Uchaguzi 2020 Magufuli ampa maagizo Waziri Jafo kupeleka bilioni 5 Uvinza ili kuokoa jahazi

Hizo pesa ni rushwa na zinatolewa kuwarubuni wananchi tu
Kusema kweli CCM na serikali yake ni wezi wakubwa. Walizibana hizo pesa alafu walipo banwa na wananchi, wanazileta kama rushwa ili wapewe kura.

Watu wa uvinza hiyo ilikuwa haki yenu mliyokuwa mmenyang'anywa, hivyo pokeeni barabara, kura kwengine.
 
Kuna mahala kuna shida, kwa nini wakati huu? Je, nec wanaona ni sahihi? CC : Kaijage
 
Nashangazwa sana mambo haya,Mgombea anatoa maelekezo kipindi hiki cha kampeni?!utafikir yuko kwenye ziara ya kiserekali,NEC wako bize kufuatilia Lissu kasema nini leo, kwa staili hii kukitoa madarakan chama hiki ni ngumu sana
Haya ndo mambo yatakayosababisha vurugu huko mbeleni
 
Sawa, pamoja na jibu lako, ungejibu maswali niliyouliza ingependeza zaidi.

Hao wananchi wasingeulizia, hizo pesa zilikuwa ziende wapi?

Kwa nini kama hizo pesa zilishatolewa, hazikupelekwa kwa wakati husika?
Kumbe unamfuatilia kila anapofanya kampeni zake...nami nimemsikiliza leo akiwa hapo Uvinza..inaonesha hiyo barabara ya kilometa 10, ilitengewa milioni mia 5 kwa ujenzi wa kilometa 1 tu ya lami kwa mwaka huu..(itakuwa lami hafifu sana bila shaka)..baada ya mgombea kusikia hivo ndo akajigeuza gafla kuwa Rais na akaagiza ziletwe bil.5 ili kilometa zote 10 zikamilike mara moja.

kwa hiyo kusema kuwa zilitengwa wananchi wamepiga kelele ndo zikaagizwa kuletwa,ni kuwasingizia tu kitu ambacho siyo kizuri hata kama ni kampeni Labda hoja yako ingekuwa hizo bil 5 zinatoka wapi,ziko kwenye bajeti?

ila kutufanya wote wajinga hatukuelewa kilichofanyika ila wewe tu ndiyo mjanja ulielewa sana nikutokututendea haki.
 
Mjinga kabisa huyo muuza sura, halafu Eti kila mchango wenye muelekeo wa kiupinzani anaelekeza uwe kwa faida ya kiCCM. Muhuni mkubwa huyo.
Anafikiri humu kuna watu wenye akili fupi za kuongozwa na mwenyekiti kama huko CCM kwao.
 
Siasa za Africa ni shida sana

Hii inaonesha kuna usiri mkubwa sana kwenye fedha za budget zinazotolewa. Fedha zinatoka kwenye bajeti hii, alafu zinafunikwa, alafu zitakazo tolewakwenye bajeti nyingine ndizo zinatumika.
 
Hii inaonesha kuna usiri mkubwa sana kwenye fedha za budget zinazotolewa. Fedha zinatoka kwenye bajeti hii, alafu zinafunikwa, alafu zitakazo tolewakwenye bajeti nyingine ndizo zinatumika.

Mtu anatoa ela then anaomba kura dah hahaha
 
Katika nchi ambayo rais unaamua chochote na hakuna wa kukuzuia sio sheria wala taasisi, unashindwaje kazi hiyo kwa mfano?
Nadhani hata mwendawazimu anaweza kuongoza nchi hii. Si unakumbuka hii kauli.? "Nimemteua waziri kichaa kichaa kama mm kushughulikia uvuvi"
 
Back
Top Bottom