Mkuu MMKJJ mambo mengi anayoonge Jatropha tumekwisha yaongeea na kuyarudia mara nyingi sana katika threads zilizopita, tatizo ninaloliona mimi humu JF kuna watu wa Magufuri na baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara yake ambao labda walishauriana naye hili swala kisiasa zaidi, na sasa wanapoona kuna wataalam wanaolijua zaidi wanakimbia na hawa jibu hoja yoyote badala yake wanafungua thread mpya, wewe subiri utaona wanakimbia humu katika hii thread kabisa na wataanzisha nyingine, lakini kitu wanachotakiwa kujua ni kuwa Tanzania hivi sasa ina wataalam tena wazuri sana katika kila kona za Dunia hii, pia inaonekana hata hapo Wizarani kwao kuna wataalam wazuri ambao mawazo yao yanapuuzwa kwasababu wao hawapo katika malengo ya Magufuri ya kisiasa, nasema hivi kwasababu ukichambuwa vyema hili swala mi naona dalili ya kuwa Waziri Mkuu alitonywa na wataalam wa Wizara hiyohiyo kuwa huyu jamaa anatengeneza bomu hapa wizarani ebu zueni haraka sana!
We angalia kwa mfano walijenga Jengo la Meneja wa TANROADS kwa gharama za walipa kodi alafu anakuja kulibomoa haraka haraka kwa ajili ya sifa, lakini Mwanakijiji ukae ukijua hii yote ni kuumiza walalahoi na walipa kodi kwasababu ya uzembe wa wachache, kwanini hatujaambiwa sababu ya hasara hiyo na imetugharimu kiasi gani?, maana kama unajenga nyumba ya serikali sehemu amabayo baadae unakuja kubomoa maana yake nini? na sehemu kubwa ya ujenzi uliobomolewa pale ulifanyika Magufuri akiwa Waziri wa wizara hiyo. kwanini watanzania wasiambiwe nini kilitokea mpaka fedha za serikali zikawekezwa sehemu ambayo haiitajiki?, na waliosababisha wamechukuliwa hatua gani? Sisi tunatakushabikia kubebeshwa mzigo ambao sio wa kwetu, maana ki ukweli ubomoaji wa jengo la TANROADS ulipaswa kwenda na hatua za kinidhamu dhidi ya Muhusika aliyeleta hasara hiyo! kwani Tanzania tunashida ya ardhi kiasi cha kuingiza serikali hasara kiasi hicho? kama walijua watabomowa baadae kwanini hawakuweka majengo ya temporary kama mbao, kontena nk. Hii peke yake inatosha kutia shaka juu ya walichokuwa wanafanya maana kama lile eneo ni Right of Way na wao ndio watunzanji wa RoW ilikuwaje wajenge jengo la kudumu ndani ya RoW?! na kwa hasara ya nani?
Mambo ya kitaalam hayapaswi kufanywa kisiasa hata siku moja, watanzania tunataka wanasiasa kutatua matatizo ya kitaalam ndio maana hatuendi mbele badala yake ni kurudi nyuma kila siku.