Magufuli bila madaraka yukoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli bila madaraka yukoje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 23, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?

  Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?

  Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?

  Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?

  Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?

  Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:

  a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.

  b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.

  Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:

  a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.

  b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

  my two cents plus the other fifty
   
 2. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Kuna tetesi zipo kwamba Mkuru anataka kumuweka huyu jamaa kwenye kitengo kingine....More info zitamwagwa hapa jamvini bila shaka!!
   
 3. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Magufuli bado namfagilia kwa ushupavu wake wa kusimamia sheria kwa vitendo. Suala la je, anapokuwa hana madaraka yukoje, to me is irrelevant. Kwani kuna mijitu ndani ya serikali ya kifisadi ya ccm imepewa madaraka yote lakini imekaa kimya na kuacha nchi inachezewa kama haina mwenyewe. Kikwete anamweka magufuli madarakani kwa kinyongo.

  Anachoogopa ni kunyoshewa vidole na watanzania endapo ataamua kumwacha kwa sababu utendaji wake wa kazi hakuna mtanzania asiyeujua. Aliwahi hata kumtia ndani kiongozi mmoja wa ccm kwa kukutwa na kokolo ya kuvulia samaki kwenye bwawa la nyumba ya Mungu.
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Tuangalie kwa ufupi. Huyu bwana alipoingia bungeni ulikuwa wakati wa Msekwa ambapo bunge lilikuwa mhuri tu na haikuwa rahisi sana kujua wapiganaji kwa uwazi hasa ukiwa ndani ya chama. Halafu akawa waziri jambo lililombana zaidi.

  Kurudi kwake bungeni tena bila kupingwa ni ishara ya kuwa wapiga kura wake walikubali kazi yake, na hiyo inamjengea hoja kuwa japo si msemaji ni mtendaji. Kama ni kweli au si kweli wananchi wa Chato wanamajibu sahihi.

  J.P Magufuli ni kiongozi ambaye ametuonyesha mengi yaliyowashinda wenzake.mambo. Anaifahamu vizuri kazi yake na yupo tayari kusimamia sheria zetu wenyewe hata kama ni za kurithi kutoka kwa mkoloni.
  Kukubalika kwake kunatokana na kufuata kanuni, sheria na mipango. Kwanfano aliposimamia ujenzi wa bara bara, ile ni sehemu ya kutumia na kuendeleza rasilimali za taifa. Alipotuonyesha kuwa tumelala na watu wanavua samaki karibu na kigamboni alisimamia rasilimali za taifa.

  J.P.M anaposema ujenzi haramu ndani ya hifadhi za bara bara anasimamia matumizi ya kile kidogo tulicho nacho kwa manufaa yetu sote,kwa kuzingatia sheria tulizozikubali sisi wenyewe na kumkabidhi azisimamie.

  Kitendo cha viongozi wa juu kumsema mbele ya mikutano ni ukiukaji wa kanuni za uwajibikaji wa pamoja 'collective responsibility'. Sijui kama PM au Rais wameshindwa kuwasiliana naye faragha hadi kusimanga hadharani.

  Viongozi wanajali kura zaidi na si sheria walizoapa kuzisimamia ' cheap popularity'. Utamaduni uliotufikisha mahali wizi, ubadhirifu na ufujaji ni sehemu ya uongozi.

  La kushangaza,ni kitendo cha J.P kutojiuzulu. Kanuni za utawala bora zinasema kunapokuwa na tofauti za mitazamo wazi kiongozi anatakiwa ajiuzulu.
  Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri hata kama si msemaji wa wazi kama
  mbunge, sijui anasubiri nini na kama anataka kuwa malaika ndani ya kundi la wahalifu.

  Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.
   
 5. m

  mzambia JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hawezi simama peke yake bila ya uwaziri kwani hana ujasiri kama wa kina selelii, lembelii na hata akina ole sendeka ktk kusimamia maslahi ya tz ila akipewa rungu(uwaziri) utasikia wavuvi haramu, bomoabomoa, zuia magari ya serikali na mengineyo.
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mkuu sana MM kila timu ina aina yake ya uchezaji na namna ya wachezaji kushirikiana,mathalan kuna kipindi bwana mdogo Rooney wa Manchester United (sio mshabiki wa timu hii) aliingia kwenye mgogoro na mwalimu wake kwa kua alitaka kucheza kwenye nafasi aliyoona inamfaa wakati mwalimu akitaka acheze pembeni!

  Mwisho wa msuguano huo ni kwamba ilibidi afuate matakwa ya mwalimu na kuomba radhi kwa yale aliyosema wakati akiwa na ghadhabu!...nachotaka kukuaminisha ni kwamba Dr Magufuli ni mtendaji wa kawaida tu pasi kua na madaraka makubwa na akiwa na madaraka makubwa seem anasahau wigo wake! Ni kibwagizo kizuri kila anapoingia kiutendaji kwa muda mfupi kwenye kitengo fulani anamfunika hata yule aliyemweka kwenye kitengo japo kiitifaki aliyemweka ndo alistahili kuonekana!

  Binafsi nasubiri kuona mwisho wa sinema hii nzuri ya kupendeza!
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Inaonyesha hana ubavu wa kujiuzulu, na hii ni bahati mbaya sana kwake - kwa vile itakuwa vigumu sana kwa yeye kufanya kazi kimakini kwa vile ataogopa mawazo ya waziri mkuu na raisi kila akitaka kuchukua hatua.
   
 8. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Binadamu tumetofautiana sana.kuna watu wanaweza kuhoji wakiwa tu hawana madaraka pindi wakiyapata huwA KIMYA.kuna watu wengine huwa kinyume chake.Nafikiri hapa cha msingi ni je alikuwa sahihi kwenye yale aliyofanya akiwa madarakani?kama alikuwa sahihi apongezwe kama hakuwa hivvyo atalaumiwa.
   
 9. T

  Tom JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa mfano kama ni kweli Magufuli alitaka Jengo la TANESCO-UBUNGO libomolewe, ilibidi afikirie kua lile jengo limejengwa kwa pesa yetu na ujenzi uliidhinishwa na Mawaziri husika walikokuwepo kabla yake Magufuli kwenye wizara hiyo. Likibomolewa leo, kesho kuna uwezekano atakuja waziri mwingine anayembadili Magufuli na akaidhinisha ujenzi tena katika sehemu hiyo - sasa utaona kua sisi ndio tunaliwa tokana na maamuzi ya kibabe toka kwa hao mawaziri wa CCM.

  Magufuli angetufaa sana kama angesimamia na kuwakaba walioidhinisha ujenzi wa hilo jengo. Pia atatufaa kama atadhibiti ujenzi holela unaoendelea kukua na hapo hapo kupigania raia kupata viwanja vilivyopimwa haraka - bomoa bomoa is too easy kumpa sifa Magufuli. Vilivyofanywa kwa makosa na wenzake kabla yake, basi na waadhibiwe kwanza ili makosa yasirudiwe.

  Kimsingi Magufuli si kiongozi mzuri, anafanya mambo kama kuruta - utafikiri amekatazwa kufikiri.
   
 10. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndg zangu,
  Sidhani kama Magufuli ana sababu ya kujiuzulu kwa kuwa tunahitaji kuwa na viongozi wenye mitazamo hasa na chanya kwa pamoja ili mawazo yao yanapogongana na kutofautiana right decisions may happens, pia wananchi tutajua nani yupo kwa maslahi ya bwana wakubwa, nani yupo kwa maslahi ya wananchi na kusimami sheria za nchi.

  Kwa maelezo haya mafupi nadhani bado serikali ya JK inawahitaji sana kina Magufuli, Sitta, Mwakyembe na wapiganaji wengine, kuna usemi mmoja unasema "If you cannot fight your enemies then join them" kujiunga nao haimaanishi umeshindwa bali utapata more opportunity ya kujua weakness and strength zao ili next time uweze kufight nao effectively.
   
 11. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndg zangu,
  Sidhani kama Magufuli ana sababu ya kujiuzulu kwa kuwa tunahitaji kuwa na viongozi wenye mitazamo hasa na chanya kwa pamoja ili mawazo yao yanapogongana na kutofautiana right decisions may happens, pia wananchi tutajua nani yupo kwa maslahi ya bwana wakubwa, nani yupo kwa maslahi ya wananchi na kusimami sheria za nchi.

  Kwa maelezo haya mafupi nadhani bado serikali ya JK inawahitaji sana kina Magufuli, Sitta, Mwakyembe na wapiganaji wengine, kuna usemi mmoja unasema "If you cannot fight your enemies then join them" kujiunga nao haimaanishi umeshindwa bali utapata more opportunity ya kujua weakness and strength zao ili next time uweze kufight nao effectively.
   
 12. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Magufuli pia namfagilia kwa kumpiga vijembe mkulu wa nchi, kwa kuhoji mbona amri kumi za mungu anavunja, wakati anajua zipo?
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Katika mapambano yoyote ya kikazi au kimaslah cha kwanza inabidi uwatambue maadui au walio tishio kwako. Waweke kwenye group moja ili iwe rahisi kuwa-monitor, then start actions.

  Hii ndio strategy ninayoiona kwa mkuu. Kwanza kawaweka JPM na Mwakyembe pamoja ili kuwa rahisi kwake kuhakikisha anawavuruga katika utekelezaji wa shughuli zao kama kuwanyima uhuru wa kufanya maamuzi ambao kimwongozo uko ndani ya uwezo wao maana ni kusimamia sheria za nchi ambazo hata mwananchi wa kawaida ana uhuru na wajibu wa kuzisimamia. Stategy ya pili anayotumia ni kutenga bajeti ambayo ni imposible kutimiza yale aliyoahidi, kuna tetesi kwamba pesa iliyopo sasa hivi haitoshi wala kujenga hizo flyovers alizoahidi itabidi watoe kwenye vyanzo vingine .

  Baada ya kuwa-frustrate wanajua kabisa kwa jinsi ya watu wa kalibha hizo wataresign. Na wkiresign sasa hivi hadi kufikia 2015 wtakuwa wmeshasahaulika so mission will be accomplished easily, then EL kama kawaida atakuwa President. Ndio maana ukiangalia EL anajitahidi sana kuwa active hata kwenye majukwaa ambayo hukutegemea anaweza kuwepo eg kupiga mistari makanisani.

  Kwa hiyo JPM kujiuzuru itakuwa amefanya walichotaka maana script imeshaandikwa wanachofanya ni actions tu. Ninachoona JPM should Not and Never do what they expected him to do. Asiwape satisfaction ya kujiuzuru mapema hivi. JPM na Mwakyembe wanatakiwa waje na mbinu mpya ya kumweleza mkuu kwamba some people got brains from their mother, its a born thing.( Type Y people)

  Haya mambo hata makazini yanatokea unapigwa vita bila sababu ili uondoke maana watu wanahofia utachukua nafasi zao. Mimi naona angalau tu-support mtu mtu ambao supposedly anaonekana antenda kazi angalau kwa miaka hii mitano wakijenga hata Km 200 za lami ni nafuu kwa wanachi kuliko aondoke afu zijengwe km 20.

  Kuhusu PM, sioni cha kumjadili maana alishaproove beyond reasonable doubt kwamba yy ni toothless and clawless dog, he ca even kill a fly. Kukiri hadharani kwamba mafisadi wana nguvu kuliko serikali, kukubali kwamba uwanja wa Nyamagana ujengwe hotel, kwa haya mawili mie nilimsamehe bure.

  Kwa hiyo JK na his team wamejipanga kuliko maelezo na usipokuwa makini kama hawakutaki unaweza ondoka na kuwaachia wajitawale watakavyo.
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Magufuli ni wa ajabu kidogo kwangu. Amewahi kusimamia kwa nguvu zote uuzwaji wa nyumba za serikali. Atwambie hii nisheria ipi alikuwa anasimamia.

  Juzi hapa kashikilia mabango yote yaliyoko pembeni mwa barabara za TANROADS yaondolewe. Hajatuambia ni sheria ipi alikuwa anasimamia. Mabango haya mwaka jana yalisheheni picha za kampeni za bosi wake JK na yalikuwepo tangu akiwa wizara hiyo enzi za Mkapa. Anajua sana kucheza na vyombo vya habari na hasa TV.

  Kwa hili hana tofauti na Lowasa.
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Kwa CCM uongozi sio utumishi bali ni ajila, sasa mnapotegemea magufuri ajiuzulu mimi nawashangaa, mtu kutoka CCM atajiuzulu tu pale atakapokumbwa na kashfa kubwa na shinikizo la umma kuwa kubwa, hapo ndipo unapoweza kusikia kiongozi kutoka CCM anajiuzulu na si vinginevyo, CCM ingekuwa kwao uongozi ni utumishi basi hata Mkwere hasingegombea hii term ya pili ili aangalie afya yake kwanza maana ni mgonjwa, na hilo haliitaji vipimo vya maabara, kwa macho tu anaoneka afya iko mushkeli licha ya kunywa kikombe kwa babu Loliondo.
   
 16. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nakushukuru ndugu yangu kwa uchambuzi wa suala limhusulo ndugu yetu Magufuli. mimi naogopa sana kuona waziri ambaye wananchi wamemwamini kwenye maeneo mengi kushindwa kuchukua wajibu wa maana kiasi cha kujiuzulu baada ya blows za nguvu za viongozi wake wakuu...hii ina maana kuwa Magufuli haaminiki na hawezi kuchukua maamuzi magumu wakati inapobidi kwa kuhofia kitumbua chake. Kama kweli Magufuli ni mzalendo alipaswa kutuonyesha wananchi kivitendo kuwa ni mzalendo kwa kukataa udhalilishaji mara mbili wa viongozi wake kwa kujiuzulu. Vinginevyo Magufuli hana sababu ya kuaminika kwa namna yoyote na watanzania.
   
 17. Bless the 12

  Bless the 12 Member

  #17
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yeah ninakubaliana na uchambuzi huu. Kwa mtazamo wangu JPM anahitaji kuchagua kati ya mawili :

  1. Afanye kazi kwa kuzembea kila kitu mpk ifikie mahali wizara iyumbe ili awafunze adabu, AU
  2. Kuwa jasiri na kuendelea kujiuzulu.
   
 18. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #18
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ngoja nimcheck Dmitry Medvedev nitarudi..............
   
 19. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji uchambuzi wako ni sahihi na mzuri sana. Kiongozi unatakiwa uwe situational, kwani utekelezaji wa sheria lazima uambatane na kuzingatia ubinadaamu, tatizo kubwa la Mh. Pombe ni mtalaamu wa kutumia Public press!!! Na nakuambia umakini wa kiongozi hujulikana pale ammbapo kuna matatizo, mfano mdogo ni zoezi la wavuvi liliendeshwa kwa kutokuwa na mkakati maalumu wa kutoa elimu kwa wavuvi ili wao waone umuhimu, pia kuangalia njia mbadala ya kuwawezesha ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku. Bahati nzuri watanzania siyo kama waarabu, lasivyo kwenye zoezi la wavuvi watu wengi wangejimwagia petrol.
   
 20. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Hawezi kujiuzulu kwa vile hajavunja sheria.

  Wajiuzulu wale wasio na uthubutu wa kuifanyia jamii ya Wanzania chochote, hasa kwenye kutoa maamuzi magumu kama Mwakyembe na mawaziri wengine. Hawa wamewafanyia nini Watz tangu wachaguliwe hadi leo? au ndio mpaka wapewe order ya nini cha kufanya ndio wafanye? ili wasionekane wamekosea? Waoga?
   
Loading...