Magufuli bila madaraka yukoje?

Magufuli bila madaraka yukoje?

sasa kwa mfano akiwa Rais Magufuli atatuongozaje?

Ataongoza vizuri tu. Nchi yenye vyama vya siasa visivyokuwa na ideology, watu wanaongoza kama vile wanakimbiza mwizi, mkimbizaji mzuri ndio bora apewe nchi, hakuna njia mbadala hapo.
 
Nchi ilishavulundwa muda mrefu na watendaji wabovu, ili kuweka mambo sawa kwa nchi iliyovulugwa kama hii tunahitaji viongozi wenye vulugu, kwa hili Magufuli anafaa. Watu wanahitaji maamuzi magumu, maamuzi magumu yakianza kutekelezwa tena tunakuwa watu wa kwanza kulalamika. Katika lundo la vigogo wote wanaong'ang'ania kuongoza mzoga huu (Tanzania), at least Pombe ndio anafaa. Mtoa maada umeonyesha bias kwenye topic hii. Kamwe sitaweza support eti Magufuli ajiuzuru kwa kuwa tu anasimamia bomoabomoa au kwa kuwa tu kawaambia watu wapige mbizi. Au kwa kuwa tu maamuzi yake huwa nayapingana na Rais na PM, I don't see any rationality on this , Unless utwambie kuwa hao viongozi walio juu yake ni watendaji wazuri kuliko yeye, then anawavuruga. Lakini kama Magufuli anafanya kwa manufaa ya Tanzania, na akiwa kati ya watu wachache ambao walisomeshwa bure enzi za Mwalimu ili waje walipe fadhira kwa taifa kwa kulitumikia, Magufuri hana haja ya kujiudhuru unless tuaminishwe kuwa JK, PM and others are doing well for this poor nation. Wapo watu wakujizuru wengi tu huko kwenye system wachafu kuliko Magufuli. Kama sheria zilikosewa watu walipwe na nyumba zibomolewe na hayo ndio wanaita maamuzi magumu. Magufuri anahitaji blending ndogo tu ila kazi anaiweza kwa watu wapenda soga kama sisi watanzania.
Katika kipindi hiki mpaka 2015 tutayasikia mengi sana na waandishi uchwara wanaotumia kalamu kuchumia tumbo wataonekana.
Watu kama Magufuli ambao hawajatumia muda wao kisiasa kujijenga Kichama wala hawajishughurishi kuwapa visenti waandishi wa habari ili waandikwe vizuri kwenye magazeti bali kutegemea utendaji wao kujijenga kisiasa wanapata shida sana kwenye mazingira ya Tanzania ambayo yamejaa waandishi wachumia tumbo.
Sasa nimeanza kuamini ni kwa nini Mpaka alimpa ulinzi wa ziada Magufuli, kweli mazingira ya Tanzania yamejaa predetors kwa watu wa aina ya Magufuli. Tunakoenda kazi iko

Uchambuzi mzuri mkuu na sipingi hata moja.Nakubaliana nawe 100%
 
Kwa mfano kama ni kweli Magufuli alitaka Jengo la TANESCO-UBUNGO libomolewe, ilibidi afikirie kua lile jengo limejengwa kwa pesa yetu na ujenzi uliidhinishwa na Mawaziri husika walikokuwepo kabla yake Magufuli kwenye wizara hiyo. Likibomolewa leo, kesho kuna uwezekano atakuja waziri mwingine anayembadili Magufuli na akaidhinisha ujenzi tena katika sehemu hiyo - sasa utaona kua sisi ndio tunaliwa tokana na maamuzi ya kibabe toka kwa hao mawaziri wa CCM.

Magufuli angetufaa sana kama angesimamia na kuwakaba walioidhinisha ujenzi wa hilo jengo. Pia atatufaa kama atadhibiti ujenzi holela unaoendelea kukua na hapo hapo kupigania raia kupata viwanja vilivyopimwa haraka - bomoa bomoa is too easy kumpa sifa Magufuli. Vilivyofanywa kwa makosa na wenzake kabla yake, basi na waadhibiwe kwanza ili makosa yasirudiwe.

Kimsingi Magufuli si kiongozi mzuri, anafanya mambo kama kuruta - utafikiri amekatazwa kufikiri. Ni kweli tunaweweza kumlaumu magufuli kwa kutaka kubomoa jengo la TANESCO kwa kigezo cha kula hasara walipa kodi wa tanzania. Sasa tujiulize ni kifanyike ili barabara iweze kutanuliwa?

Mkuu ilo unalo dai ni sawa lakini ukumbuke magufuli sio wazimwenye dhamana na hiyo mipango miji au ujenzi holela mwenye dhamana hiyo ni wazili tibaijuka
 
Magufuli bado namfagilia kwa ushupavu wake wa kusimamia sheria kwa vitendo
. Suala la je, anapokuwa hana madaraka yukoje, to me is irrelevant. Kwani kuna mijitu ndani ya serikali ya kifisadi ya ccm imepewa madaraka yote lakini imekaa kimya na kuacha nchi inachezewa kama haina mwenyewe. Kikwete anamweka magufuli madarakani kwa kinyongo.

Anachoogopa ni kunyoshewa vidole na watanzania endapo ataamua kumwacha kwa sababu utendaji wake wa kazi hakuna mtanzania asiyeujua. Aliwahi hata kumtia ndani kiongozi mmoja wa ccm kwa kukutwa na kokolo ya kuvulia samaki kwenye bwawa la nyumba ya Mungu.

Hatutaki sweeping statements, naomba utoe mfano wa sheria gani anazisimamia?
 
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?

Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?

Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?

Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?

Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?

Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:

a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.

b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.

Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:

a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.

b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty

Mhe John magufuli amekuwa kwenye barza la Mawaziri toka awmu ya kwanza ya Benjamin Mkapa hadi sasa. Ni katika kipindi hicho hicho taifa limeshuhudia wizi na ubadhirifu mkubwa wa raslimali na fedha za taifa ukitekelezwa na viongozi wakuu wa nchi hii k.m RAD, EPA, MEREMETA, TANGOLD, kuuzwa kwa mashirika ya umma kama vile NBC, TTCL n.k kwa be za kutupwa; Seikali ambayo yeye ni mmojawapo kufanya maamuzi kuitia baraza la mawaziri kutengua maelekezo ya Mwalimu Nyerere kuwa madini ya nchi hii hayozi hivyo yasichimbwe hadi pale taifa litakapokuwa limejijengea uwezo wa kunufaika kutokana na raslimali hizo n.k

Kitendo cha Mahe John magufuli kuendelea mpaka leo kuwa mjumbe halali wa baraza la mawaziri kinathibitisha dhahiri kuwa yeye pia ni fisadi na hupiga kura za ndio kuruhusu hujuma zote ziliyotajwa hapo juu dhidi ya watanzania.

Aidha Mhe John Magufuli anayo role yake binafsi katika hujuma ya nyumba za serikali nchi nzima, kwa jinsi alivyotekeleza zoezi hilo na yeye mwenyewe, ndugu hata kufikia mawahara zake kugawiwa nyumba za serikali ni uthibitisho wa ufisadi wake.
 
Hii thread imekaa ki assumption zaid, inahoji "Kama angekua Hana madaraka" the news ni kua anayo na anayatumia ipasavyo na hicho ndo kinamatter maana amesimama katika nafasi yake
 
Mhe John magufuli amekuwa kwenye barza la Mawaziri toka awmu ya kwanza ya Benjamin Mkapa hadi sasa. Ni katika kipindi hicho hicho taifa limeshuhudia wizi na ubadhirifu mkubwa wa raslimali na fedha za taifa ukitekelezwa na viongozi wakuu wa nchi hii k.m RAD, EPA, MEREMETA, TANGOLD, kuuzwa kwa mashirika ya umma kama vile NBC, TTCL n.k kwa be za kutupwa; Seikali ambayo yeye ni mmojawapo kufanya maamuzi kuitia baraza la mawaziri kutengua maelekezo ya Mwalimu Nyerere kuwa madini ya nchi hii hayozi hivyo yasichimbwe hadi pale taifa litakapokuwa limejijengea uwezo wa kunufaika kutokana na raslimali hizo n.k

Kitendo cha Mahe John magufuli kuendelea mpaka leo kuwa mjumbe halali wa baraza la mawaziri kinathibitisha dhahiri kuwa yeye pia ni fisadi na hupiga kura za ndio kuruhusu hujuma zote ziliyotajwa hapo juu dhidi ya watanzania.

Aidha Mhe John Magufuli anayo role yake binafsi katika hujuma ya nyumba za serikali nchi nzima, kwa jinsi alivyotekeleza zoezi hilo na yeye mwenyewe, ndugu hata kufikia mawahara zake kugawiwa nyumba za serikali ni uthibitisho wa ufisadi wake.

naunga mkono kwa 110%.
kiongozi ambaye dhamira yake haina room for uzandiki hawezi kuendelea kuwa sehemu ya serikali zandiki. as simple as that.
 
Magufuli ni kiongozi mtiifu sana kwa wakubwa wake na mara nyingi huitikia kwa haraka sana na kuzitekeleza amri za hao wakubwa. Kwa maneno mengine ana nidhamu ya woga! Tatizo kubwa alilonalo ni kufanya zaidi ya alichotumwa, yaani badala ya kufanya kadha anafanya kadha wa kadha na hivyo kuwaweka wakubwa wake katika wakati mgumu wa kurekebisha pale alipopitiliza.

Ujasiri alionao Magufuli wakati wote huamini wakubwa wake wanaridhia kila anachofanya wakati sivyo. Hali hii humfanya kuwa mropokaji!
 
Mwanakijiji maada yako ni safi sana kuhusu huyu jamaa JohnPombe Magufuli.
I want to be transparent on this,Sitaki kutafuna maneno. Mimisi shabiki wala mwanachama wa CCM ila nataka niweke waz i tu kuhusu huyu PombeMagufuli.
Marehemu Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere alikuwa akisemaKUONGOZA NI KUONYESHA NJIA. Tatizo tulilo nalo kwa hii Serikali ya Kiwete nikwamba imeshindwa kuongoza kabisa na hasakwenye hii awamu yake ya lalasalama. Ni Dr.John Pombe Magufuli peke yake ndaniya CCM anayeonekana angalao kidogo kuwa anawezaKUONGOZA NA KUSIMAMIA SHERIA.
Serikali ya Kiwete chini ya CCM imejaa Mawaziri wengi ambaoni makanjanja. Hawajui wanafanya nini kwenye wizara zao. Hakuna wanachowazazaidi ya KUONGEZEWA POSHO ZA VIKAO HUKO BUNGENI.
Katika principles za Management wanasema kuwa Kiongozi aumtawala siku zote hapendi kuweka mtu chini yake halafu huyo mtu akaanzakuonekana yuko smart zaidi kiutendaji kuliko hata huyo Mkuu wake!!! Hili ndilotatizo lililopo kwa sasa kati ya Kiwete na Magufuli na kati ya Mizengo Pinda naMagufuli. Mana yake ni kwamba Magufuli anaonekanakuwa MCHAPA KAZI KULIKO RAIS NA WAZIRIMKUU. Kwa hiyo kiutendaji au kiprotokali hii haitakiwi. Kwanini wewe wa chiniuonekana ni bora kuliko wakubwa wako?
Kwa hiyo basi Magufuli anapigwa vita na Rais wake na halikadhalika na PM! Hivyo karibu kila maamuzi anayofanya Magufuli lazima yapigwevita maana anataka kuwapiku Wakubwa zake! Huu ni ujinga mkubwa sana kwaviongozi wa CCM.Wanashindwa kuona kwamba huyu Magufuli ndiyo anayepigania CCMangalao iendelee kuonekana ingawa tunajua inapumlia Oksijeni huko ICU.
 
Tuangalie kwa ufupi. Huyu bwana alipoingia bungeni ulikuwa wakati wa Msekwa ambapo bunge lilikuwa mhuri tu na haikuwa rahisi sana kujua wapiganaji kwa uwazi hasa ukiwa ndani ya chama. Halafu akawa waziri jambo lililombana zaidi.

Kurudi kwake bungeni tena bila kupingwa ni ishara ya kuwa wapiga kura wake walikubali kazi yake, na hiyo inamjengea hoja kuwa japo si msemaji ni mtendaji. Kama ni kweli au si kweli wananchi wa Chato wanamajibu sahihi.

J.P Magufuli ni kiongozi ambaye ametuonyesha mengi yaliyowashinda wenzake.mambo. Anaifahamu vizuri kazi yake na yupo tayari kusimamia sheria zetu wenyewe hata kama ni za kurithi kutoka kwa mkoloni.
Kukubalika kwake kunatokana na kufuata kanuni, sheria na mipango.
Kwanfano aliposimamia ujenzi wa bara bara, ile ni sehemu ya kutumia na kuendeleza rasilimali za taifa.
Alipotuonyesha kuwa tumelala na watu wanavua samaki karibu na kigamboni alisimamia rasilimali za taifa.

J.P.M anaposema ujenzi haramu ndani ya hifadhi za bara bara anasimamia matumizi ya kile kidogo tulicho nacho kwa manufaa yetu sote,kwa kuzingatia sheria tulizozikubali sisi wenyewe na kumkabidhi azisimamie.

Kitendo cha viongozi wa juu kumsema mbele ya mikutano ni ukiukaji wa kanuni za uwajibikaji wa pamoja 'collective responsibility'. Sijui kama PM au Rais wameshindwa kuwasiliana naye faragha hadi kusimanga hadharani.

Viongozi wanajali kura zaidi na si sheria walizoapa kuzisimamia ' cheap popularity'. Utamaduni uliotufikisha mahali wizi, ubadhirifu na ufujaji ni sehemu ya uongozi.

La kushangaza,ni kitendo cha J.P kutojiuzulu. Kanuni za utawala bora zinasema kunapokuwa na tofauti za mitazamo wazi kiongozi anatakiwa ajiuzulu.
Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri hata kama si msemaji wa wazi kama
mbunge, sijui anasubiri nini na kama anataka kuwa malaika ndani ya kundi la wahalifu.

Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.

Bunge kuwa mhuri hakumzuii mbunge mwenye uchungu na raslimali za taifa kujitokeza na wananchi kumtambua.

Ni dhahiri wabunge wengi wa CCM akiwemo Mhe Magufuli huonga kupita katika chaguzi ndogo na uchuguzi mkuu kama amabvyo tumethibitishiwa yaliyotokea huko chato.

Hatutaki sweeping statements kama hizi tuja sheria gani anasimamia ili tuichambue na udahifu wake katika kusimamia sheria hiyo pia.

Ili ujenzi wa miundo mbinu kama barabara uweze kuwa endelevu hapa nchini ni lazima raslimali za taifa zisimamie vizuri kwa manua ya wote. Kama Magufuli amekuwa katika barza la Mawaziri toka mwaka 200o na ndipo wizi na ubadhirifu wa raslimali na mali za umma mkubwa ambao haujawahi kushuhudiwa ukitendwa na viongozi wa kitaifa k.m vile RAD, EPA, MEREMETA n.k ; tumuweke katika fungu gani na yeye ni fisadi, Nchi hii inyo mifano ya viongozi waliowahi kupinga maamuzi ya baraza la mawaziri kama vile Lyatonga Mrema na hivyo kupoteza nafasi ya uwaziri. kwanini Magufuli kama kweli ni msafi anashindwa kupinga maamuzi ya baraza la mawaziri yanayohujuma maslahi ya taifa?

Hilo la hifadhi za barabara ndio hulijui kabisa, na kama unalijua lizungumzea kwa kutaja sheria ipi anasimamia na ipi hao wananchi wanavunja? ili tuweze kuelimishana hapa.

Magufuli hajawahi kuwa na ajenda ya kusimamia raslimali samaki, uundwaji wa wizara ya kitoweo ilikuwa ni mbinu ya Luhanjo and team ya kumuondoa Magufuli wizara ya ardhi baada ya kuwa ametofautiana na Katibu Mkuu Salome Sijaona (miongoni mwa makatibu wakuu wa Luhanjo) kuhusu miardi ya uendelezwaji maeneo ya pembezoni mwa Jiji la DSM, hivyo walitumia fursa ya Lowassa kujiuzulu kuundwa kwa wizara hiyo na Magufuli akaondolewa ardhi na nafasi yake kuchukuliwa na Chiligati. Kwa kuwa wakubwa wake wanafahamu kuwa Mhe John Magufuli ni "Robot" alikabidhiwa takwimu ambzo kil kukicha alikuwa akizikariri na kuimba katika vyombo vya habari. Tujiulize katika sekta ya samaki alisidia kwa lipi kama sio kulitia taifa hasara ktk "Samaki wa Magufuli" kwa kukaidi ushauri wa wataalamu kwa pupa za kutafuta sifa.

In short Mhe John Magufuli hafai hata kupewa ukatibu kata. Ujerumani iliwaji kufanya makaosa kama haya kumkabidhi uraisi mtu mweny dalili zote za udikteta Hitler, alichaguliw akwa kura halali za wajerumani na ndio alisababisha vite vikuu vya dunia kwa kuvamia nchi zingine kwa tamaa ya kidkteta ya kutawala dunia. Hata kama tuana matatizoi namna gani ni heru tubaki na matatizo yetu kuliko kumptia mtu mwenye dalili za udikteta uongozi. Hivi leoMhe John Magufuli hawezi hata kufanya kiz na serikali za mitaa, wakati wa Mkapa alikuwa hawezi hata kufanya kazi na mawaziri wenzie.

Leo hii tukimpa Magufuli nchi akiamua kuanzisha vita nani ataweza kumshauri? Acha kabisa kucheza na moto ni heri kubaki na Kikwete wetu ambaye tunaweza kumkosoa na kumshauri na akasikia kuliko watu wenye dalili za udikteta, mtaacha hata hizo nyumba na magari yenu mkimbie nchi hii
 
sasa kwa mfano akiwa Rais Magufuli atatuongozaje?
Uzuri mmoja wa Maghufuli ni usimamizi wa sheria na maamuzi halali bila kuangalia makunyanzi ya yeyote. Sifa hii wanasiasa wengi hasa wa kuchaguliwa hawana. Analo tatizo la kutopima na kuona usahihi, uhalali na tija ya baadhi ya maamuzi kwa mfano Cabinet ya Mkapa ilipoamua wajiuzie nyumba na viwanja vya serikali.
 
Mhe John Magufuli alishindwa kujiuzuru wakati Waziri Mkuu Pinda na JK walipomkemea kuhusu kutumia ubabe kubomoa nyumba za wananchi anaodai kuwa wamejenga katika hifadhi ya barabara kwa sababu anafahamu wazi kuwa alikuwa akitumia sheria feki
kuhalalisha madai yake,

Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 kinatamka kuwa "Ugawaji wa ardhi uliofanywa kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya tarehe 01 Januari 1970 na tarehe 31 Desemba 1977, kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila kuzingatia sheria yoyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu kwa kisheria kwa kundi la watu waliogawiwa ardhi hiyo......

Na kifungu cha 16 kinatamaka "Kwa madhumuni ya kuepusha mashaka na ili kuwezesha kuwapo kwa usalama wa miliki ya ardhi na hivyo kuchangia maendeleo ya ardhi ya kijiji, masharti ya Kifungu cha 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na Halmashauri ya Kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya tarehe 01 Januari 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria hii na kwamba badala ya tarehe zilizotajwa katika kifungu cha 15, kumewekwa tarehe kati ya tarehe 01 Januari 1978 na tarehe ya sheria hii kuanza kutumika".

Sasa ni wapi katika Tanzania hii hapakuwa ardhi ya kijiji? ndio maana Waziri Mkuu na JK walimwagiza nyumba za wananchi zibomolewe tu pale barabara zinapotaka kujengwa na kwa kushirikisha ngzai za mkoa, willaya Manispaa na Serikali za mitaa ili kuwabaini wale wanaostahili na wasiostahili kulipwa fidia kwani sio kila aliyejenga nyumba hapo alivamia eneo la hifadhi ya barabara.

Kama Magufuli angekuwa ni kiongozi mzuri anayefuata sheria kama baadhi ya watu wanavyotutaka tuamini ni dhahiri kuwa angefuata sheria zote za nchi hii zilizopitishwa na bunge na sio kuchagua baadhi ya sheria. Mawaziri huapa kiitii katiba ya nchi sasa huku kuwakosesha wananchi haki zao kwa makusudi ili kupata umaarufu ndio iiutii katiba. Japo JK na Pinda wana udhaifu wa kibinadamu lakini katika suala hili la kumwadabisha huyu mbabe nawafagilia sana na nipo tayarii kumvumilia JK na serikali yake kuliko kumpatia huyu mbabe madaraka akija kuamua kuanzisha vita itakuwaje?
 
Uzuri mmoja wa Maghufuli ni usimamizi wa sheria

.na maamuzi halali bila kuangalia makunyanzi ya yeyote. Sifa hii wanasiasa wengi hasa wa kuchaguliwa hawana. Analo tatizo la kutopima na kuona usahihi, uhalali na tija ya baadhi ya maamuzi kwa mfano Cabinet ya Mkapa ilipoamua wajiuzie nyumba na viwanja vya serikali.
Naomba utaje hiyo sheria anayoisimamia ili tuijadili badala ya kutaja mambo kwa ujumla wake
 
Kinachonifurahisha kwa masikitiko ni pale unapokuta waliomkoromea magufuli wanajulikana kwa kukosa meno na nguvu kiasi cha kuwa bendera ambayo hutikiswa hata na pumzi badala ya upepo! Mifano ipo mingi hasa kwenye epa,meremeta, kagoda, na hivi karibuni tuzo ya dowans ambapo tumewashuhudia watawala wakubwa kabisa wakigeuka kuwa bendera.

Unaonyesha dhahiri kuwa hujui hata set up ya Katiba yetu. Nani kakuambia kuwa Magufuli sio part ya huo uchafu ulioutaja yaani epa,meremeta, kagoda, na hivi karibuni tuzo ya dowans; magufuli hasa been part of the Executive since the year 2000 kwa kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri. Namfagilia sana Lyatonga Mrema aliyeamua kupingana maanuzi ya barza la mawaziri la Mwinyi na hivyo kupoteza uwaziri, lakini sio huku kuganga njaa kwa magufuli.
 
Naomba utaje hiyo sheria anayoisimamia ili tuijadili badala ya kutaja mambo kwa ujumla wake
Anazitaja mara kwa mara kwa kila maamuzi anayofanya kama waziri mwenye dhamana ikiwemo hii ya kupandisha nauli ya feri. Alifuata taratibu zote.
 
Anazitaja mara kwa mara kwa kila maamuzi anayofanya kama waziri mwenye dhamana ikiwemo hii ya kupandisha nauli ya feri. Alifuata taratibu zote.

kwa hiyo unashabikia kitu blindly bila ya kujua hizo sheria zinasemaje, kwa taarifa yako Magufuli natumia sheria feki na hupindisha sheria to serve his purpose. Ndio maan wakubwa wake walimkemea kuacha ubabe. Ni vyema ukitaka kuzungumza mbele ya watu jielimishe kwanza hizo sheria ndipo huzitaje mbele ya watu.
 
WaTz wote njaa inasumbua. So hata kama ukipewa wewe nafasi kubwa ni hakika utajiangalia mwenyewe kwanza na familia yako. Na hasa katika kipindi hiki ambapo ilitabiriwa ya kuwa "watu watakuwa wenye kupenda fedha, wenye kujipenda wenyewe, wenye mfano wa utauwa huku wakikana nguvu zake".
 
Mkuu

Bado sijapata madhumuni ya article hii.

kwangu mimi sioni kuna umuhimu wa kufikiria Magufuli akiwa nje ya madaraka. Wengi tumemjua akiwa na madaraka na uwezo wake wa kutumia madaraka yake kusimamia sheria. Mimi binafsi nadiriki kusema kwa upande wa kutumia madaraka kusimamia sheria huyu bwana amefanikiwa.

Wapo wengi kama yeye ambao wamepewa madaraka na wameacha mambo yakiharibika. Sasa kuanza kufikiria Magufuli nje ya madaraka sioni mantiki. Sisi tumemjua kupitia madara na tunataka atumie hayo madaraka kufanikisha majukumu yake kwa kufuata sheria.

Kuanza kuzungumzia Magufuli atakuwaje akipewa madaraka makubwa kwa kujiuliza utendaji wake bila madaraka ni kujichanganya. Kwa nini tupige ramli ufanisi wake wa madaraka makubwa huku tukijilazimisha kumfikiria akiwa hana madaraka!! Kukosa madaraka ni sawa kuwa na madaraka makubwa zaidi!!

Tusicheze ngoma za watu. Kama kuna kundi limeanza kumwogopa kwa 2015, basi waanze kujipambanua kwa kutumia madaraka waliyonayo leo. Siyo kwa kuja na hoja zinazopingana.
 
kwa hiyo unashabikia kitu blindly bila ya kujua hizo sheria zinasemaje, kwa taarifa yako Magufuli natumia sheria feki na hupindisha sheria to serve his purpose. Ndio maan wakubwa wake walimkemea kuacha ubabe. Ni vyema ukitaka kuzungumza mbele ya watu jielimishe kwanza hizo sheria ndipo huzitaje mbele ya watu.
Kila anapozitaja sote tunasikia. Mimi huzitafuta na kuzisoma pia. Hakuna anakopindisha. Vinginevyo angenasa siku nyingi Bungeni ambako UONGO ni mwiko na unajua ana maadui wengi tu hasa ndani ya CCM, BUNGENI na serikalini kwa utendaji wake ambao wengi mnadhani anausaka URAIS. Acheni Maghufuli afanye kazi. Urais utakuja wenyewe. Hautafuti kama baadhi yenu.
 
:A S embarassed:
Nimeona michango mizuri ya great thinkers,chamsingi ni kujitahidi kuwa na data mtu unapoongea mambo muhimu hasa yanayogusa mustakabali wa nchi yetu,labda niulize wadau hivi tukiambiwa tutaje top three ya mawaziri wa awamu hii ambao japo utendaji wao unaonekana bila kuhusisha ushabiki nani atakuwemo?
 
Back
Top Bottom