dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,955
- 9,527
Kuna watu huwa mnaona future au?Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?
Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?
Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?
Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?
Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?
Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:
a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.
b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.
Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:
a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.
b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.
my two cents plus the other fifty
Duh!! Unaweza sema uchawi ila ndo hivyo kuna watu mna karama zenu aisee.Atatuongoza vibaya zaidi kuliko huyu wa sasa
Mkuu tindo
Kwanza, ahsante kwa kutenda haki ya kunisikiliza kabla ya 'hukumu'.
Pili, nasimama na bandiko langu ulilonukuu kwa mantiki yake,kwamba tunahitaji kiongozi mwenye 'discipline, vision, goals and action' kama nilivyomalizia.
Tunahitaji kiongozi anayesimamia kanuni na sheria na si anayetaka cheap popularity.
Swali, je, haya yanawahusu waliotajwa?
Tatu, kuna misemo ya watu maarufu inayoeleza kwanini bandiko langu linaweza kuwa na msimamo tofauti
Rais Lincoln wa US alisema '' If you want to test a man's character give him power ''
Kwa kiswahili kisicho rasmi, ukitaka kujua tabia ya mtu mpe madaraka
Lord Acton, British Historian alisema '' Absolute power corrupts absolutely'
Kwa kiswahi kisicho rasmi, mtu akiwa na madaraka juu ya watu au vitu, madaraka hayo humlevya''
Ni upi mrejesho wa maelezo yangu kwa sasa?
Ukisoma bandiko la asili, nimetumia neno '' Viongozi'' kwa maana ya Leaders na si Watawala (rulers)
Tunahitaji mfano wa kiongozi ni Nyerere. Pamoja na mapungufu aliyokuwa nayo kama mwanadamu, Nyerere alikuwa na sifa hizi, kuthamini Utu, kuthamini Maisha ya watu, kuheshimu haki zao na kuheshimu sheria.
Katika kipindi cha miaka kadhaa tangu bandiko la asili nimeshuhudia yale yaliyosemwa na Rais Lincoln na Lord Acton pamoja na yale aliyosimamia mwalimu Nyerere .
Hakuna usimamizi wa sheria kwa viongozi bali usimamiaji wa kisheria kwa watawala.
Mtawala haihitaji kufuata sheria anahitaji sheria zimfuate.
Kiongozi anasimamia sheria hata kama zinakwenda kinyume na matakwa yake
Kuna kubomoka kwa kwa taasisi za nchi. Mapungufu ya mihimili yetu yalikuwepo, lakini kwa kwa sasa ni kama vile mihimili imeungana. Natamani awepo mtu wa kunielimisha tofauti ya uvccm/uwt na Bunge au Mahakama!
Maendeleo ya kweli ni ya watu kuwa sehemu ya kujitawala(si kutawaliwa) ,sehemu ya kuongoza na ni huru katika kusema, kupanga na kushiriki bila vitisho au kuandamwa.
Wananchi wakiwa huru hata katika lindi la umasikini bado ni matajiri.
Mwisho, kupo kubomoka kwa misingi inayotufanya sisi tuwe Taifa.
Hatuwezi kuwa Taifa kukiwa na mbegu au hisia za kibaguzi , hofu na wasi wasi.
Kwamba, kutofautiana kimawazo ni kosa la jinai kama si uhaini.
Kwamba, uzalendo ni kuimba mapambio na si kuamini katika Utaifa unaotujenga sisi kama watu wamoja.
Kwamba, tunazidi kugawanyika katika misingi ya kikanda , kikabila, na itikadi zote za kidini na kisiasa.
Endapo hatuheshimu haki za watu kuishi kama inavyosema katiba, haki za kujieleza, kupokea na kutoa habari, kushiriki na kupanga. Kama hatuthamini maisha ya watu! maendeleo yoyote hayatakuwa na maana.
Tutahitaji kumuomba radhi mkoloni aliyetuheshimu hata pale tulipotofautiana naye kimawazo.
Hakumpiga Nyerere risasi kwa kusema arudi Ulaya. Mkoloni hakufunga watu kwa kushiriki siasa .
Kama ni hivyo, kwanini leo tunababaika kuiona tofauti ya kujitawala na ile ya kutawaliwa na mkoloni?
Nadhani maoni yangu yatakuwa yamejibu hoja yako
Ahsante
Ukweli uliojificha lakini unaonekanaa. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.
b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.
Wewe ni nabii usiyevuma. Hongera!b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.
Kaamua kuunga mkono "juhudi",sasa jaribu kumuuliza leo
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?