Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 37,725
- 24,624
Ndugu zangu Watanzania,
Dunia nzima inaendelea kufuatilia kwa ukaribu sana na kwa umakini wa hali ya juu sana juu ya Ziara ya Mheshimiwa Rais Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Nchini Urussi.
Ambapo vyombo mbalimbali vya Habari Duniani kote vimeonekana kupigana vikumbo kupata taarifa za kila dakika za Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania.
Ikumbukwe ya kuwa RAIS Samia ni kiongozi Mwenye ushawishi zaidi Duniani na ambaye amekuwa anafuatiliwa sana mitandaoni na kila sehemu. kutokana na uchapakazi wake na nguvu ya ushawishi aliyonayo kwa sasa .
Sasa kuna kitu cha kuvutia kimetokea katika ziara hiyo ya Mheshimiwa Rais.Ambapo ni kuonekana kwa Mlinzi maarufu Wa Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli na aliyejizolea umaarufu Mkubwa Duniani kote . kutokana na umakini ,umahiri na uhodari wake katika Suala zima la Ulinzi na Usalama Wa Rais.
Ambapo Mlinzi huyo ameonekana akiwa Mwenye Tabasamu ,furaha na bashasha pale alipokuwa akisalimiana ana kwa ana na Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu wetu Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Ni tukio Ambalo limevutia na kuteka hisia za watu wengi sana Duniani kote . ni tukio ambalo limewakosha watu wengi sana hasa kutokana na ukweli kuwa Mlinzi huyo amekuwa akipendwa , kukubalika na kufuatiliwa na watu wengi sana Duniani kote.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.