Magufuli bila madaraka yukoje?

Magufuli bila madaraka yukoje?

Tunajadili hoja ya if I were a tree..., au kama Kikwete asingekuwa Mukuere, leo angekuwa wapi? Hatutakuja pata hitimisho zuri..

Lakini pia hapa kuna jambo moja zuri katika mada hii, nalo ni kuwa: tunamjadili Magufuli kwa sababu ametokeza kichwa chake juu...
 
Kaka (sijui dada) kwani hadi juzi tuu alipokosana na mabosi wake kuhusu bomoa bomoa hadi PM akamwambia go slow mzee na bomoa alikuwa anasimamia nini? Tatizo sisi tunafanya makosa na tunatafuta sympathy ya viongozi wavivu na wabadhirifu na wavinjaji wa katiba. Hii haiwezekani! Kiongozi ni Pombe ambaye kwa sehemu unamwona akisimama kidete. Tibaijuka nae alikuwa ameanza kwanvguvu hiyo japo kwa sasa havumi tena.... Kimsingi ni vibaya kama tunatafuta huruma za viongozi na tunaweza kuwatisha viongozi kuwa kama hufanyi jambo fulani sisi hatuwapi kura wakati mojawapo ya majukumu ya kiongozi ni kusimamia sheria. Sasa kiongiz asimamie sheriaon the expense of kura afahamike vile aua awakumbatie wavunja sheria (ambao si wengi kwenye jamii) ili waumie wananchi walio wengi?
Hatutaki sweeping statements, naomba utoe mfano wa sheria gani anazisimamia?
 
MImi nahisi wanaopinga utendaji wa Pombe Magufuli kwa mambo ya Kigamboni au hata bomoa bomoa wana lao jambo. Ni wavunja sheria. Ningependa kusikiliza wale wanaohoji mambo kama uuzwaji wa nyumba kwa maana ya yeye kujinunulia nyumba....but kwa haya tunayojadilia ya bomoa bomoa na ulipaji nauli Pombe yuko juu. Nampongeza na wala hateteleki! Pengine kutoteteleka kwake ndo kunaonekana kuwa ubabe. Natamani siku yakimzidi ajivue gamba na kusema kama PM na wengine wanamwambia go slow mzee yeye kama msimamizi wa sheria aji'ng'atue!
 
Kila anapozitaja sote tunasikia. Mimi huzitafuta na kuzisoma pia. Hakuna anakopindisha. Vinginevyo angenasa siku nyingi Bungeni ambako UONGO ni mwiko na unajua ana maadui wengi tu hasa ndani ya CCM, BUNGENI na serikalini kwa utendaji wake ambao wengi mnadhani anausaka URAIS. Acheni Maghufuli afanye kazi. Urais utakuja wenyewe. Hautafuti kama baadhi yenu.

Usijifiche nyuma ya kauli za Magufuli, nataka wewe kama mchnguaji utaje hata sheia moja ambayo unadai kuisoma. Kitendo cha kushindwa hata kutaja jina la sheria husika kinadhihirisha wewe ni shabiki na tunapoteza mida kujadili na mashabiki.
 
Sina uwezo wa kuzikariri sheria hizi kama afanyavyo Maghufuli mwenyewe. Nawashangaa mnaofahamu anazivunja/anazipindisha sheria za nchi kwa manufaa yake mnamwacha huku mkijua mahakama zetu ziko wazi kila siku ya kazi. Tungekuwa na Maghufuli wawili tu nchi hii mambo yangekuwa tofauti. Hajui kufisadi, kujilimbikizia mali, kutafuta vyeo kila mahali, hana makundi wala maswahiba,...
 
Mkuu MM pole kwa majukumu!
Mara zote nathamini na ninaheshimu sana michango yako lakini kwa hili la leo naona umeteleza kidogo. JPM ni kiongozi ambaye kwa CCM amejaribu japo kwa uchache kuonyesha uchapakazi kazi. Ni lazima tuelewe kuwa JPM sio malaika na kwa maana hiyo ana mapungufu mengine mengi ya kibinadamu kama ilivyo kwa watu wote. Kwa hiyo kitendo cha yeye kuwa na mapungufu katika utendaji wake sio cha ajabu. Lakini sioni kibaya ambacho JPM amekifanya na kwa hiyo ni lazima ajiuzuru.

Pamoja na hayo sioni mantiki yoyote ya wewe kutaka kujua Magufuli bila madaraka anakuwaje!? Its irrelevant! Ukijua anavyokuwa bila madaraka itakuwa na msaada gani! Wengi wetu tumemjua Magufuli akiwa na madaraka na amefanya aliyofanya! Cha msingi ni je akiwa na madaraka anafanya nini!? Kama ni hivyo tujiulize JK, Pinda, Makinda na mawaziri wengine wote bila madaraka wanakuwaje! Sijaona hoja yoyote ya msingi kwenye thread yako zaidi ya siasa! Tuwaache wanasiasa wenzake wapambane nae lakini sisi tuendelee kujadili hoja za msingi na sio kuchochea mambo yasiyo na msingi.

Kwa mtazamo wangu katika mawaziri wa JK, at least JPM ameonyesha umakini wa kufuatilia mambo ndani ya wizara yake hata kama kuna mapungufu kidogo.
 
Tatizo la Magufuli ni kutegemea utendaji wake.

Hana 'mtandao' wa ushindi huko CCM, hana waandishi 'njaa' wa kumpigia debe na kumpamba.

Yuko kivyake akichapa kazi bila kumwangalia nyani usoni. Na hii ndiyo inam cost
 
namfagilia kinoma magufuli ni mchapakazi na ni hodari mwenye kumlaumu ana chuki zake binafsi
 
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?

Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?

Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?

Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?

Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?

Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:

a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.

b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.

Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:

a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.

b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty
Watanzania bwana!! kwanini mnamjadili Magufuli kujiuzulu???yaani na makala kabisa mmekaa ya kujadili Magufuli kujiuzulu????you guys!!! are you serious??mmekosa kabisa cha kujadili tz hii ya hovyo mpaka mnajadili kujiuzulu kwa Magufuli???na ndiyo mnaitwa sijui think tanks!!kweli?? hivi....ebu MMKJ naomba tu(kwa vile umeamua kujadili utendaji wa huyu waziri)..ebu tueleze ni waziri gani katika cabinet ya JK ambaye anamkaribia angalau Magufuli kiutendaji???just be frank alafu tueleze humu.....maana sasa naona imefikia tz kweli ule ukweli wa kwamba waziri anaezungumzia uvundo anabezwa na wale walioko kimya huku wakipiga siasa wakionekana wana nafuu....this is absolutely ridiculous yaani......Hivi..lets be frank...Magufuli anatofautiana na Rais na Waziri mkuu ambao wanaonyesha utendaji gani kwa wananchi wao kiasi cha kumfanya Magufuli awe na justification ya kujiuzulu????hawa Rais na Waziri mkuu wana maamuzi gani wamewafanyia watanzania kiasi cha kumfanya Magufuli awafanye wakose imani juu ya uwezo wake kiutendaji????...you guys...hizi siasa(tena on a personal level)hazitaisaidia tz kamwe.....kwa vie mmeamua kumjadili Magufuli on a personal level...pia mjadilini comparatively...yaani pia mlinganisheni na mawaziri wenzake ktk cabinet then mje humu na conclusion as to who is fairly supposed to resign ktk cabinet ya JK(kama si woote pamoja na rais wao....)......pevukeni wajamaa......
 
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?

Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?

Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?

Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?

Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?

Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:

a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.

b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.

Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:

a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.

b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty
Those days!! Kwa sasa vipi?
 
nabashiri kuwa anajisikia vizuri, hasa ktk mada hii mengi ya content zake kwa sasa zipo dhahiri kabisa, hivyo mleta mada anafikiria vizuri.

Ninadhani humjui unayemzungumzia ndugu, jaribu kutafuta mada zake katika kipindi hiki cha utawala wa Uncle Magufuli utaelewa ninamaanisha nini.
 
Kila kitu kinaonekana sasa
mhmmmmmmmmm!!!!!!!! nadhani hautakuwa fair kuhitimisha kama mdugu chakaza pale juu kutokana na utofauti wa muda wa madaraka baina yao. mwaka 1 kwa 10,..............................?????????????
 
Back
Top Bottom