Dr.
Eliezer Feleshi ndiye alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma
(DPP) aliyetuhumiwa na Rais
John Pombe Magufuli mwaka
2016 kwa kuichezea kesi inayojulikana kama kesi ya ''samaki wa Magufuli'' na kuifanya serikali ishindwe mahakamani.
Rais aliyasema hayo
mwaka 2016 wakati alipokuwa akifungua kikao cha kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa Mikoa.
Rais Magufuli alisema DPP (
Eliezer Feleshi) aliondoa makosa 19 ambayo yangewafunga watuhumiwa na kubakiza kosa moja lakini baadaye yeye, Waziri Magufuli, akaamua kwenda kulalamika kwa
Jaji Mkuu ambapo baadaye yaliongezwa na kuwa makosa matatu.
Rais amesema huo mchezo ulikuwa unachezwa kwenye ofisi ya DPP ili serikali ishindwe Mahakamani kwa sababu ambazo anazifahamu DPP,
Eliezer Feleshi. Cha kushangaza DPP Eliezer Feleshi akateuliwa na Rais Kikwete mwaka 2014 kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Pamoja na hayo
Dr. Eliezer Feleshi hivi sasa ameteuliwa na huyo huyo
Rais John Pombe Magufuli kuwa
Jaji Kiongozi! Uteuzi huu kwa kweli umewaacha wananchi wengi wakijiuliza kulikoni!
cc:
[B]JokaKuu[/B].