Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu na kuhutaji viongozi kujitoa kwa moyo katika kufanikisha hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.

Kama CCM kiliweza Kumteua Yeye kuwa ' Flag Bearer ' wake na sasa anafanya hayo mambo makubwa na mazuri basi ni CCM hiyo hiyo tena itampata ' Flag Bearer ' mwingine na huenda akawa ni Mchapakazi, Mtu mzuri na Kipenzi cha Watanzania wengi kama siyo wote kuliko hata Yeye, hivyo nae ataweza Kuifanya Tanzania yetu hii mambo makubwa na ya Kimaendeleo. Alianza Hayati Mwalimu, akaja Mzee Mwinyi, akafuata Mzee Mkapa, halafu Mzee Kikwete na sasa Yeye na atakuja mwingine tena. CCM haikaukiwi Watu wazuri na haina rekodi ya Kukosea katika Kuteuwa Wagombea wake.
 
Bora deni likue tu lakini tunaona miradi kama hiyo, kwani hakuna nchi isiyodaiwa waulize USA wana deni kiasi gani kwa wachina.
Hivi nyie mabinti wa Siku hizi mnatatizo gani
Haya turuhusu Ushoga kwa kuwa Marekani pia Wameruhusu Ushoga kwa raia wao

We unafurahia Deni kuongezeka kwa kuanzisha Miradi isiyo na manufaa yoyote kwa raia wa kawaida

Haya kale Mataaluma ya Reli
 
Miradi mingi inayotekelezwa Sasa ilikuwa planned miaka mingi iliyopita. Kwa hiyo anayofanya sasa Kuna watu waliyaanzisha lakini hawakuweza kuyakamilisha kwa sababu muda wao uliisha wakaondoka madarakani, Hivyo Basi yeye siyo special sana kiasi kwamba watanzania walio baki hawana uwezo wa kuongoza isipokuwa yeye tu. Kwenye hili hata tunaomuunga mkono tutamkataa.
 
kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu na kuhutaji viongozi kujitoa kwa moyo katika kufanikisha hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.
Mtoto acha kupiga mayowe, acha watu waone wenyewe😁 ameajiri watu wa kumsifia sasa ameona haitoshi ameamua aingie ulingoni mwenye we
 
Back
Top Bottom