Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,908
- 16,466
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu ameiomba Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Mashtaka DPP na amlipe fidia kwa ucheleweshaji wa shauri lake.
Lissu amesema hayo mbele ya Majaji watatu wa rufani Shimiwa Mwarija, Muruke na Khamis ambapo amedai kuwa kesi yake imwcheleweshwa kwa makusudi kwa siku 139 huku akikaa gerezani kwa mwaka mmoja na miezi mitafu sasa.
"Kwa jinsi ambavyo nimeyazungumzia yameletwa kwa lengo moja tu kurefusha kwsi ya msingi na ukirefusha kesi ya msingi mjibu maombi ataendelea kukaa Ukonga Prison na leo ni siku ya 139 tangu hii mbinu ya kuchelewesha kesi waianzishe. Nimo gerezani leo mwaka na miezi mitatu lakini kwa sababu ya ucheleweshaji huu wa siku 139 (kuanzia Februari 24, 2026 hadi leo Julai 3, 2026)" amelalamika Lissu
Ameendelea kuieleza Mahakama ya Rufani kuwa kitendo hicho cha DPP kinaendana kinyume na matakwa ya kikatiba juu ya DPP kuhakikisha mwenendo wa mahakama hautumiki vibaya ni maslahi ya umma kuzingatiwa huku akihoji ni yapi maslahi a umma kwenye kesi hiyo. "Maombi haya yana maslahi gani ya umma." alihoji Lissu
Katika kukazia maombi yake kwa Mahakama Lissu alisema "Ombi langu sio tu mahakama hii iyakatae maombi hayo ni kutumia Mamlaka ya Mahakama Kuu kumuamuru mleta maombi alipe fidia kwangu kwa sababu ya ucheleweshaji huu kwa sababu ya taabu aliyonisabishia kwa siku 139. Mumuamuru DPP anilipe fidia kwa usumbufu wote huu." Ameongeza Lissu
Akijibu hoja za Lissu Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga amepinga madai ya Lissu kuwa maombi hayo yameletwa kwa ajili ya kuchelewesha kesi akisema kuwa si nia ya DPP.
Kuhusu malipo ya fidia kwa kuchelesha usikilizwaji wa kesi amesema kuwa kifungu alichokitumka Lissu hakitumiki katika mazingira ya shauri hilo. Amefafanua kuwa akifungu hicho kinatumika pale ambapo mahakama inakuwa imesikiliza kesi na kuamua kuwa haina msingi.
Baada ya kusikiliza pingamizi la awali pamoja na maombi haya ya msingi Mahakama ya Rufani imeahirisha shauri hili na imesema itatangaza siku ya uamuzi.