Rais akiongea na viongozi wa juu wa jeshi la polisi ameeleza jinsi serikali ilivyoshindwa kesi ya samaki. Eti makosa yalikuwa 19, cha ajabu DPP alipeleka moja tuu. Magufuli akalalamika kwa mwanasheria mkuu, wakapeleka tena mengine matatu na jamaa wakashinda kiulaini.
Kituko kingine, eti kuna mke wa waziri kamtukana traffic polisi wakati kitekeleza majukum yake, rais ameagiza hyo askari apandishwe cheo na pia ameshaongea na hyo waziri kumuonya.
Rais ameongea kwa uchungu mambo kibao yanayoumiza yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya askari wachache na kusababisha hasara kubwa kwa taifa.
Chanzo: Kipindi cha Makala ya Rais, TBC.