Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

Khaa jiwe naona anawaaminisha watz kua bila ye Tz isingekua hapa .

Km ambavyo ameshawaaminisha wana CCM kua ye ndio bora.
 
Tilioni 1.5 yetu kwanza ipo wapi? haya ma miradi kwetu sio ishu ishu ni ustawi wa wananchi maendeleo ya vitu hata Nyerere aliwahi kuya challenge
 
Hahaha...hata Mungu anapingwa, sembuse binadamu. hapa ni mwendo uleule wa kupokezana vijiti kila miaka 5-10
 
"Nchi yetu ni tajiri, Watanzania tunaweza, Jengo hili limegharimu Mabilioni ya fedha zaidi ya bilioni 700, fedha hizi zimetolewa na Watanzania kwa asilimia 100, ambapo asilimia 15 fedha taslimu na 85% tumekopa , na mkopo huu utarejeshwa kupitia kodi zetu" - JPM #UzinduziTerminal3

This dude is a chronic bipolar!
 
Kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu na kuhutaji viongozi kujitoa kwa moyo katika kufanikisha hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.
Maana yake hana mpango wa kuondoka.
 
Sweet talker tu hakuna lolote, vilaza tu ndo watashika anayoyasema bila kujiuliza.
Wanayomfanyia mwandishi wa habari yule sasa hivi tu ni evidence tosha huyu jamaa maneno mengi ila ana tabia za kimadulo. Ovyo sana
 
Bora deni likue tu lakini tunaona miradi kama hiyo, kwani hakuna nchi isiyodaiwa waulize USA wana deni kiasi gani kwa wachina.

Waulize ethiopia wana miradi kuliko yenu, lakini raia maelfu kwa maelfu, wanaondoka kama mizigo
 
Kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu na kuhutaji viongozi kujitoa kwa moyo katika kufanikisha hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.
Kama nchi ni tajiri inakuwaje uwazulumu wastaafu pension zao?
 
Duu imenikumbusha tajiri mzee mwenye mashamba alipofariki mtoto alijifanya mjanja akachukua hati za mashamba akakopa pesa akajenga magorofa kuanzia kijijini kwao mpaka mjini akanunua mabasi 30 kwa mkupuo akanunua Hotel 4 akanunua ndege ya kukagua mashamba na helkopta Nenda leo kamtazame utasikitika AMEONDOKA BABA WA TAIFA sasa watoto Wamefika na mitindo tofauti ya kuongoza MALI Jee zitapona ?
 
Back
Top Bottom