Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo F. Mbowe kaonyesha kushangazwa na jinsi Chama Cha Mapinduzi kinavyohaha kama vile ndio wapinzani na Ukawa ni chama dola... Hali kama hiyo ya chama dola (CCM) kuhaha haijawahi kutokea kipindi cha nyuma kama safari hii. Hii ni dalili ya kushindwa mapema sana!
Vile vile mwenyekiti huyo kashangaa baadhi ya watu wanataka mdahalo wakati mgombea wa CCM hajui hata Rais wa Libya ni nani.... Ikumbukwe wiki iliyopita Magufuli akiwa Tanga alisema Rais wa Libya aliyepinduliwa alikuwa ni Saddam Hussein baadaye akasema hapana sio Saddam... Saddam alikuwa wa Kuwait.... Huyo ndio mgombea ambaye chama chake kinataka mdahalo..
Na mwisho Mbowe kaonyesha hali ya kumshangaa Magufuli kutumia logo ya M4C na kusema huko sasa ndiko kuchanganyikiwa zaidi na kuishiwa kwa chama hicho na mgombea wake.....