Rais akiongea na viongozi wa juu wa jeshi la polisi ameeleza jinsi serikali ilivyoshindwa kesi ya samaki. Eti makosa yalikuwa 19, cha ajabu DPP alipeleka moja tuu. Magufuli akalalamika kwa mwanasheria mkuu, wakapeleka tena mengine matatu na jamaa wakashinda kiulaini.
Kituko kingine, eti kuna mke wa waziri kamtukana traffic polisi wakati kitekeleza majukum yake, rais ameagiza hyo askari apandishwe cheo na pia ameshaongea na hyo waziri kumuonya.
Rais ameongea kwa uchungu mambo kibao yanayoumiza yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya askari wachache na kusababisha hasara kubwa kwa taifa.
Chanzo: Kipindi cha Makala ya Rais, TBC.
Kituko kingine, eti kuna mke wa waziri kamtukana traffic polisi wakati kitekeleza majukum yake, rais ameagiza hyo askari apandishwe cheo na pia ameshaongea na hyo waziri kumuonya.
Rais ameongea kwa uchungu mambo kibao yanayoumiza yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya askari wachache na kusababisha hasara kubwa kwa taifa.
Chanzo: Kipindi cha Makala ya Rais, TBC.
Rais Magufuli amemtuhumu DPP kwa kuichezea kesi inayojulikana kama kesi ya ''samaki wa Magufuli'' ili serikali ishindwe mahakamani.
Kesi hiyo ilipewa jina hilo kwa sababu washitakiwa 36 kutoka mataifa tofauti, waliokuwa wakikabiliwa na kesi hiyo walikamatwa wakati John Magufuli akiwa Waziri katika Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na alishiriki kwa karibu katika tukio hilo.
Rais ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao cha kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa Mikoa.
Rais Magufuli amesema DPP aliondoa makosa 19 ambayo yangewafunga watuhumiwa na kubakiza kosa moja lakini baadaye akaamua kwenda kulalamika kwa Jaji Mkuu ambapo baadaye yaliongezwa na kuwa makosa matatu.
Rais amesema huo mchezo ulikuwa unachezwa kwenye ofisi ya DPP ili serikali ishindwe Mahakamani kwa sababu ambazo anazifahamu DPP.
Wakati wa sakata la ''samaki wa Magufuli'', Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) alikuwa ni Eliezer Feleshi ambaye August 2014 aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kwa sasa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ni Biswalo Mganga ambaye aliteuliwa October 2014.
Rais alisema kuna kesi za mafisadi toka mwaka 2009 hazijapelekwa mahakamani lakini kesi za wezi wa kuku hazichukui muda mrefu kupelekwa mahakamani.
Rais amewambia DPP, Biswalo Mganga kujipanga vizuri ili atende haki kwa wananchi wote kwa sababu ofisi yake huondoa kesi au makosa yanayoonekana kuwafunga mafisadi.
''Ni lazima niseme ukweli ili mfahamu mwelekeo wa serikali ya sasa'' alisema.
Kesi ya samaki wa Magufuli ilisharipotiwa hapa;
Na Hapa;
VIDEO YA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI:
Kama una Megabyte ndogo angalia kuanzia dakika ya 14:20
NOTA BENE:
Kumbe tulikuwa tunatoa lawama kwa Magufuli kuhusu serikali kushindwa hii kesi ya ''samaki wa Magufuli'' bila kufahamu hali halisi ilivyokuwa katika kutayalisha mashitaka.
Tumemkaanga sana Magufuli kwenye hili suala kumbe tatizo lilikuwa kwenye ofisi ya DPP.
Ama kweli, jambo usilolijua ni kama usiku wa giza!