Magufuli: DPP aliichezea kesi ya ''samaki wa Magufuli''

Magufuli: DPP aliichezea kesi ya ''samaki wa Magufuli''

DPP ni kama Jaji, sio rahisi kumtumbua, pia ukifikia hatua ya kumtumbua mtu kama Feleshi basi jitafakari mala mbilimbili.

Uliza mwanasheria yeyote wa serikali atakueleza boss wao huyo wa zamani ni mtu wa aina gani, Feleshi ni mwadilifu na mchapa kazi hasa, licha ya kuwa boss lakini kila siku ukitoa jpili lazima saa kumi na moja alfajiri yumo ofisini na anaondoka saa mbili usiku, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, hakuna mtu angethubutu kumpa rushwa Feleshi maana hata huo ujasiri sijui unaupata wapi.

Hii ni kama tu ile issue ya UDA watu walimsema sana humu eti alihongwa ndo maana akaiondoa kesi mahakamani baada ya watu kuelezwa nini kilitokea ndo wakaona kumbe si mtu wa kuwa compromised na ndo wakagundua Hossea alikuwa mtu wa aina gani.
Kuna tofauti kati ya Jaji na DPP kamanda na hata security of tenure yao ni tofauti
 
Duhh, hii kali ya mwaka. Matusi yamezidi mpaka watu mnaogopa kupost!
Sasa watu hawataki facts bali kile wanachokiamini, hauwezi kushindana nao sababu kuna kundi limeibukia hapa juzi tu wanachokijua ni kutukana na ubishi unreasonably
 
Kumbe hata Rais Magufuli alishailalamikia ofisi ya DPP.

Kumbe tulishindwa kesi kwa sababu ya DDP alitaka serikali ishindwe kesi.

Kuna watu naona Mkuu ana uchungu nao maana hawakuonyesha kumuheshimu huko nyuma. Tatizo hakuna aliyetegemea kuwa ndiye yule anayekuja!!
 
Rais akiongea na viongozi wa juu wa jeshi la polisi ameeleza jinsi serikali ilivyoshindwa kesi ya samaki. Eti makosa yalikuwa 19, cha ajabu DPP alipeleka moja tuu. Magufuli akalalamika kwa mwanasheria mkuu, wakapeleka tena mengine matatu na jamaa wakashinda kiulaini.

Kituko kingine, eti kuna mke wa waziri kamtukana traffic polisi wakati kitekeleza majukum yake, rais ameagiza hyo askari apandishwe cheo na pia ameshaongea na hyo waziri kumuonya.

Rais ameongea kwa uchungu mambo kibao yanayoumiza yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya askari wachache na kusababisha hasara kubwa kwa taifa.

Chanzo: Kipindi cha Makala ya Rais, TBC.
Hiyo TBC ndiyo kitu gani?
 
Wewe unaamini hilo? Jaji Mkuu anaweza vipi kuongeza mashtaka yaliyoondolewa na DPP mfano? na kwa nini hayakurejeshwa yote kama DPP hakuwa na hoja? lakini tukumbuke kesi ni ushahidi, na pia DPP ni taasisi.

Hapa kaka Eliezer umesingiziwa big time. (Political Stunt)
Sijawahi kuona Charge Sheet inarekebishwa wakati wowote ule tena na Jaji Mkuu.(Lord Help Us)

Victoire are you this gullible?
Judiciary na DPP wanaingiliana kivipi jamani?
 
Nadhani humfahamu vizuri Jaji Dkt Feleshi wewe, kama kunamwanasheria muadilifu hata mmoja alobakia hapa Tanzania basi ni Feleshi, niliwahi kusema hapa natamani sana Feleshi angefanya kazi na Magufuli akiwa kama DPP nchi ingenyooka hii, kama unajua Ikulu ilikuwa inamuingilia then unatoa wapi ujasiri wa kumtuhumu Feleshi?

Ahsante sana.
Dkt Mbuki waliamua kumchafua tu, kipindi kile.
Na baada ya Werema nikategemea anaweza kuwa Attorney General sema ofisi yao imejaa figisu balaa.
Kipindi hiki nakategemea tena, wala hata hakuchaguliwa basi nkasikitika tu.
The guy ni muadilifu saaaana.
 
Mkuu umewahi kuwa na Kesi mahakamani au nawee unasikia habari kwa watu.....kwa taarifa yako Kwenye Mahakama zetu Mwenye HELA ndio anaamua matokeo ya KESI msibaki kuimba nadharia humu

Wewe jamaa unajua unayeongea naye ndiye Dkt Mbuki Feleshi mwenyewe?
Sasa unataka kumfundisha nini Dkt wa sheria?
 
Hahahahaaa Magu acha kuzuga na mambo ya kesi, kama hasara umeshatupa na hatuta lisahau hili na nyumba zetu ulizogawa ovyo ovyo na Mv dar, tutapambana tuondoe kinga ya rais kushtakiwa kwenye katiba mpya,!! Nakushaur pambana mfumuko wa bei, watanzania wamechoka na comedy za majipu
Tatizo la Magufuli ni mnafiki sana asiyekubali makosa....yeye mwenyewe ana madhambi yake.
 
Ahsante sana.
Dkt Mbuki waliamua kumchafua tu, kipindi kile.
Na baada ya Werema nikategemea anaweza kuwa Attorney General sema ofisi yao imejaa figisu balaa.
Kipindi hiki nakategemea tena, wala hata hakuchaguliwa basi nkasikitika tu.
The guy ni muadilifu saaaana.
Huwa naumia sana watu wanapomsema vibaya Dkt Feleshi, I wish wangemjua, jamaa ni mwadilifu na mchapa kazi hasa, ni jaji wa kanda ya Dar lakini mwezi jana tu nilisikia akifunga watu Morogoro na jana taarifa ya habari ITV usiku kahukumu Iringa, niliwahi kusema humu pia nilitegemea ndiye angekuwa AG, baada ya kuachwa nikategemea wanamuandaa kuwa CJ lakini nimekuja shangazwa sana na kauli hizi za Mhe Rais dhidi yake.
 
Mh. Mwl na Dr. Rais, huyu mtu yupo na anahudumu kwenye serikali yako. Tena ni jaji sasa. Ushahidi unao, muundie tume ya kijaji achunguzwe na kushtakiwa ukimjumlisha na yule hakimu na wanasheria wa arvs feki waliotoa utetesi dhaifu na kuiingiza nchi kwebye gharama ya 60bilion huku wanalipwa mishahara ya umma. Anzia hapo mahakamani huku kwingine ni rahisi kuthibiti. Usiogope hawa wanasheria wasio wazalendo na wanaokosa utu na ubinadamu.
 
Bado kidogo mtajua haikuwa mamlaka ya nchi hii wala ya mh. Magufuli kuuza nyumba. Mtakapojua mtashangaa. Fanyeni utafiti!!!
 
Kumbe hata Rais Magufuli alishailalamikia ofisi ya DPP.

Kumbe tulishindwa kesi kwa sababu ya DDP alitaka serikali ishindwe kesi.
Acha kuwafanya watanzania wote wajinga! Kwani kabla ya kukamata hizo fish hakumjua DPP wa nchi yake. je, hiyo ilikuwa kesi yake ya kwanza kushindwa? Mbona ile ishu ya kugushi nyaraka ya umeya dar haisemei! au atailalamikia akishamaliza awamu yake. Hisia zinawafanya watanzania kujiona kama wameamka kumbe bado wako kwenye usingizi mzito!
 
Acha kuwafanya watanzania wote wajinga! Kwani kabla ya kukamata hizo fish hakumjua DPP wa nchi yake. je, hiyo ilikuwa kesi yake ya kwanza kushindwa? Mbona ile ishu ya kugushi nyaraka ya umeya dar haisemei! au atailalamikia akishamaliza awamu yake. Hisia zinawafanya watanzania kujiona kama wameamka kumbe bado wako kwenye usingizi mzito!

Mbona wewe ni mjinga tayari!!?
 
Back
Top Bottom