Uchaguzi 2020 Magufuli ampa maagizo Waziri Jafo kupeleka bilioni 5 Uvinza ili kuokoa jahazi

Kumbe unamfuatilia kila anapofanya kampeni zake...nami nimemsikiliza leo akiwa hapo Uvinza..inaonesha hiyo barabara ya kilometa 10, ilitengewa milioni mia 5 kwa ujenzi wa kilometa 1 tu ya lami kwa mwaka huu..(itakuwa lami hafifu sana bila shaka)..baada ya mgombea kusikia hivo ndo akajigeuza gafla kuwa Rais na akaagiza ziletwe bil.5 ili kilometa zote 10 zikamilike mara moja.

kwa hiyo kusema kuwa zilitengwa wananchi wamepiga kelele ndo zikaagizwa kuletwa,ni kuwasingizia tu kitu ambacho siyo kizuri hata kama ni kampeni Labda hoja yako ingekuwa hizo bil 5 zinatoka wapi, ziko kwenye bajeti?

ila kutufanya wote wajinga hatukuelewa kilichofanyika ila wewe tu ndiyo mjanja ulielewa sana nikutokututendea haki

Sorry, sijakuelewa unachotaka kusema/kumaanisha. Naomba aliyemuelewa anisaidie.

Pili tafadhali sana husiniwekee maneno mdomoni. hilo la kuwafanya wajinga halipo kwenye uzi wangu, wewe ndo umekuja nalo, kwa hiyo hayo mengine ni wewe umeyaweka na si mimi.

Ni vizuri kujikita kwenye mada bila kubadilisha maneno ambayo yanaweza haribu maana halisi ya ujumbe uliokusudiwa.
 
Hii inaonesha kuna usiri mkubwa sana kwenye fedha za budget zinazotolewa. Fedha zinatoka kwenye bajeti hii, alafu zinafunikwa, alafu zitakazo tolewakwenye bajeti nyingine ndizo zinatumika.
Bajeti yake ipo kwenye bajeti iliyopitishwa bunge hili la June Cha ajabu Nini? Unataka bajeti iliyotengwa June isifanye kazi ?
 
Kufuatana na maadili na sheria za uchaguzi, hii siyo rushwa?
Kwa hiyo bajeti iliyopitishwa June na Bunge hutaki ifanye kazi? Wafanyakazi wasilipwe mishahara, suppliers wa serikali iwe vyakula mashuleni ,contractors nk wasilipwe Wakati pesa ilishapitishwa na bunge?
 
Bajeti kuu ikipita huwa kuna mafungu kama haya. Mnaleta hoja ambazo zinafanya Chadema ionekane haina watu makini. Zilikwapuliwa na nani? Tumia akili.
Kenge umejiingiza ndani ya msafara wa mamba eeh? Lile fungu la 1.5Tn ambalo Prof Assad akiwa CAG alilinyooshea kidole ndilo muda hutumika kama vile ambavyo Mheshimiwa atakabyoona inamfaa. mungu oyeee!
 
Hao waliokuwa wanatunga sheria za uchaguzi hawakujua kuna wakati rais anaweza kuwa mgombea? Hivi unajua unachoongea au unaleta utoto hapa?
Kwa hiyo ametamka natoa bil tano ili mnipe kura? Wananchi wametoa kero juu ya barabara akatumia nafasi ya urais kuitatua kamanda. Tuache mambo ya kitoto.
 
Mlitaka ampe maagizo Lissu, kwani yeye si ndiye Rais wa nchi hii sasa tatizo ni lipi akitimiza wajibu wake?
 
Hii ni rushwa. Kampeni zimemshida!!
Inamaana sisi kupata hayomaendeleo mpaka wakati wakampeni mtu akiwa kabanwa kama hivi mimi haponaona lisu kwakushirikiana nawananchindio katupa hizo b 5 ameona kule mamtwara kaskazini nakusini mambeya huko halisionzuri ndio amekumbuka kujiimarisha huku magharibi Hatumtaki alichoma nyavu zetu halali kabisa nakuteka engiene zetu atwambie kwanini alichoma nyavu ambazo zinalipa leseni?
 
Back
Top Bottom