Ndugu MM, topic yako hii, inaweza kukuweka mahali pabaya hata wewe, kwa sababu inaonekana kama kumjadili mtu. Tukumbuke kuwa simple minds discuss people...
Kuhusu Pombwe Magufuri, ni mwana sayansi. Watu wengi waliosoma sayansi wana namna yao ya utendaji. Wakijua principle inasema hivi..wao huanza kutekeleza kulingana na hiyo principle inavyosema. Si waongeaji sana kama wewe MM, au kama walivyo wanasiasa per se. Hawaongei sana kama wansheria, au watu waliosoma sana historia. Hawa ni watu, katika aina za watu, wenye kundi lao, ni watendaji.
Kuhusu uuzaji wa nyumba, ilikuwa ni maamuzi ya pamoja katika baraza la mawaziri, kipindi cha serikali ya BW Mkapa. Mkapa alikuwa na utaratibu wa kufanya vikao na mawaziri wake ili waweze kuwa na uamuzi wa pamoja. Naona Kikwete hilo si muhimu sana, yeye anawatembelea huko huko wizarani kwao mmoja mmoja. Kwahiyo baada ya uamuzi huo, Magufuri alianza kutekeleza kwa kishindo principle ya baraza la mawaziri.
Kuhusu hili la bomoa bomoa, naona lina sababu tatu (1) sheria ndio inataka hivyo (2) ilani ya uchaguzi inatao ahadi ya kujenga fly overs na usafiri wa kasi (3) alipelekwa wizara hiyo kwenda kuondoa malalamiko mengi yaliyokuwepo ikiwa ni pamoja na ufisadi.
Kwasababu hizo tu rais alitakiwa kumpa special treatment, yaani kuwa naye karibu ili kuweza kumrekebisha pale anapoharibu na kumpa moyo ili afanye ile kazi aliyompa aifanye katika hiyo wizara ngumu.
Magufuri, amejijengea jina, ambalo hata asipokuwa na madaraka, wengi mtamkumbuka. Ndiyo maana leo tunamjadili yeye na siyo Dr Kawambwa. Ndio maana Lyatonga Mrema ambaye hana madaraka ya uwaziri, lakini nchi nzima tunakumbuka utendaji wake. Hata Hayati Moringe Sokoinne, pia hatasahaulika kwa uwezo wa kutekeleza na kufuatilia utekelezaji katika serikali ya awamu ya kwanza.
Mwisho, kila mtu anaweza kuwa na taswira yake kutegemea na kazi anayofanya, madaraka aliyopewa na aina ya mkuu wake wa kazi alivyo. Kama Dr JP Magufuri angekuwa anafanya kazi chini ya rais Nyerere au Dr Slaa, nadhani angeweza kuwa na manufaa makubwa sana kwa taifa hili.