Earthmover
JF-Expert Member
- Sep 28, 2012
- 25,975
- 25,288
.....
....eeeeh nguvu ya mamba iko kumayi sasa kumayi kauka
....eeeeh nguvu ya mamba iko kumayi sasa kumayi kauka
Ukipita mtaa wa Lumumba utamke hayo maneno utapata shida sanaIli uthibitishe haya maneno yako kuwa Magufuli kachuja au lah nenda mtaani alafu ukikuta kikundi cha watu tamka haya maneno kuwa "Magufuli hafai".. Kitachokutokea kutoka kwa wananchi usisite kuja kutuambia ata kama ukiwa ICU.
Sasa rais mwema alisema atayageuza yaishi kama mashetaniMimi naona kauli hii ya JPM imekaa kinyume. Nadhani majizi, mafisadi, wahujumu uchumi ndo Mashetani. Malaika ni wapole na hawaibi na si mafisadi. Sasa taifa la mashetani ni zuri kweli? Naona taifa la malaika ndo linafaa kuishi.
Ili uthibitishe haya maneno yako kuwa Magufuli kachuja au lah nenda mtaani alafu ukikuta kikundi cha watu tamka haya maneno kuwa "Magufuli hafai".. Kitachokutokea kutoka kwa wananchi usisite kuja kutuambia ata kama ukiwa ICU.
EL hajachuja mpaka sasa
....Ukipita mtaa wa Lumumba utamke hayo maneno utapata shida sana
....Mimi natumia matikiti mkuu.
Heshima kwako mkuu. Hii ndiyo hoja yenyewe; hakuna cha kuongeza. Wanaosherehekea Magufuli kutengenezewa "personality cult" wajiandae kuhuzunika muda si mrefu. Kwa kifupi, hao ndio maadui zake wakuu wanaomharakisha kujiunga na safu za marais wengi hapa Afrika na dunia ya tatu wanaoaminishwa kuwa wao pekee ndiyo dola "L'etat? C'est moi!".
Hata Marekani walijaribu kumkuza George W. Bush kihivyo (asiyekuwa nasi yuko dhidi yetu). Hadi leo wanajutia kwa sauti na kimyakimya adha alizowaletea kwa kadhia zisizo na mantiki alizoasisi huko Iraq, Libya, n.k. Wakati ule ukikosoa maamuzi yake (na ya gwiji Dick Cheney) ulikuwa ukibandikwa nembo ya adui wa taifa la Marekani.
Alipokuwa kule Arusha (kama wiki mbili zimepita) alisema kuwa wabadhilifu wa Sukari anawajua na majina anayo. Hiki ni kichekesho sana, sasa kama unawafahamu kwa nini usiende kuwakamata, kama sio mambo ya kinafiki ni nini sasa hiki?
Akaenda mbali zaidi akasema"wameficha sukari Mbagala" mazombi wake wakaenda huko, waliporudi wakasema ile sukari inamilikiwa ki halali, kodi imelipiwa na haina shida... Jamaa akaumbuka.
eti mazombie yake mkuu umenifurahisha sanaMkuu naomba tujadili ishu ya NIDA
Nadhani unakumbuka kuwa Mtendaji mkuu wa NIDA (Dickson Mwaimu) pamoja na wasaidizi wake 3 walisimamishwa kazi kutokana na kile Magufuli alichodai ni ubadhilifu.
Sasa jiulize, kesi ya hawa watu hipo katika mahakama gani, ni kitu gani kinachofanya hadi leo wasifikishwe mahakamani, ni uchunguzi gani unaofanyika mwezi wa 4 sasa.
Huu ni mfano mmoja tu.
Je unakumbuka kesi ya wale jamaa wa TRA? Umeshajiuliza mbona haisikiki tena?