Magufuli bila madaraka yukoje?

Magufuli bila madaraka yukoje?

Magufuli amekuwa katika baraza la mawaziri la Mhe Benjamini Mkapa vipindi vyote viwili na kushiriki kubariki mikataba mibovu yote inayotesa nchi, kufulkia watu wakiwa hai huko Bulyanhulu, EPA, KAGODA, MEREMETA n.k. Kibaya zaidi alichoongeza binafsi ni kutumia ubabe kuuza nyumba za serikali kwa bei poa. Hilo ni dhambi ya kwake binafsi.

Kuhusu kufuata sheria, kwa kuwa anatambua kuwa watanzania wengi wana kiu ya kuona sheria zikifuatwa basi Magufuli hutumia kauli mbiu hiyo kujipigia chapuo lakini ukichunguza kwa makini yeye sio muumini mzuri wa utawala wa sheria na kanuni za utawala bora.
 
Mhe. Dr Pombe si msafi na mwadilifu kihivyo, ni mpenda sifa flani na publicity tu. Kama angekuwa na ubavu angechomoa hiyo post. Huyu jamaa si ndo aliuza nyumba za wananchi na sasa viongozi wa serikali inawajibika kukaa hotelini kwa gharama zetu.Mchumia tumbo tu.Pita mitaa ya kwake pale O'bay/Ada Estate uone uadilfu wake.
 
Ndugu MM, topic yako hii, inaweza kukuweka mahali pabaya hata wewe, kwa sababu inaonekana kama kumjadili mtu. Tukumbuke kuwa simple minds discuss people...

Kuhusu Pombwe Magufuri, ni mwana sayansi. Watu wengi waliosoma sayansi wana namna yao ya utendaji. Wakijua principle inasema hivi..wao huanza kutekeleza kulingana na hiyo principle inavyosema. Si waongeaji sana kama wewe MM, au kama walivyo wanasiasa per se. Hawaongei sana kama wansheria, au watu waliosoma sana historia. Hawa ni watu, katika aina za watu, wenye kundi lao, ni watendaji.

Kuhusu uuzaji wa nyumba, ilikuwa ni maamuzi ya pamoja katika baraza la mawaziri, kipindi cha serikali ya BW Mkapa. Mkapa alikuwa na utaratibu wa kufanya vikao na mawaziri wake ili waweze kuwa na uamuzi wa pamoja. Naona Kikwete hilo si muhimu sana, yeye anawatembelea huko huko wizarani kwao mmoja mmoja. Kwahiyo baada ya uamuzi huo, Magufuri alianza kutekeleza kwa kishindo principle ya baraza la mawaziri.

Kuhusu hili la bomoa bomoa, naona lina sababu tatu (1) sheria ndio inataka hivyo (2) ilani ya uchaguzi inatao ahadi ya kujenga fly overs na usafiri wa kasi (3) alipelekwa wizara hiyo kwenda kuondoa malalamiko mengi yaliyokuwepo ikiwa ni pamoja na ufisadi.

Kwasababu hizo tu rais alitakiwa kumpa special treatment, yaani kuwa naye karibu ili kuweza kumrekebisha pale anapoharibu na kumpa moyo ili afanye ile kazi aliyompa aifanye katika hiyo wizara ngumu.

Magufuri, amejijengea jina, ambalo hata asipokuwa na madaraka, wengi mtamkumbuka. Ndiyo maana leo tunamjadili yeye na siyo Dr Kawambwa. Ndio maana Lyatonga Mrema ambaye hana madaraka ya uwaziri, lakini nchi nzima tunakumbuka utendaji wake. Hata Hayati Moringe Sokoinne, pia hatasahaulika kwa uwezo wa kutekeleza na kufuatilia utekelezaji katika serikali ya awamu ya kwanza.

Mwisho, kila mtu anaweza kuwa na taswira yake kutegemea na kazi anayofanya, madaraka aliyopewa na aina ya mkuu wake wa kazi alivyo. Kama Dr JP Magufuri angekuwa anafanya kazi chini ya rais Nyerere au Dr Slaa, nadhani angeweza kuwa na manufaa makubwa sana kwa taifa hili.
 
Mm na wanajamii, msishangae sana kwa Magufuli kuto kujiuzulu, ni kawaida ya serikali ya ccm kupishana mara zote, mmesahau Marsha alikuwa anapishana na bosi wake kuhusu uraia wa bashe yeye kama waziri akatoa yake na mkulu yake.

hii ndio ccm bana msiishangae hata kdg
 
Mwanakijiji nimerudia kauli hii mara nyingi...........hakuna jipya kwa magufuri maana hata kwenye hawamu iliyopita aliweka X kwenye nyumba nyingi tu na hadi anaondoka Mkapa na kuingia JK hakuna lililofanyika zaidi ya watu kupiga rangi na kufuta uchafu waliowekewa kwenye nyumba zao na maisha kuendelea.
Nawahakikishia kuwa na huu ni usanii ule ule. Hakuna jipya hakuna litakalotokea, na Magufuri anafahamu hilo.
Mambo ya kujiuzulu sijui nini hayo ndio msahau kabisa!!!!! hawezi na nasema hawezi. Ubavu huo autoe wapi bana?
Nchi hii ni ya ajabu sana. Yaani mwenyekiti wa CCM tena wa zamani (not current) na waziri mdogo tu kwenye hawamu hii kule Bukoba ambao nyumba zao zimewekewa X wamemfanya waziri mkuu na rais wa nchi kutoka povu, unadhani magufuri ni nani? Nyie acha tu usanii wetu uendelee.
Hivi wewe mwanakijiji ulimuelewa rais? Upande mmoja anasema wasibomolewe, upande mwingine anasema watu wajue kuna siku watabomolewa tu, upande mwingine anadai busara, upande mwingine anasema wasubiri(yaani watu waendelee kukaa) mpaka siku barabara zitakapokuwa zinaanza kujengwa ndio waondoke! unaelewa alikuwa anamaanisha nini?
Tuangalie mengine haya ya Magufuri ni usanii mwingine.
 
Alisimamia na kubariki kuuzwa kwa nyumba za serikali
Alitumia wadhifa wake kushinikiza mdogo wake kupewa nyumba za NHC
Ana vimada kadhaa Chuo Kikuu Mlimani
Ni mtu anayependa sifa na kutaka kuonekana kwamba yeye ni mtendaji kuliko wengine
Ni mkabila....na kutokana na hilo Wasukuma wamemtenga na kumwita yeye sio Msukuma halisi
Ni mbabaishaji
 
Magufuli anafaa sana, mbona Pinda ana Madara makubwa amefanya nini?!! kwani Pinda na Magufuli nani mtendaji hata kama ni kwa kutumia madaraka?!! kwangu pinda hafai kabisa hata kuwa naibu katibu mkuu,kazi yake ni kulia lia tuuu lakini hana kitu
 
Tatizo ni kutokuheshimu sheria zilizopo. Sheria ziko wazi kabisa lakini watu hawaheshimu hizo sheria unategemea nini? Jengo lilie la Tanesco kisheria halikutakiwa kujengwa pale. Lakini kutokana na kutokuheshimu sheria zilizowekwa watu wamejenga wakichukuliwa hatua wanapiga kelele zisizo na msingi.
Kwa mfano kama ni kweli Magufuli alitaka Jengo la TANESCO-UBUNGO libomolewe, ilibidi afikirie kua lile jengo limejengwa kwa pesa yetu na ujenzi uliidhinishwa na Mawaziri husika walikokuwepo kabla yake Magufuli kwenye wizara hiyo. Likibomolewa leo, kesho kuna uwezekano atakuja waziri mwingine anayembadili Magufuli na akaidhinisha ujenzi tena katika sehemu hiyo - sasa utaona kua sisi ndio tunaliwa tokana na maamuzi ya kibabe toka kwa hao mawaziri wa CCM.

Magufuli angetufaa sana kama angesimamia na kuwakaba walioidhinisha ujenzi wa hilo jengo. Pia atatufaa kama atadhibiti ujenzi holela unaoendelea kukua na hapo hapo kupigania raia kupata viwanja vilivyopimwa haraka - bomoa bomoa is too easy kumpa sifa Magufuli. Vilivyofanywa kwa makosa na wenzake kabla yake, basi na waadhibiwe kwanza ili makosa yasirudiwe.

Kimsingi Magufuli si kiongozi mzuri, anafanya mambo kama kuruta - utafikiri amekatazwa kufikiri.
 
Unajua wana JF, watanzania wengi wamezoea viongozi ambao wanajua kutunga sheria lakini hawana ujasiri wa kusimamia sheria, na hawa kama Mh PINDA ndio wana mlalamikia Maghufuli. Tunahitaji Tanzania mtu kama JP Maghufuli, mtu ambaye hatafuti sifa kwa kujikomba kwani ametangaza rasmi kuwa hata kama ofisi ya CCM itakuwa ndani ya hifadhi ya barabara ataivunja bila huruma. Ni lini watanzania watajua kuwa kweli ukijenga kumbi ya starehe bila kibali utakatwa na kustakiwa, ni lini Watanzania wataamini kuwa kweli ukijenga ndani ya hifadhi ya barabara utavunjiwa? Ndio maana watu wanajenga wakiamini hakuna hatua yakuwavunjia zaidi ya kusemasema tu kwa maneno na hasa kama maswaiba wao wako katika kundi hilo

Jamani Maghufuli anatoa somo, kuna taratibu za kuishi Mijini, ndo maana DSM haiwezi kuwa safi kwani viongozi hawana ujasiri wa kutekeleza sheria na hivyo kila sehemu imekuwa gulio/soko na kuongeza msongamano usiokuwa wa lazima. Wameshindwa kuwaondoa wapiga debe sababu tu ya kuchekacheka na kanuni na sheria

BIIIIG UP Maghufuli.
 
Tuangalie kwa ufupi. Huyu bwana alipoingia bungeni ulikuwa wakati wa Msekwa ambapo bunge lilikuwa mhuri tu na haikuwa rahisi sana kujua wapiganaji kwa uwazi hasa ukiwa ndani ya chama. Halafu akawa waziri jambo lililombana zaidi.

Kurudi kwake bungeni tena bila kupingwa ni ishara ya kuwa wapiga kura wake walikubali kazi yake, na hiyo inamjengea hoja kuwa japo si msemaji ni mtendaji. Kama ni kweli au si kweli wananchi wa Chato wanamajibu sahihi.

J.P Magufuli ni kiongozi ambaye ametuonyesha mengi yaliyowashinda wenzake.mambo. Anaifahamu vizuri kazi yake na yupo tayari kusimamia sheria zetu wenyewe hata kama ni za kurithi kutoka kwa mkoloni.
Kukubalika kwake kunatokana na kufuata kanuni, sheria na mipango. Kwanfano aliposimamia ujenzi wa bara bara, ile ni sehemu ya kutumia na kuendeleza rasilimali za taifa. Alipotuonyesha kuwa tumelala na watu wanavua samaki karibu na kigamboni alisimamia rasilimali za taifa.

J.P.M anaposema ujenzi haramu ndani ya hifadhi za bara bara anasimamia matumizi ya kile kidogo tulicho nacho kwa manufaa yetu sote,kwa kuzingatia sheria tulizozikubali sisi wenyewe na kumkabidhi azisimamie.

Kitendo cha viongozi wa juu kumsema mbele ya mikutano ni ukiukaji wa kanuni za uwajibikaji wa pamoja 'collective responsibility'. Sijui kama PM au Rais wameshindwa kuwasiliana naye faragha hadi kusimanga hadharani.

Viongozi wanajali kura zaidi na si sheria walizoapa kuzisimamia ' cheap popularity'. Utamaduni uliotufikisha mahali wizi, ubadhirifu na ufujaji ni sehemu ya uongozi.

La kushangaza,ni kitendo cha J.P kutojiuzulu. Kanuni za utawala bora zinasema kunapokuwa na tofauti za mitazamo wazi kiongozi anatakiwa ajiuzulu.
Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri hata kama si msemaji wa wazi kama
mbunge, sijui anasubiri nini na kama anataka kuwa malaika ndani ya kundi la wahalifu.

Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.

Magufuli sio mtu anayefuata sheria hata kidogo, anatumia kauli mbiu ya "sheria" kujijengea umaarufu tu, kwa kuwa anafahamu watanzania wengi ni wavivu kusoma sheria hivyo wataamini kauli aake kuwa ni waziri. Mfano hai wa Magufuli kutofuata sheria na kukandamiza hali za wananchi ni case ifuatayo:- Mwaka 1999 wakati inatungwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999, Magufuli alikuwa miongonji mwa wabunge walioipitisha. Kifungu cha 15 cha sheria hiyo kinatamka hivi UGAWAjI WA ARDHI ULIOFANYWA KWA MTU AU KUNDI LA WATU WAISHIO AU WALIOTAKIWA KUHAMIA NA KUISHI KATIKA KIJIJI WAKATI WOWOTE KATI YA 01 JAN 1970 HADI 31 DES 1977 , KAMA UGAWAJI HUO ULIFANYWA KWA MUJIBU WA SHERIA AU KINYUME CHA SHERIA AU BILA KUZINGATIA SHERIA YOYOTE, SASA INATHIBITISHWA KUWA UGAWAJI HUO NI HALALI NA KWAMBA DAIMA NI WENYE NGUVU YA KUTOA HAKI NA WAJIBU WA KISHERIA KWA KUNDI LA WATU WALIOGAWIWA ARDHI HIYO....." Aidh Kifungu cha 16 Kinatamka .......... MASHARTI YA KIFUNGU 15 YATATUMIKA KILA MARA UGAWAJI WA ARDHI YA KIJIJI ULIPOFANYWA NA HALMASHAURI YA KIJIJI AU MAMLAKA NYINGINE YOYOTE MNAMO NA BAADA YA 01 JAN 1978 HADI TAREHE YA KUANZA KUTUMIKA KWA SHERIA HII.

Wakati wa opersheni vijiji miaka ya 1970's maenEo kati ya Ubungo hadi Kiruvia pia vilianzishwa vijiji vya Kimara, Mbezi Kibamba na Kiruvia ambavyo vilibadsilishiwa hAdhi na kuwa chini ya Mipango Miji mwaka 1985. Kwa mujibu wa vifungu vy sheria iliyotajwa hapo juu ambayo Mhe John magufuli lishiriki kuipitisha wananhci wote waliokuwa wakiishi katika vijiji hivyo hadi mwaka 1985 wana haki na ardhi wanayoimiliki na kama Serikali inaitaka ardhi hiyo ni lazima kuwalipa fidia. Kwa maneno mengine ukisoma kwa makini maneno in bold sheria feki anazotumia Magufuli za 1930's na 1967 ziliisha uhai katika maeneo yaliyokuwa vijiji vya ujamaa kutokea mwaka 1999.

Kwa kuwa Mhe John Magufuli alifahamua kuwa Serikali huchulewa kuchapa, kusambaza na kutoa elimu kwa wananchi ya sheria mbali mbali zinazopitishwa na bunge kutoakana na ukosefu wa fedha, mwaka 2000 alipochaguliwa kuwa waziri wa ujenzi kwa mara ya kwanza (ikiwa ni miezi michache baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo) bila huruma wala ubinadamu wowote Magufuli akaagiza kupandwa kwa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara Mita 120 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro pande zote mbili, kati ya Ubungo hadi Kibaha. Upana halali wa hifadhi ya barabara ni Mita 22 tu. Hata kama sheria ya vijiji ilifuta hata sheria ya barabara, kama Magufuli angekuwa amedea na Upana halali wa Road Reserve wa Mita 22 pande zote mbili kidogo wananchi wangeweza kumwelewa kuwa ana nia njema.

Hivyo Magufuli alitoa maagizo na kuwatendea wananchi mambo yaliyo kinyume cha sheria ya Ardhi ya Vijiji vifungu nilivyovitaja hapo juu. Na ili kuhakikisha wananchi kati ya Ubungo hadi Kibaha wanakosa haki yao kabisa kwa ubabe wake wa kawaidia aliingia katika ardhi na makazi halalai ya wananchi chini ya sheria zilizotungwa na bunge bila ya kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa, Tarafa, Kata wala Serikali za Mitaa na mpaka sasa hataki majadiliano ya iana yoyote yanayohusu haki za wananchi hawa. Je huu ndio mfano wa kiongozi bora mnayemtaka? Viongozi kama hawa Mwalimu Nyerere alisema hawafai hata kupewa Ujumbe wa shina.

Magufuli aliamua kuwatendea unyama huo wananchi wanaoishi kati ya Ubungo hadi Kibaha kwa kuwa alifahamu wananchi wana ufahamu mdogo wa haki zao chini ya sheria ya vijiji. Kutokana na kuwa na ufahamu mdogo wananchi wanaomiliki ardhi na makazi ndani ya eneo hilo walikaa kimya na kuathirika kijamii na kiuchumi kwa miaka 9 mpaka 2010 alipoanzsiha zoezi la kutaka kubomoa nyumba hizo kwa kisingizio cha kutekeleza mradi wa mabasi yaendayo kasi na msongamnao wa magari.

Cha ajabu upana unaohitajiwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi hauzidi Mita 10, mfano hai ni upana ulioachwa na jengojipya la Benki ya Wananchi ya Dar es Salaam (DCB) lililojengwa hivi karibuni pale Magomeni na ukarabati wa kusogeza nyuma uizo wa Chuo cha DIT. Kwa hali hiyo, Je ni kweli nyumba zilizoko Mita 100 kutoka katikati ya barabara kati ya Ubungo hadi Kimara Magufuli alizoagizi ziweweke alama ya X na kuagiza zibomolewe zinazuia ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasiau zinachanmgia vipi msongamano wa magari?

Ndio maana wakubwa wake wameagiza historia ya maeno izingatiwe na wananchi walipwe fidia kama kuna hajaya nyumba kubomolewa.

Kuhusu Magufuli kusemwa hadharani ni haki yake kwa kuwa Gazeti la Tanzania Daima liliripoti kuw kabla ya Waziri Mkuu kumsema hadharani alimwita na wakakaa mara mbili kuhusu suala hilo lakini Magufuli akakaidi na kutunga msamiati kuwa ameapa kulinda sheria. Hivuo ili kulinda haki za wananchi na kulinda serikali ili ni lazima ashughulikiwe kidogo.
 
Mwanakijiji nimerudia kauli hii mara nyingi...........hakuna jipya kwa magufuri maana hata kwenye hawamu iliyopita aliweka X kwenye nyumba nyingi tu na hadi anaondoka Mkapa na kuingia JK hakuna lililofanyika zaidi ya watu kupiga rangi na kufuta uchafu waliowekewa kwenye nyumba zao na maisha kuendelea.
Kama unadhani hana ubavu mbona Pinda na JK Jasho linawatoka? Si waache kwa vile hakuna jipya uone? kama ni usanii utakuwa si wa Maghufuli utakuwa ni wa Rais kama anavyojulikana kuwa ni MSANII.
 
Ukiangalia kwa umakini Hii "skendo" inatosha kwa watu makini ugunduakuwa Pombe sio kiongozi makini hata kidogo but just an opportunist anayetumia nafasi aliyopewa kujionyesha kuwa anajali na akini kumbe just opportunist.
 
Tatizo ni kutokuheshimu sheria zilizopo. Sheria ziko wazi kabisa lakini watu hawaheshimu hizo sheria unategemea nini? Jengo lilie la Tanesco kisheria halikutakiwa kujengwa pale. Lakini kutokana na kutokuheshimu sheria zilizowekwa watu wamejenga wakichukuliwa hatua wanapiga kelele zisizo na msingi.

Naomba ushahidi kuwa jengo la Tanesco halikustahili kujengwa hapo? Kama sio unategemea kauli za Magufuli pekee.
 
Tukiweka siasa pembeni kwenye baraza la mkwere hakuna waziri mtendaji kama Magufuli full Stop
 
Unajua wana JF, watanzania wengi wamezoea viongozi ambao wanajua kutunga sheria lakini hawana ujasiri wa kusimamia sheria, na hawa kama Mh PINDA ndio wana mlalamikia Maghufuli. Tunahitaji Tanzania mtu kama JP Maghufuli, mtu ambaye hatafuti sifa kwa kujikomba kwani ametangaza rasmi kuwa hata kama ofisi ya CCM itakuwa ndani ya hifadhi ya barabara ataivunja bila huruma. Ni lini watanzania watajua kuwa kweli ukijenga kumbi ya starehe bila kibali utakatwa na kustakiwa, ni lini Watanzania wataamini kuwa kweli ukijenga ndani ya hifadhi ya barabara utavunjiwa? Ndio maana watu wanajenga wakiamini hakuna hatua yakuwavunjia zaidi ya kusemasema tu kwa maneno na hasa kama maswaiba wao wako katika kundi hilo

Jamani Maghufuli anatoa somo, kuna taratibu za kuishi Mijini, ndo maana DSM haiwezi kuwa safi kwani viongozi hawana ujasiri wa kutekeleza sheria na hivyo kila sehemu imekuwa gulio/soko na kuongeza msongamano usiokuwa wa lazima. Wameshindwa kuwaondoa wapiga debe sababu tu ya kuchekacheka na kanuni na sheria

BIIIIG UP Maghufuli.

TATIZO HAPA MAGUFULI ANATUMIA SHERIA ZILIZOISHA UHAI KUTAMBUA UPANA WA HIFADHI YA BARABARA. HIFADHI YA BARABARA ILIKUWA NI MITA 22, MWAK 2009 IKAONGEZWA KUFIKIA MITA 30 KWA MUJIBU WA IBARA 27 (2) YA KANUNI ZA SHERIA ZA BARABARA ZA 2009, WAZIRI AKITAKA ARDHI YOYOTE KUWA SEHEMU YA BARABARA AU HIFADHI YA BARABARA ANATAKIWA KUWASILIANA NA WAZIRI WA ARDHI ILI ENEO HILO LIWEZE KUTENGWA HIVYO MWAKA 2009 UPANA WA HIFADHI YA BARABARA ULIPONGEZWA KWA MITA 8 KUTOKA MITA 22 HADI 30 KILA UOPANDE NCHI NZIMA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA BARABARA. ALICHOPASWA KUFANYA MAGUFULI NI KUWASILINA NA MAMA TIBAIJUKA WAZIRI WA ARDHI ILI MITA 8 HIZO ZILIZOONGEZEKA ZITENGWE RASMI KWA WANANCHI KULIPWA FIDIA.

IBARA YA 4 INATAMKA KUWA BAADA YA KUWASILINA NA WAZIRI WA ARDHI, WAZIRI WA UJENZI ANAPASWA KUNUNUA ARDHI HUSIKA. LAKINI KWA KUTUMIA NJIA ZA KIHUNI NA UBABE MAGUFULI ALIIAGIZA TANROAD KUFANYA KAZI AMBAYO SHERIA MAGUFULI ALIZOAPA KUZILINDA ZINATAMKA BAYANA KUWA KUWA ITAFANYWA NA WIZARA YA ARDHI YA KUTENGE ENEO HILO. NDIO MAAN KITENDO CHA KUWEKA ALAMA ZA X KATIKA NYUMBA ZA WANANCHI NJE YA MITA 22 KIMEPINGWA NCHI NZIMA. nI KUTOKANA NA KUKIUKA SHERIA ZA BARABARA ZINZOTAMKA KUWA ANAYHUSIKA NA KUTENGA ARDHI HIYO NI WIZARA YA ARDHI SIO TANROAD KWA ALAMA ZA X.
 
Attachments

Magufuli sio mtu anayefuata sheria hata kidogo, anatumia kauli mbiu ya "sheria" kujijengea umaarufu tu, kwa kuwa anafahamu watanzania wengi ni wavivu kusoma sheria hivyo wataamini kauli aake kuwa ni waziri. Mfano hai wa Magufuli kutofuata sheria na kukandamiza hali za wananchi ni case ifuatayo:- Mwaka 1999 wakati inatungwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999, Magufuli alikuwa miongonji mwa wabunge walioipitisha. Kifungu cha 15 cha sheria hiyo kinatamka hivi UGAWAjI WA ARDHI ULIOFANYWA KWA MTU AU KUNDI LA WATU WAISHIO AU WALIOTAKIWA KUHAMIA NA KUISHI KATIKA KIJIJI WAKATI WOWOTE KATI YA 01 JAN 1970 HADI 31 DES 1977 , KAMA UGAWAJI HUO ULIFANYWA KWA MUJIBU WA SHERIA AU KINYUME CHA SHERIA AU BILA KUZINGATIA SHERIA YOYOTE, SASA INATHIBITISHWA KUWA UGAWAJI HUO NI HALALI NA KWAMBA DAIMA NI WENYE NGUVU YA KUTOA HAKI NA WAJIBU WA KISHERIA KWA KUNDI LA WATU WALIOGAWIWA ARDHI HIYO....." Aidh Kifungu cha 16 Kinatamka .......... MASHARTI YA KIFUNGU 15 YATATUMIKA KILA MARA UGAWAJI WA ARDHI YA KIJIJI ULIPOFANYWA NA HALMASHAURI YA KIJIJI AU MAMLAKA NYINGINE YOYOTE MNAMO NA BAADA YA 01 JAN 1978 HADI TAREHE YA KUANZA KUTUMIKA KWA SHERIA HII.

Wakati wa opersheni vijiji miaka ya 1970's maenEo kati ya Ubungo hadi Kiruvia pia vilianzishwa vijiji vya Kimara, Mbezi Kibamba na Kiruvia ambavyo vilibadsilishiwa hAdhi na kuwa chini ya Mipango Miji mwaka 1985. Kwa mujibu wa vifungu vy sheria iliyotajwa hapo juu ambayo Mhe John magufuli lishiriki kuipitisha wananhci wote waliokuwa wakiishi katika vijiji hivyo hadi mwaka 1985 wana haki na ardhi wanayoimiliki na kama Serikali inaitaka ardhi hiyo ni lazima kuwalipa fidia. Kwa maneno mengine ukisoma kwa makini maneno in bold sheria feki anazotumia Magufuli za 1930's na 1967 ziliisha uhai katika maeneo yaliyokuwa vijiji vya ujamaa kutokea mwaka 1999.

Kwa kuwa Mhe John Magufuli alifahamua kuwa Serikali huchulewa kuchapa, kusambaza na kutoa elimu kwa wananchi ya sheria mbali mbali zinazopitishwa na bunge kutoakana na ukosefu wa fedha, mwaka 2000 alipochaguliwa kuwa waziri wa ujenzi kwa mara ya kwanza (ikiwa ni miezi michache baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo) bila huruma wala ubinadamu wowote Magufuli akaagiza kupandwa kwa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara Mita 120 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro pande zote mbili, kati ya Ubungo hadi Kibaha. Upana halali wa hifadhi ya barabara ni Mita 22 tu. Hata kama sheria ya vijiji ilifuta hata sheria ya barabara, kama Magufuli angekuwa amedea na Upana halali wa Road Reserve wa Mita 22 pande zote mbili kidogo wananchi wangeweza kumwelewa kuwa ana nia njema.

Hivyo Magufuli alitoa maagizo na kuwatendea wananchi mambo yaliyo kinyume cha sheria ya Ardhi ya Vijiji vifungu nilivyovitaja hapo juu. Na ili kuhakikisha wananchi kati ya Ubungo hadi Kibaha wanakosa haki yao kabisa kwa ubabe wake wa kawaidia aliingia katika ardhi na makazi halalai ya wananchi chini ya sheria zilizotungwa na bunge bila ya kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa, Tarafa, Kata wala Serikali za Mitaa na mpaka sasa hataki majadiliano ya iana yoyote yanayohusu haki za wananchi hawa. Je huu ndio mfano wa kiongozi bora mnayemtaka? Viongozi kama hawa Mwalimu Nyerere alisema hawafai hata kupewa Ujumbe wa shina.

Magufuli aliamua kuwatendea unyama huo wananchi wanaoishi kati ya Ubungo hadi Kibaha kwa kuwa alifahamu wananchi wana ufahamu mdogo wa haki zao chini ya sheria ya vijiji. Kutokana na kuwa na ufahamu mdogo wananchi wanaomiliki ardhi na makazi ndani ya eneo hilo walikaa kimya na kuathirika kijamii na kiuchumi kwa miaka 9 mpaka 2010 alipoanzsiha zoezi la kutaka kubomoa nyumba hizo kwa kisingizio cha kutekeleza mradi wa mabasi yaendayo kasi na msongamnao wa magari.

Cha ajabu upana unaohitajiwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi hauzidi Mita 10, mfano hai ni upana ulioachwa na jengojipya la Benki ya Wananchi ya Dar es Salaam (DCB) lililojengwa hivi karibuni pale Magomeni na ukarabati wa kusogeza nyuma uizo wa Chuo cha DIT. Kwa hali hiyo, Je ni kweli nyumba zilizoko Mita 100 kutoka katikati ya barabara kati ya Ubungo hadi Kimara Magufuli alizoagizi ziweweke alama ya X na kuagiza zibomolewe zinazuia ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasiau zinachanmgia vipi msongamano wa magari?

Ndio maana wakubwa wake wameagiza historia ya maeno izingatiwe na wananchi walipwe fidia kama kuna hajaya nyumba kubomolewa.

Kuhusu Magufuli kusemwa hadharani ni haki yake kwa kuwa Gazeti la Tanzania Daima liliripoti kuw kabla ya Waziri Mkuu kumsema hadharani alimwita na wakakaa mara mbili kuhusu suala hilo lakini Magufuli akakaidi na kutunga msamiati kuwa ameapa kulinda sheria. Hivuo ili kulinda haki za wananchi na kulinda serikali ili ni lazima ashughulikiwe kidogo.

Mh ulivyojenga hoja yako inatia mshaka sana. Unataka tuamini kuwa Maghufuli ana kinyongo na wakazi kuanzai ubungo hadi kibaha kitu ambacho siwezi kuamini kirahisi angalia kauli hii:[ Na ili kuhakikisha wananchi kati ya Ubungo hadi Kibaha wanakosa haki yao kabisa kwa ubabe wake wa kawaidia aliingia katika ardhi na makazi halalai ya wananchi chini ya sheria zilizotungwa na bunge bila ya kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa, Tarafa, Kata wala Serikali za Mitaa na mpaka sasa hataki majadiliano ya iana yoyote yanayohusu haki za wananchi hawa. Je huu ndio mfano wa kiongozi bora mnayemtaka? Viongozi kama hawa Mwalimu Nyerere alisema hawafai hata kupewa Ujumbe wa ]

Hivi wakati maghufuli anaagiza kupanda mawe na mabango yanayoonyesha road reserve ni 120m Je hakuna sheria iliyomwongoja na kwamba alikuwa anabuni tu mwenyewe? Je unaujua mpango mzima wa fly overs utakavyokuwa na kuwa MT10 tu zinatosha.

Hata hivyo, siwezi ku argue kwenye sheria kwani zinahitaji utafiti wa kutosha.
 
Sioni shida Maguli anatufaa kwa tabia yake ya kufuata sheria. Sheria haina kufikilia. Katika sheria unaifuata ilivyoandikwa. You dont care about consequences! Magufuli anaweza akawa msemaji mzuri bila madaraka lakini kama ukimya wake unampa nafasi ya kuwa waziri na hatimaye kutimiza malengo ya kufuata sheria...huenda hiyo ni dream yake...sioni tatizo
 
TATIZO HAPA MAGUFULI ANATUMIA SHERIA ZILIZOISHA UHAI KUTAMBUA UPANA WA HIFADHI YA BARABARA. HIFADHI YA BARABARA ILIKUWA NI MITA 22, MWAK 2009 IKAONGEZWA KUFIKIA MITA 30 KWA MUJIBU WA IBARA 27 (2) YA KANUNI ZA SHERIA ZA BARABARA ZA 2009, WAZIRI AKITAKA ARDHI YOYOTE KUWA SEHEMU YA BARABARA AU HIFADHI YA BARABARA ANATAKIWA KUWASILIANA NA WAZIRI WA ARDHI ILI ENEO HILO LIWEZE KUTENGWA HIVYO MWAKA 2009 UPANA WA HIFADHI YA BARABARA ULIPONGEZWA KWA MITA 8 KUTOKA MITA 22 HADI 30 KILA UOPANDE NCHI NZIMA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA BARABARA.

Mkuu attachment yako in road width tu hamna roadreserve!
 
Magufuli sio mtu anayefuata sheria hata kidogo, anatumia kauli mbiu ya "sheria" kujijengea umaarufu tu, kwa kuwa anafahamu watanzania wengi ni wavivu kusoma sheria hivyo wataamini kauli aake kuwa ni waziri. Mfano hai wa Magufuli kutofuata sheria na kukandamiza hali za wananchi ni case ifuatayo:- Mwaka 1999 wakati inatungwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999, Magufuli alikuwa miongonji mwa wabunge walioipitisha. Kifungu cha 15 cha sheria hiyo kinatamka hivi UGAWAjI WA ARDHI ULIOFANYWA KWA MTU AU KUNDI LA WATU WAISHIO AU WALIOTAKIWA KUHAMIA NA KUISHI KATIKA KIJIJI WAKATI WOWOTE KATI YA 01 JAN 1970 HADI 31 DES 1977 , KAMA UGAWAJI HUO ULIFANYWA KWA MUJIBU WA SHERIA AU KINYUME CHA SHERIA AU BILA KUZINGATIA SHERIA YOYOTE, SASA INATHIBITISHWA KUWA UGAWAJI HUO NI HALALI NA KWAMBA DAIMA NI WENYE NGUVU YA KUTOA HAKI NA WAJIBU WA KISHERIA KWA KUNDI LA WATU WALIOGAWIWA ARDHI HIYO....." Aidh Kifungu cha 16 Kinatamka .......... MASHARTI YA KIFUNGU 15 YATATUMIKA KILA MARA UGAWAJI WA ARDHI YA KIJIJI ULIPOFANYWA NA HALMASHAURI YA KIJIJI AU MAMLAKA NYINGINE YOYOTE MNAMO NA BAADA YA 01 JAN 1978 HADI TAREHE YA KUANZA KUTUMIKA KWA SHERIA HII.

Wakati wa opersheni vijiji miaka ya 1970's maenEo kati ya Ubungo hadi Kiruvia pia vilianzishwa vijiji vya Kimara, Mbezi Kibamba na Kiruvia ambavyo vilibadsilishiwa hAdhi na kuwa chini ya Mipango Miji mwaka 1985. Kwa mujibu wa vifungu vy sheria iliyotajwa hapo juu ambayo Mhe John magufuli lishiriki kuipitisha wananhci wote waliokuwa wakiishi katika vijiji hivyo hadi mwaka 1985 wana haki na ardhi wanayoimiliki na kama Serikali inaitaka ardhi hiyo ni lazima kuwalipa fidia. Kwa maneno mengine ukisoma kwa makini maneno in bold sheria feki anazotumia Magufuli za 1930's na 1967 ziliisha uhai katika maeneo yaliyokuwa vijiji vya ujamaa kutokea mwaka 1999.

Kwa kuwa Mhe John Magufuli alifahamua kuwa Serikali huchulewa kuchapa, kusambaza na kutoa elimu kwa wananchi ya sheria mbali mbali zinazopitishwa na bunge kutoakana na ukosefu wa fedha, mwaka 2000 alipochaguliwa kuwa waziri wa ujenzi kwa mara ya kwanza (ikiwa ni miezi michache baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo) bila huruma wala ubinadamu wowote Magufuli akaagiza kupandwa kwa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara Mita 120 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro pande zote mbili, kati ya Ubungo hadi Kibaha. Upana halali wa hifadhi ya barabara ni Mita 22 tu. Hata kama sheria ya vijiji ilifuta hata sheria ya barabara, kama Magufuli angekuwa amedea na Upana halali wa Road Reserve wa Mita 22 pande zote mbili kidogo wananchi wangeweza kumwelewa kuwa ana nia njema.

Hivyo Magufuli alitoa maagizo na kuwatendea wananchi mambo yaliyo kinyume cha sheria ya Ardhi ya Vijiji vifungu nilivyovitaja hapo juu. Na ili kuhakikisha wananchi kati ya Ubungo hadi Kibaha wanakosa haki yao kabisa kwa ubabe wake wa kawaidia aliingia katika ardhi na makazi halalai ya wananchi chini ya sheria zilizotungwa na bunge bila ya kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa, Tarafa, Kata wala Serikali za Mitaa na mpaka sasa hataki majadiliano ya iana yoyote yanayohusu haki za wananchi hawa. Je huu ndio mfano wa kiongozi bora mnayemtaka? Viongozi kama hawa Mwalimu Nyerere alisema hawafai hata kupewa Ujumbe wa shina.

Magufuli aliamua kuwatendea unyama huo wananchi wanaoishi kati ya Ubungo hadi Kibaha kwa kuwa alifahamu wananchi wana ufahamu mdogo wa haki zao chini ya sheria ya vijiji. Kutokana na kuwa na ufahamu mdogo wananchi wanaomiliki ardhi na makazi ndani ya eneo hilo walikaa kimya na kuathirika kijamii na kiuchumi kwa miaka 9 mpaka 2010 alipoanzsiha zoezi la kutaka kubomoa nyumba hizo kwa kisingizio cha kutekeleza mradi wa mabasi yaendayo kasi na msongamnao wa magari.

Cha ajabu upana unaohitajiwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi hauzidi Mita 10, mfano hai ni upana ulioachwa na jengojipya la Benki ya Wananchi ya Dar es Salaam (DCB) lililojengwa hivi karibuni pale Magomeni na ukarabati wa kusogeza nyuma uizo wa Chuo cha DIT. Kwa hali hiyo, Je ni kweli nyumba zilizoko Mita 100 kutoka katikati ya barabara kati ya Ubungo hadi Kimara Magufuli alizoagizi ziweweke alama ya X na kuagiza zibomolewe zinazuia ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasiau zinachanmgia vipi msongamano wa magari?

Ndio maana wakubwa wake wameagiza historia ya maeno izingatiwe na wananchi walipwe fidia kama kuna hajaya nyumba kubomolewa.

Kuhusu Magufuli kusemwa hadharani ni haki yake kwa kuwa Gazeti la Tanzania Daima liliripoti kuw kabla ya Waziri Mkuu kumsema hadharani alimwita na wakakaa mara mbili kuhusu suala hilo lakini Magufuli akakaidi na kutunga msamiati kuwa ameapa kulinda sheria. Hivuo ili kulinda haki za wananchi na kulinda serikali ili ni lazima ashughulikiwe kidogo.

Ndugu, huu ndio pembuzi yakinifu. Hapa jamvini tunataka hoja zenye data na siyo ushabiki usio na maana yoyote. Umewajibika kwa kiwango cha juu kama watu watawajibika kama hivi basi jamvi litarudisha heshima yake ambayo naona inaporomoka kila kukicha kwa sababu za ushabiki. Big up Jatropha. kama kuna mtu anapinga hoja zako aje na hoja nzito siyo tetesi, uongo na hisia - Ufisadi
 
Mkuu attachment yako in road width tu hamna roadreserve!

Road width ndimo ndani yake kuna roads reserve. kwa kifupi ni kitu kimoja. Sema tu pia kuna sheria ya Barabara ya Mwaka 2007 ambayo imengeza upana wa barabara kutoka mita 45 kwenda mita 60 ukiacha barabara ya morogoro
 
Back
Top Bottom