Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Mkuu naomba tujadili ishu ya NIDA

Nadhani unakumbuka kuwa Mtendaji mkuu wa NIDA (Dickson Mwaimu) pamoja na wasaidizi wake 3 walisimamishwa kazi kutokana na kile Magufuli alichodai ni ubadhilifu.

Sasa jiulize, kesi ya hawa watu hipo katika mahakama gani, ni kitu gani kinachofanya hadi leo wasifikishwe mahakamani, ni uchunguzi gani unaofanyika mwezi wa 4 sasa.

Huu ni mfano mmoja tu.

Je unakumbuka kesi ya wale jamaa wa TRA? Umeshajiuliza mbona haisikiki tena?
funika kombe...
 
kuzuia vibali vya sukari pasipo kuitathimini na kuibua Richmond mpya ya sukari sasa.
Alipokuwa kule Arusha (kama wiki mbili zimepita) alisema kuwa wabadhilifu wa Sukari anawajua na majina anayo. Hiki ni kichekesho sana, sasa kama unawafahamu kwa nini usiende kuwakamata, kama sio mambo ya kinafiki ni nini sasa hiki?

Akaenda mbali zaidi akasema"wameficha sukari Mbagala" mazombi wake wakaenda huko, waliporudi wakasema ile sukari inamilikiwa ki halali, kodi imelipiwa na haina shida... Jamaa akaumbuka.
 
Mwanzoni mwa utawala wake ilikuwa kila gazeti linamwandika yeye tena vizuri. Vijiwe vyote kuanzia vya kahawa, daladala, bar na maofisini story alikuwa ni yeye tena watu wakimsema kama malaika mkombozi.

Ghafla upepo ukabadilika, watumishi wakaanza kukosoa utumbuaji majipu, wafanyabiashara wakakosoa mbinyo wake kwenye kodi, wanasiasa wakahoji style yake ya uongozi. Wananchi wa kawaida wakanigwa na maisha magumu (ingawa hawa bado wamebakiza kaimani fulani). Vyombo vya habari wanalalamikia kuminywa uhuru wao.

Kiujumla upepo unavuma vibaya kwa JPM naye ameshakiri ugumu wa kiti chake mpaka akasema angejua asingegombea urais. Je, rais wetu amekosea wapi mpaka hali imegeuka mapema hivyo?


Amekosea kujitanabahisha kichama na kusahau kwamba raisi ni utumishi wa taifa na si wa CCM. Anachuja kwa kasi kwa sababu anavyozidi kujizamisha ki CCM ndivyo anavyozidi kuuvaa uhusika wa CCM ambaye ndiye adui mkubwa wa Watanzania waliofariki, waliopo na watakaokuwepo. CCM ni adui mkubwa zaidi ya ujinga, umaskini na maradhi, na hakuna mtu atakayejitanabahisha kulinda maslahi ya adui CCM, atabaki kuwa mwema kwa watanzania wenye mateso yasiyosemekana!.

Angetaka kuendele kung'ara, angekaa kwenye nafasi ya raisi ajenge nchi lakini si kusimamia maslahi haramia ya CCM halafu bado Watanzania waendelee kumwamini!.
 
Tunaangamia kwa kukosa maarifa tatizo ameshindwa kutumia hekima na busara na muda mwingi anapambana na kivuli chake na pia gharama ya kukulinda chama cha mapinduzi ni kubwa sana Kama anataka kufanikiwa lazma aanze kutengeneza msingi nchi ambayo ni katiba bora hayo majipu yanapasuka yenyewe kupitia katiba na cyo mbwembwe za kwenye TV
 
Ameharibu uchumi na anadhani kutumbua watu ndo dawa ya kuboresha maisha.EL aliwaambia watu kua kutakua na mvumo mkubwa(hang over) ya shangwe lakini zitazima ghafla na kwamba haoni future nzuri ya uchumi siku za usoni kwa vile mkuu wa kaya hana maono na leadership skills miezi 6 tayari.Kwa maoni yangu we should build strong instituitions badala ya kutegemea utashi wa mkuu wa kaya.
 
Hebu mtoa thread achunguzwe kama sio jpu anategemea majip kuisho mjin
 
Nimekupata mkuu.

Ule ni udhaifu wa kukusa Leadership Skills. Kama Leader hakutakiwa kabisa ku act namna hile.

Kwenye Leading and influencing hatushauriwa tuwe tunawa reprimand subordinate wetu mbele ya halaiki ya watu - hilo ni moja, pili waziri Mahiga hakuwa na kosa lolote alilolifanya yeye kama yeye, yale yalikuwa ni mambo ya mkewe kugombana na traffic, sasa kwa nini umfokee waziri wako mbele ya umma? Je ulishindwa kumsema mkiwa wawili?
We have leaders and subordinates. Some people were just meant to be led, given orders, carry them out and give feedback. As a minister he was an exceptional figure, a symbol of workmanship but as the president all tht will come into question and the effect is what we are seeing right now. Come two years watanzania wote watakuwa wanalia vilio tofauti na hapa kazi tu. Mark this it wont even be the citizens that will prove his incapabilities as a leader, it will be his own subordinates who are day in day out reprimanded and humiliated publicly. As they say a disgruntled worker leads to a bunkrupt boss...............
 
Huwezi kuendesha nchi kwa ufanisi ukitengeneza sifa binafsi. Tatizo la kupenda sifa sana ndilo linaiangusha serikali hii, kukosolewa ndio nafasi nzuri ya kuendesha mambo smoothly. Awamu ya nne pamoja na ubovu wake wote lakini ile hali ya kukubali kusemwa hadharani ilikuwa inawapa watu nafasi ya upunguza machungu yao.
Magu kaona Nape anafunga magazeti, anazuia matangazo ya Bunge na anakataa kusemwa akadhani itamsaidia lakini inammaliza kabisa, miezi sita hali iko hivi jee miaka miwili?
 
Huwezi kuendesha nchi kwa ufanisi ukitengeneza sifa binafsi. Tatizo la kupenda sifa sana ndilo linaiangusha serikali hii, kukosolewa ndio nafasi nzuri ya kuendesha mambo smoothly. Awamu ya nne pamoja na ubovu wake wote lakini ile hali ya kukubali kusemwa hadharani ilikuwa inawapa watu nafasi ya upunguza machungu yao.
Magu kaona Nape anafunga magazeti, anazuia matangazo ya Bunge na anakataa kusemwa akadhani itamsaidia lakini inammaliza kabisa, miezi sita hali iko hivi jee miaka miwili?
point
 
Nadhani utakuwa unachuja halafu hujielewi Kama unachuja
 
Wananchi walikua wanashangilia mwisho wa Siku maisha mtaani yamekua magumu zaidi kuliko hata Kipindi cha Kikwete. Naona Sasa Zile sifa na mapambio zimegeuka na kua kilio ndio maana umaarufu unazidi kupungua
 
Hiv ni nani aliyesema atakayekuja iangusha CCM atatoka CCM. Mi naic kma unabii umekamilika.
TB Joshua alikuja Tanzania akatembea peku....kibiblia hii ni mbaya sana.....ni sawa na wale manabii waliovaa magunia kulaani wafalme ambao baadae falme zao zilipigwa mapigo makali
 
Ni lazima mbegu ifukiwe kwanza ili kuweza kuchipua tena, safari bado inaendelea ngoja tusubiri muda sahihi wa kutoa hukumu
 
Back
Top Bottom