kodi zetu sote

We acha kuzungumza vitu sio kweli hakuna mahujaji wanaopelekwa bure bule kilichotokea mwaka juzi ni watu waliokwama kwenda hijja walishindwa kusafiri baada ya kutokea kutokuelewa baina ya ATCL na waandaaji wa hiyo safari. Hakuna mtu anayepelewa bure hapa. Shule za kikatoliki na makanisa mengine on the other side yalikuwa yakila kuku kwa mrija hilo halina ubishi. Kama una evidence kuwa waislamu wanapelekwa bure tunaomba lakini sio hili unasema uongo.
 
Kindly Mr Mdondojai, provide an empirical evidence to substantiate your allegation.
 
We acha kuzungumza vitu sio kweli hakuna mahujaji wanaopelekwa bure bule kilichotokea mwaka juzi ni watu waliokwama kwenda hijja walishindwa kusafiri baada ya kutokea kutokuelewa baina ya ATCL na waandaaji wa hiyo safari. Hakuna mtu anayepelewa bure hapa. Shule za kikatoliki na makanisa mengine on the other side yalikuwa yakila kuku kwa mrija hilo halina ubishi. Kama una evidence kuwa waislamu wanapelekwa bure tunaomba lakini sio hili unasema uongo.

mwaka huu serikali ilikosa hela za kuwasafirisha wakaamriwa watangaze wametapeliwa.

hahaha!!
 
jiulize kwanza wewe ni nani kabla ya kuniuliza mimi.

kama unadhani mimi ni kuku basi na wewe ni kuku vilevile
Mbona unajishtukia mkuu, hakuna aliye kwita kuku wala bata, ila juwa kuwa nchi hii si ya Wakristo peke yao... Sawa!?
 
Yote maisha tu. After all mahakama inawahusu waumini ambao kwa hali ya Kibongo, ni wazi kuwa wengi sana watakuwa na mkono mmoja maana kwa kupenda kwao ********** watahukumiwa sana. Tujiandae kupata walemavu wengi zaidi.:embarrassed:
hapa ndiyo sipati picha, kuna watu watabadili dini
 
Mimi ni christian naomba wakristo tuwe na moyo wa uvumilivu kama waislamu.kwa nini nawaita ni wavumilivu,sababu hizi hapa.
Wakristo 1.jumapili ni mapumziko
2.mwaka mpya
3.ijumaa kuu
4.jumatatu ya pasaka
5.chrismas
6.boxing day

waislam 1.ijumaa siku ya kazi.
2.idd zipo 3 kama sijakosea ni mapumziko.
3.mwaka mpya,kimyakimya.
Kama kweli tunataka amani ya kweli tuwape waislamu haki yao.tz hizi dini zipo karibu sawa sasa kama kuna mmoja ataonewa kwa namna yoyote ile nakwambia amani tutaipoteza.naomba wakristo wenzangu msinishambulie kwani hiyo ndiyo njia ya kweli kwani hata biblia inasema hata mtumwa wako tu unatakiwa kumpa haki yake.
Hii nchi hakuna mwenye mamlaka ya kumtawala mwenzake na kama mmoja wetu atajidanganya kulifumbia macho hili ataona matokeo yake.
Waislamu wapewe mahakama ya kadhi na mapumziko siku ya mwaka mpya wa kiislamu na tuwaombe radhi kwa kutuvumilia
hapo ndipo tutakuwa na amani ya kweli na sikukuu zote tutasherehekea kwa pamoja na amani.
Nawasilisha.

wewe siyo mkristo
 
Back
Top Bottom