Magufuli: DPP aliichezea kesi ya ''samaki wa Magufuli''

Magufuli: DPP aliichezea kesi ya ''samaki wa Magufuli''

Sasa kama muda ulikwisha hawezi kuniaminisha mm great thinker kuwa eti sijui nani alifanya ashindwe kesi. Labda ni njia ya kujisafisha ili aonekane anamaamuzi mazuri ambayo hayaliingizi taifa kwenye hasara. Vipi kuhusu sukari? Nani kasababisha emefeli? Msiongozwe na ushabiki. Lazima Muwe mnatumia akili zenu


Daaah, eti Great Thinker.... Wewe ndiye Great Thinker? Aaah, basi sawa..!!!!

BACK TANGANYIKA
 
One man show is a real disaster to the nation. Why can't he opt for a harmonised constitution? Cheap popularity doesn't get us any where. Mind you

Naamini unajua maana ya utashi wa kisiasa (political will) ili sheria na taratibu tulizojiwekea zofanye kazi.
 
FELESHI ALIKUWA MRA RUSHWA NO MOJA.HALAFU WALE WACHINA WALIKUWA WANAVUA KWA BARAKA ZA IKULU.MAGUFURI ALIKUWA ANAPIGANA VITA AMABAYO MKUU WAKE WA KAZI ALIKUA AKIIFADHILI.NDO MAANA KATI YA MAKOSA 19 DPP ALILAZIMISHWA YAPELEKWE AMAKOSA MAWILI ILI SERIKALI ISHINDWE NA MAGUFURI AONEKANE NI MKURUPUKAJI.KUMBUKA KIKWETWE,LOWASA NA MAMEMBE WALIKUWA HAWATAKI UTENDAJI WA MAGUFURI KWANI ALIKUWA ANAWAFUNIKA HIVYO KUANZA KUMHOFIA KATIKA SAFARI YAO YA KISIASA
Nadhani humfahamu vizuri Jaji Dkt Feleshi wewe, kama kunamwanasheria muadilifu hata mmoja alobakia hapa Tanzania basi ni Feleshi, niliwahi kusema hapa natamani sana Feleshi angefanya kazi na Magufuli akiwa kama DPP nchi ingenyooka hii, kama unajua Ikulu ilikuwa inamuingilia then unatoa wapi ujasiri wa kumtuhumu Feleshi?
 
Rais halalamiki, anasema kilichotokea wakati wa kesi ya samaki aliokamata wakati ule!
Uzuri Rais anafahamu kila palipooza. Ukifahamu tatizo ni nusu ya kutatua tatizo lenyewe
Kuna baadhi ya watu wanashindwa hata kuelewa mantiki ya Rais kutoa mfano kuhusu kesi ya ''samaki wa Magufuli.

Kuna wengine hawafahamu hata tofauti ya kutoa taarifa na kulalamika.

Kuna wengine wana ajenda ya kutafuta mapungufu ya Rais Magufuli kwa kila suala analolifanya. Kwa sasa wanakuja na suala la Rais kulalamika ili ionekane kwa wenye fikra fupi kuwa Rais ni dhaifu.
 
Mh kweli jf kuna kila watu.. Yaani kuna watu maisha yao siasa siasa unaweza kuta hata kuoga kwao siasa. Raisi anatoa ukweli wa mambo wao wanaleta siasa. Hivi sukari wasingekosea wangeagiza maana ninavyojua mtu akikosea anajirekebisha sasa juzi tu wameona warekebishe watu hao
 
Ina maana hata hili ilibidi asubiri hadi awe Rais ndio aseme kama hii kesi ilichezewa?

Ova
 
hivi unajielewa ulichoandika? unajua rais ni nani na ana mamlaka gani?
Inawezekana sijielewi!

Mimi ninafahamu Rais ni Rais na Rais wa Tanzania ana mamlaka ya Rais wa Tanzania kama yalivyoainishwa katika Sura ya Kwanza na Sura ya Pili ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 specifically kuanzia Ibara ya 33-46.

Naomba unielimishe ili nijielewe!
 
Rais Magufuli amemtuhumu DPP kwa kuichezea kesi inayojulikana kama kesi ya ''samaki wa Magufuli'' ili serikali ishindwe mahakamani.

Rais ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao cha kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa Mikoa.

Rais Magufuli amesema DPP aliondoa makosa 19 ambayo yangewafunga watuhumiwa na kubakiza kosa moja lakini baadaye akaamua kwenda kulalamika kwa Jaji Mkuu ambapo baadaye yaliongezwa na kuwa makosa matatu.

Rais amesema huo mchezo ulikuwa unachezwa kwenye ofisi ya DPP ili serikali ishindwe Mahakamani kwa sababu ambazo anazifahamu DPP.

Rais alisema kuna kesi za mafisadi toka mwaka 2009 hazijapelekwa mahakamani lakini kesi za wezi wa kuku hazichukui muda mrefu kupelekwa mahakamani.

Rais amewambia DPP kujipanga vizuri ili atende haki kwa wananchi wote kwa sababu ofisi yake huondoa kesi au makosa yanayoonekana kuwafunga mafisadi.

''Ni lazima niseme ukweli ili mfahamu mwelekeo wa serikali ya sasa'' alisema.

Kesi ya samaki wa Magufuli ilisharipotiwa hapa;

Na Hapa;


VIDEO YA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI:




Mweee ... Duuu
Nimeisikiliza hii Documentary yote, Kwa Kweli Kazi anayo Rais. Na anavyosema WaTanzania wamuombee, Kumbe ni Kweli.
 
Kwa ninavyoona watoa haki itabidi kufanya kila linalowezekana kumridhisha " Bwana mkubwa" .
 
One man show is a real disaster to the nation. Why can't he opt for a harmonised constitution? Cheap popularity doesn't get us any where. Mind you

Huo utumbo uloweka hapo ndo uliotufikisha hapa., hii ilikua inahitaji dictator na JPM atosha.. Hii sio awamu ya kuchekacheka rais anazama na majina ya wauza unga.. Hapa kazi tu jombiii
 
Huyu bwana Mungu amlinde. He is very open, he didn't hit around the bush. Just straight to the target. Hahahahaha
Na hata body language inaonyesha kabisa ana amini kile anachokiongea.
Ofisi ya DPP ni jipu. Pia kuhusu CCP vijana kwenda na vimemo, nadhani hiyo imeishakuwa desturi ya jeshi la polisi. Yaani kama huna God father siyo rahisi kupata nafasi CCP. (Almost 90% ya wanaojiunga CCP wana ma God father)
Ameongea masuala ambayo hata mwananchi wa kawaida mwenye common sense anayaona serikalini.
 
Feleshi hapa anasemwa,Feleshi jitokeze kaka ,ni kweli uliichezea ile kesi ya samaki?
Wewe unaamini hilo? Jaji Mkuu anaweza vipi kuongeza mashtaka yaliyoondolewa na DPP mfano? na kwa nini hayakurejeshwa yote kama DPP hakuwa na hoja? lakini tukumbuke kesi ni ushahidi, na pia DPP ni taasisi.
 
Sasa na yeye analalamika wananchi wafanyeje? hio si kesi ya jinai?irudishwe mahakamani!!!!!
Ninaamini umesoma tu heading na kutoa comment!

Ni wapi Rais amelalamika?

Soma thread nzima kwa uangalifu ili uelewe vizuri au angalia video niliyoweka kwa msaada zaidi.
 
Hii nikama anatutaarifu kuwa Dr Feleshi alivuta mpango wa kutosha sana kutoka kwa Wachina wale. Na kwa kesi ambayo ukiacha kufungwa tuu walikuwa wanapata hasara ya mabilioni ya shilingi. Jee Feleshi atakuwa kavuta ngapi? Na ni wazi kwa kesi kubwa kama ile mkuu aliyekuwepo alifahamu nini kinaendelea na hakujali serikali itabidi ipoteze bilioni ngapi. Jee anatufahamisha kisayansi kuwa mtangulizi wake ameshiriki uharamia huo?
Nadhani pia Feleshi alipewa ujaji kana sikosei, jee mtu wa aina hiyo anaweza kuaminika kutumikia wadhifa huo wa ujaji? Hapa maswali ni mengi sana!
Mkuu Kikwete alikuwa na madili mengi sana ya meli. Mpaka mweli za mafuta....
 
Back
Top Bottom